Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Huwezi ukaacha kujenga reli, ukasema hii hela naenda kupandisha mishahara

Tatizo wao wanataka tuongeze sent ila sie twapunguza paye percentage tu so ni njia indirect ya kuongeza mshahara.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Mnafanya yale tusiyowaomba lakini kile tunachoomba hamtupatii,Mtoto wako akikuomba mkate wampa jiwe?
Tukiomba ajira mnanunua ndege,tukiomba Tume Huru mnatuletea askari wa jeshi LA akiba na kukata Majina ya wagombea nchi nzima?
CCM MNA tatizo gani hasa?Tumewakosea nini?
 
Ila hela ya kuwalipa wabunge million 200+ kila m'moja kama pension ndani ya masaa 24 mara baada ya kuvunja bunge ipo, ila wazee waliotumika maisha yao yote pesa hamna mpaka wengine kupata matatizo kiafya na wengine kufariki kabisa, hii laana haitawaacha salama.
 
Wafanyakazi kazi kwenu kuamua kusuka au kunyoa.
 
Kwa ufupi ni kwamba ikiwa wafanyakazi wakimpa kura huyu mtu ni kisaini mitano tena bila nyongeza.
 
jiandae siku zenu zaja kibri na madhalau hayajawai kumuacha mtu salama ,ccm mna madhalau sana na kibri cha kiwango cha rami , kuongeza mishara ya wafanyakazi ni shida but kuna pesa kibao mnatumia kwenye mambo ya ajabu , ajabu , mtanyooka nawambieni mungu ni wetu wote na hatamuacha mwanae hata mmoja ahangamie kwa kibri na madhalau ya ccm
 
Kwa kuongezea kwenye hoja hiyo, upinzani haujui maana halisi ya maendeleo.

Je, Bunge au Taasisi zozote zinapopanga fedha za maendeleo huwa ni maendeleo yapi kama siyo ya vitu?

Haki au uhuru hauna maana kama hakuna maendeleo ya vitu. Ubora wa maendeleo ya vitu katika usafiri (barabara na magari, viwanja vya ndege na ndege, bandari na meli) ndio unawawezesha wapinzani kuzunguka Tanzania (haki yao ya kufanya kampeni) wakitoa matusi na kuhamasisha vurugu.

Maendeleo katika vyombo vya habari (radio, tv, mitambo ya kuchapisha magazeti, mitandao ya kijamii, vifaa vya kupaza sauti) ndio unawawezesha wapinzani kusema hayo wanayoyasema (uhuru) kwenye kampeni.

Hakika upinzani umekwama kabisa kutafsiri "maendeleo" kiuhalisia.
 
Mgombea urais wa ccm amesema, hawezi kuongeza wafanyakazi mshahara na huku anajenga reli,elimu bure,miradi mikubwa kwa sababu na wafanyakazi watatumia hivyo vitu

Poleni wafanyakazi ,twende na Lissu

Wakulima na tuliojiari twendeni na Magufuli,kwasababu hivyo vitu vinafaida sana kwa shughuli zetu za kimaendeleo .
 
Hivi kuna anaejua mzigo wa kubebwa na reli mbili sgr na meter gauge utatoka wapi na ni tani ngapi kwa mwaka?
Tazara si imekufa kwa kukosa mzigo halafu tunaongeza central line ziwe mbili!
 
Sasa hawajapandishiwa Miaka Mi5 wanafunzi wanakaa kwenye madawati?

Sent from my POT-LX1 using JamiiForums mobile app
Miaka mi5 reli ya Magufuli bado iko Kibaha je wananchi wa Dodoma, Mwanza, Kigoma hawajajenga kwa kukosa usafiri?
Miaka mi5 Bwawa umeme la Stiegler's Gorge bado ni jangwa tu, je Mradi wa REA wa kuvipatia umeme Vijiji vyote nchini umekwama?
 
Miaka mi5 reli ya Magufuli bado iko Kibaha je wananchi wa Dodoma, Mwanza, Kigoma hawajajenga kwa kukosa usafiri?
Miaka mi5 Bwawa umeme la Stiegler's Gorge bado ni jangwa tu, je Mradi wa REA wa kuvipatia umeme Vijiji vyote nchini umekwama?
Ni Mradi wa Flyover ya Ubungo tu ambayo itaweza kukamilika ambapo pesa imetoka Afdb.

Miradi ambayo iko funded 100% na Serikali nina shaka kama itaweza kumalizika 100% by 2025.


Sent from my POT-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Yaani Magu anazingua ile mbaya, amedharau hata sheria za utumishi kwenye annual increment tu. Anahitaji sana kusaidiwa
 
Kwahiyo hajapandisha mishahara!Sasa mbona hapo anasema amepandisha mishahara???
Kama sielewi vile!
"Maendeleo hayana vyama"
.
.
"Msipochagua CCM siwaletei maendeleo"
.
Dr. Shika: (RIP) Tutaelewana tu !
 
Akikujibu niite
Tatizo lilokuwepo na bado lipo ni uongozi, utendaji, uwajibikaji.

Rais Magufuli alianza vizuri sana na akatengeneza mfano bora sana mwanzoni.

Matatizo yalianza pale aliposhindwa kumwajibisha Makonda. Hapo ndipo downfall ilipoanza.

Tumbua teua tumbua teua. Kila anayeingia anafanya yale yale.

Sent from my POT-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Nikimtukana humu jamvini!Melo na jamaa zake wananifungia jf!napigwa ban!!HONGERA JF KWA KUMPENDA JPM NAONA ANAWAPANDISHIA MISHAHARA KILA MWAKA!!!HAMJUI TUNAKOSA HELA YA BANDO NA TUNAJIBANA ILI TUKOMENTI HUMU JAMVINI??????NYIE NI MA CCM KIAINA!!!!
 
Huyu mzee anatuonaje yaani, anafikiri watoto wetu wanakula reli? Ni makosa yetu acha tuyalipie na kuyaishi ila Mungu ana mipango yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…