Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mgombea wa Urais wa JMT kupitia CCM, Dkt. Magufuli
Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni na leo yuko Itigi mkoani Singida.
Magufuli akiwa na Mwigulu na wanaCCM wakiserebuka
Akiwa huko akaongelea uzuri wa nyumba za Singida na kusikitika zinavyopigwa vumbi ndipo ghafla akaitwa meneja wa Tanroad mkoa wa Singida mbele ya hadhara ya kampeni.
Mazungumzo yao yalikuwa hivi.
=======
“Nyomi” ya CCM Itigi
Dkt Magufuli: Ahadi yangu ya mjini ilikuwa kilomita 8 sasa ntatengeneza 10 pamoja na hii barabara niliyokuja nayo, nasema kwa dhati, sisemi kwa sababu ya kura. Nasema kwa sababu hii ni haki yenu.
Huu mji umependeza sana, mmejenga nyumba nzuri sana. Haiwezekani nyumba nzuri nzuri ziwe zinaendelea kupigwa mavumbi, nasema hapana kabisa lazima tutengeneze lami na mimi lazima niwaahidi ukweli. Mheshimiwa mkuu wa mkoa sijui yuko wapi? Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Singida hili ndio liwe la kwanza kushughulikiwa, asante sana.
Na regional manager wa Tanroads yupo au msaidizi wake? Njoo hapa, chukua mic
Dkt. Magufuli: Regional manager
Regional manager: Ndio mheshimiwa
Dkt. Magufuli: Pamoja na wa Tarura, nataka mkae hapa, kuanzia leo sisi tukiondoka.
Regional manager: Ndio mheshimiwa
Dkt. Magufuli: Mchague baadhi ya barabara zitakazotosha kwenye KM 10(Regional manager: Ndio mheshimiwa Rais).
Dkt Magufuli: Tangaza tenda mwezi huu, pesa usiulize, mimi nitatoa pesa kwa ajili ya kutengeza barabara hii. Itigi Oyee, (Wananchi: Oyee kwa shangwe). Kwa hiyo mjulishe chief executive wa Tanroard, mjulishe na waziri wa ujenzi, tunaanza mara moja, wala tusichelewe na hii wala sio hongo, mimi bado ni Rais kwa hiyo natoa maagizo. Tangaza tenda ya barabara za mjini Itigi kilomita 10, zitengenezwe kwa kiwango cha lami.
Regional manager: Ndio mheshimiwa Rais.
Magufuli akinadi sera za CCM Itigi, Singida
Dkt. Magufuli alifunga suala hilo na kuendelea na kampeni kwa kuelezea ubaya wa kugawa nchi katika majimbo na kuwataka wana-Itigi wawafundishe kwa kuwanyima kura wanaotaka kufanya hivyo.