Kama asipopita Kaskazini kura zetu asahau..
Niwe mkweli kaskazini ndio sehemu JPM anakubalika zaidi kuliko kanda ya ziwa na dsm, nimepita kote huko nilikokutaja, arusha na moshi vijiwe vingi vinamzungumzia magufuli na miradi yake.
Jana nilikutana na wahudumu wa hotel wameacha shughuli zao wanamsikiliza kwenye runinga. Nikawaomba wapunguze sauti nina kikao online, aise walinishambulia, wananiuliza wewe ni chadema? Nikawaambia naomba tusemezane, kabla ya kwenda mbele mimi kamwe sijawahi kuwa mnazi wa chama cha siasa labda cha ushirika.
Nikawauliza mmesikiliza yooote aliyoongea magufuli na polepole kwenye runinga, naomba mmoja wenu anitajie katika yote yaliyotamkwa ni lipi amenufaika nalo au kulipata yeye kama yeye? Nikaona kimya, wakaniuliza kwani wewe kuna jambo gani magufuli amekufanya wewe kama wewe mpaka usimkubali? Nikawajibu tu kwa ufupi, mafao yangu, nyongeza zangu za mshahara kabla ya kustaafu, nanunua sukari robo kilo kwa familia ya watu 12 kutokana na bei. Sukari kwangu ni kwa ajili ya watoto tu wajukuu zangu wawili.
Baada ya kusema hayo nikarudisha swali langu kwao na kuwakumbusha hawajanijibu, wakaniambia sio lazima wapate wao kwani ni kwa ajili ya watanzania wote. Sikuridhika na jibu hilo, this time nikawauliza kama ni kwa ajili ya tanzania yote wao ni wakenya? Mbona hawajaguswa na hayo wanayosema ni ya watanzania wote?
Nilichokuja kuhitimisha ni kuwa this time Lema na timu ya Upinzani kaskazini this time wamepooza sana, wame underperform kwa kiwango kikubwa mno, haiwezekani kuruhusu wananchi wako wakapotoka kwa kiwango hiki mpaka kuwa rahisi kuwa trapped na propaganda nyepesi hivi za maendeleo ya uwanja wa ndege na barabara wasizozijua hata.
Lema mdogo wangu, ume underperform, nadhani hata Lissu ameamua asijishughulishe sana na kaskazini akiamini unanguvu ya kuwaelimisha watu bado lakini, umesinzia hakuna mfano, vijiwe vyote nilivyopita huku hali si nzuri kwenu, sio saluni, bar, sokoni mpaka kwenye dala dala.
Itoshe kusema upinzani this time mtaanguka vibaya kaskazini, msijipe matumaini yasiyokuwepo kwa kuangalia historia ya kaskazini. Shida kubwa nilioiona huku watu wana hofu kubwa mno ya kunyimwa maendeleo wakiendelea kuambatana na upinzani. Nimemaliza