Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Natamani kufika kila eneo kufanya kampeni lakini siwezi

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Natamani kufika kila eneo kufanya kampeni lakini siwezi

Ajitie ufundi akanyage Kusaini ndio atajua faida za dhaluma. Alichokiona Kagera anakiona machoni kabla hajakanyaga Kusaini.
Baki huku kwa praise team huko watakutoa busha awamu hii ujikute unavaa msuli bila kupenda.
 
Kwa walichomfanyia watu wa Mtwara ile mwaka jana hadi mzee magu akapoteza network hata ningekuwa mimi nisingekwenda , ila ningemtuma Benard Membe akaniombe kura za huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee: Hali ni mbaya kwakweli kwa nilichowafanyia watu wa kusini siwezi kwenda huko nimeona nimtume waziri mkuu akasaidie kuokoa jahazi

Campaign manager : sasa mzee ujue watu hawatakuelewa kabisa usipotokea hata kidogo

Mzee: Wewe hujui kitu wale wazee wakule wamenipania sana kuna siku walinitumia moshi nusura waniuwe, ngoja nizuge zuge hapa dar mpaka siku ziishe.
Dsm napo na hizi mvua hapakaliki, magu ana gundu sio bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikwete alipiga mizunguko yote na round zote nchi nzima. Kwamba yeye hakua Rais na hakua na kazi za kufanya?
Semeni tu ukweli.
 
😀Anaogopa korosho?
Anamtuma waziri mkuu?
Kwani kampeni ni kazi ya serikali?

Nimeamini trip shamba, trip garage!

Everyday is Saturday..............................😎
Kimsingi chuma kimeshatepeta. Starling TL kabakia mwenyewe kwenye Movie baada ya maadui zake wote kupoteana.
 
Kama asipopita Kaskazini kura zetu asahau..

Niwe mkweli kaskazini ndio sehemu JPM anakubalika zaidi kuliko kanda ya ziwa na dsm, nimepita kote huko nilikokutaja, arusha na moshi vijiwe vingi vinamzungumzia magufuli na miradi yake.

Jana nilikutana na wahudumu wa hotel wameacha shughuli zao wanamsikiliza kwenye runinga. Nikawaomba wapunguze sauti nina kikao online, aise walinishambulia, wananiuliza wewe ni chadema? Nikawaambia naomba tusemezane, kabla ya kwenda mbele mimi kamwe sijawahi kuwa mnazi wa chama cha siasa labda cha ushirika.

Nikawauliza mmesikiliza yooote aliyoongea magufuli na polepole kwenye runinga, naomba mmoja wenu anitajie katika yote yaliyotamkwa ni lipi amenufaika nalo au kulipata yeye kama yeye? Nikaona kimya, wakaniuliza kwani wewe kuna jambo gani magufuli amekufanya wewe kama wewe mpaka usimkubali? Nikawajibu tu kwa ufupi, mafao yangu, nyongeza zangu za mshahara kabla ya kustaafu, nanunua sukari robo kilo kwa familia ya watu 12 kutokana na bei. Sukari kwangu ni kwa ajili ya watoto tu wajukuu zangu wawili.

Baada ya kusema hayo nikarudisha swali langu kwao na kuwakumbusha hawajanijibu, wakaniambia sio lazima wapate wao kwani ni kwa ajili ya watanzania wote. Sikuridhika na jibu hilo, this time nikawauliza kama ni kwa ajili ya tanzania yote wao ni wakenya? Mbona hawajaguswa na hayo wanayosema ni ya watanzania wote?

Nilichokuja kuhitimisha ni kuwa this time Lema na timu ya Upinzani kaskazini this time wamepooza sana, wame underperform kwa kiwango kikubwa mno, haiwezekani kuruhusu wananchi wako wakapotoka kwa kiwango hiki mpaka kuwa rahisi kuwa trapped na propaganda nyepesi hivi za maendeleo ya uwanja wa ndege na barabara wasizozijua hata.

Lema mdogo wangu, ume underperform, nadhani hata Lissu ameamua asijishughulishe sana na kaskazini akiamini unanguvu ya kuwaelimisha watu bado lakini, umesinzia hakuna mfano, vijiwe vyote nilivyopita huku hali si nzuri kwenu, sio saluni, bar, sokoni mpaka kwenye dala dala.

Itoshe kusema upinzani this time mtaanguka vibaya kaskazini, msijipe matumaini yasiyokuwepo kwa kuangalia historia ya kaskazini. Shida kubwa nilioiona huku watu wana hofu kubwa mno ya kunyimwa maendeleo wakiendelea kuambatana na upinzani. Nimemaliza
 
Ana ogopa kuzomewa kama Kagera.
Moshi na Arusha tuna msubiri.

Futa hili mkuu, Moshi Arusha nguvu yake ni thabiti, amini nikwambiavyo, tuhimize timu ya kampeni ya upinzane wakaweke nguvu kule otherwise kuna aibu itatokea maeneo uliyoyataja while ni ngome ya wapinzani.

CCM imefanikiwa kuwajaza hofu ya kunyimwa maendeleo wakazi wa Arusha na Moshi
 
Subiri tarehe 28 kamanda utaelewa gari ya gereji ni ipi?

Lisu wako hafikishi hata asilimia 20. Najua utabisha kwakuwa umepumbazwa na ile mikwara yake na mafuriko ambayo hayaingii hata mara tano kwa mafuriko ya slaa achilia mbali haya ya juzi ya Lowasa.

Nilitegemea ungesema hayaingii kwenye mafuriko ya Magufuri, sasa unalinganisha mgombea wa sasa na mtu asiyegombea? Unakosa akili mwanaitikadi mwenzangu, unaniangusha.

Lissu anashindana na Magufuri sio na Slaa au Lowassa. Hatujatumwa hivi, @johnthebabtist nisaidie hapa ili tusimuache mwenzetu nyuma. Tumehimizwa kujenga hoja nzito ili kuzishinda imani za wananchi
 
Back
Top Bottom