Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Huwa sipendi kuendeshwa na mahaba. Napenda niendeshwe na akili yangu unayolala kwenye ukweli. Mahaba yafuate akili yangu.Mawazo ya mpumbavu nayo yaheshimiwe, wengi wanaompinga magufuli walizoea kupiga pesa. Ntakupa mfano wa Zitto Kabwela alipokuwa mwenyekiti wa ile kamati (jina kapuni) alianzisha ujenzi wa Ghorofa na alipotolewa ujenzi umesimama mpaka leo. Wote mnakumbuka alimwandama magufuli na akafikia kusema kama anataka amani basi amrudishe kwenye nafasi ya uenyekiti. Walioandika barua kuzuia Tanzania isipewe misaada ni wapinzani lakini matokeo wanamtupia lawama magufuli. Watanzania tuwe makini, wapinzani sio kwamba haajui Magu anafanya nini, lahasha, wanajua ana dhamira njema ila kutimiza majukumu yao ndio kelele hizo. Zamani bandari haikuwa ma mita za mafuta kwa hiyo mtu ndo alikuwa anaamua tu niseme zimepita lita kadhaa, huyu hawezi kumpenda Magufuli hata kidogo. Nchi kuijenga lazima pae na maumivu. Tuvumiliane.
Ukweli ni kuwa Magufuli, yapo mambo amefanya vema, na kuna mengine ameharibu.
Amefanya vema kukamilisha miradi iliyokuwa imeanzishwa na mtangulizi wake:
1) kusambaza umeme vijijini
2) kusambaza maji
3) kuendeleza ukarabati wa hospitali
4) Ukarabati na ujenzi wa mashule, mahakama, stand na masoko
5) Ujenzi wa barabara za mitaani
6) Ujenzi wa madarasa
Magufuli amefanya vizuri pia kwenye mambo yafuatayo
1) kusimamia vizuri matumizi ya fedha za serikali
2) kudhibiti ujambazi
3) Kusimamia nidhamu ya wafanyakazi
4) Uanzishaji wa masoko ya kuuzia madini
Miradi mipya mikubwa mitatu - reli, ndege na umeme, ni miradi mizuri lakini hii miradi inatumia fedha nyingi na haiwezi kujihudumia wala kuanza kurudisha fedha hivi karibuni. Miradi hii haikustahili kufanyika yote kwa pamoja. Kwa fikra zangu, angeanza na reli.
MAENEO AMBAYO AMEFANYA VIBAYA KABISA:
1) Ukatili kwa kutumia watu wasiojulikana kuteka, kupoteza na kuua watu. Hili ni kosa kubwa sana lusilostahili msamaha. Na siku moja ni lazima iundwe TUME YA MARIDHIANO ili tujue ni nini hasa kilimtokea Ben Sanane, Azory Gwanda, na tujue kwa nini walitaka kumwua Tundu Lisu, na wengine waliotekwa na kisha kutupwa maporini, na wale wengine waliouawa na miili yao kutupwa kwenye viroba
2) Kubambikia watu kesi za uhujumu uchumi na kutakatisha fedha, na kisha kuwalazimisha wakiri makosa baada ya kuwatesa kwa kuwaweka mahabusu kwa muda mrefu
3) Kufukarisha watu kwa kutumia sheria zisizo rafiki za TRA na uhujumu uchumi
4) Kuharibu mazingira ya uwekezaji kiasi cha kuua na kufukuza uwekezaji
5) Kutowajali wafanyakazi kwa kutowapa ongezeko la mishahara
6) Kutoheshimu utu na kuwaona watu wengine hawastahili heshima. Na yeye pekee na wateule wake kuwa ndio wenye mamlaka yasiyohojiwa wala kukosolewa
7) kutoheshimu katiba, sheria na kanuni. Kupalilia ubaguzi na kuendekeza upendeleo. Ili kudumisha upendeleo, badala ya kuheshimu taaluma, kila eneo akawajaza makada wa CCM, na zaidi watu wa kanda moja. Hili ni kosa kubwa kabisa la pili. Ni kinyume na kiapo chake
8) Kutoheshimu mipaka na kuingikia utendaji wa mihimili mikuu ya Jamhuri
9) Kudhamiria na kusimamia kifo cha demokrasia, haki na uhuru wa raia na vyombo vya habari, vyama vya siasa na maoni ya raia
10) Kutunga sheria mbaya kwa nia ya kuwadhibiti watu, kuondoa uwazi wa matumizi ya fedha ya Serikali
11) Kuhatibu mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyokuwepo kwa kujrnga hisia za kibaguzi na kupandikiza fikra kwa watu waamini kuwa kila mzungu ni mnyonyaji na adui. Kuharibu mahusiano yetu ya karibu na nchi ya Kenya. Na kwenye hili kama si busara za Kenyata, huenda hata mipaka ya nchi ingekuwa tayari imefungwa
Sent using Jamii Forums mobile app