Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Sio hongo, mimi bado ni Rais, natangaza tenda ya barabara za mjini Itigi KM 10

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887

Mgombea wa Urais wa JMT kupitia CCM, Dkt. Magufuli

Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni na leo yuko Itigi mkoani Singida.


Magufuli akiwa na Mwigulu na wanaCCM wakiserebuka

Akiwa huko akaongelea uzuri wa nyumba za Singida na kusikitika zinavyopigwa vumbi ndipo ghafla akaitwa meneja wa Tanroad mkoa wa Singida mbele ya hadhara ya kampeni.​


Mazungumzo yao yalikuwa hivi.
=======

β€œNyomi” ya CCM Itigi

Dkt Magufuli: Ahadi yangu ya mjini ilikuwa kilomita 8 sasa ntatengeneza 10 pamoja na hii barabara niliyokuja nayo, nasema kwa dhati, sisemi kwa sababu ya kura. Nasema kwa sababu hii ni haki yenu.

Huu mji umependeza sana, mmejenga nyumba nzuri sana. Haiwezekani nyumba nzuri nzuri ziwe zinaendelea kupigwa mavumbi, nasema hapana kabisa lazima tutengeneze lami na mimi lazima niwaahidi ukweli. Mheshimiwa mkuu wa mkoa sijui yuko wapi? Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Singida hili ndio liwe la kwanza kushughulikiwa, asante sana.

Na regional manager wa Tanroads yupo au msaidizi wake? Njoo hapa, chukua mic

Dkt. Magufuli: Regional manager

Regional manager: Ndio mheshimiwa

Dkt. Magufuli: Pamoja na wa Tarura, nataka mkae hapa, kuanzia leo sisi tukiondoka.

Regional manager: Ndio mheshimiwa

Dkt. Magufuli: Mchague baadhi ya barabara zitakazotosha kwenye KM 10(Regional manager: Ndio mheshimiwa Rais).

Dkt Magufuli: Tangaza tenda mwezi huu, pesa usiulize, mimi nitatoa pesa kwa ajili ya kutengeza barabara hii. Itigi Oyee, (Wananchi: Oyee kwa shangwe). Kwa hiyo mjulishe chief executive wa Tanroard, mjulishe na waziri wa ujenzi, tunaanza mara moja, wala tusichelewe na hii wala sio hongo, mimi bado ni Rais kwa hiyo natoa maagizo. Tangaza tenda ya barabara za mjini Itigi kilomita 10, zitengenezwe kwa kiwango cha lami.

Regional manager: Ndio mheshimiwa Rais.


Magufuli akinadi sera za CCM Itigi, Singida

Dkt. Magufuli alifunga suala hilo na kuendelea na kampeni kwa kuelezea ubaya wa kugawa nchi katika majimbo na kuwataka wana-Itigi wawafundishe kwa kuwanyima kura wanaotaka kufanya hivyo.

 

Wakazi wa Itigi mjini, mkoani Singida wametangaziwa neema na Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi baada ya meneja wa wa TANROADS kuagizwa kutangaza tenda mwezi huu wa tisa na kuanza mchakato wa barabara hiyo yenye urefu wa KM 10.

β€œMeneja wa TANROADS tangaza tenda mwezi huu ya ujenzi wa KM 10 za Barabara hapa Itigi Mjini, pesa usiulize, Mimi nitatoa pesa kwa ajili ya kutengeneza Barabara kwa kiwango cha lami, mjulishe Waziri wa Ujenzi, hii sio hongo, Mimi bado ni Rais natoa maagizo”-JPM



 
Maendeleo hayana chama
 
Sio ni utekelezaji wa bajeti ya mwaka guy iliyopitishwa na bunge la june mwaka guy

Utekelezaji wa bajeti huwa hausimami kwa sababu ya uchaguzi

Hata bajeti ya tume ya mwaka guy wanayotumia ni iliyoidhinishwa n.a. bunge la June
Umesema sahihi kabisa siongezi neno.

Nchi haijawahi kusimama, hata corona ilipokuja serikali ya Tanzania iliendelea kupiga kazi. Hii ndiyo sifa pekee ya JPM yeye ni kazi tu. 5 mingine kwake
 
.... rushwa za uchaguzi hizo. Maadili ya Uchaguzi hayam-exempt mgombea ambaye ni Rais kwamba anaweza kutoa fedha kwenye kampeni bali yanakataza "mgombea yeyote" kufanya hivyo.
Sio rushwa ni utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu nliyopitishwa na bunge la june mwaka huu

Utekelezaji wa bajeti huwa hausimami kwa sababu ya uchaguzi

Hata bajeti ya tume ya mwaka huu wanayotumia ni iliyoidhinishwa na bunge la June
 
Huyu mzee keshapoteana dadeki πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

CCM mko wapi jamani??? Mzee anawavua nguo hukuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Anavunja sheria za uchaguzi waziwazi
 
CCM mpumzisheni huyu mzeee! Aiseee anaharibu zaidi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Aisee how comes anafanya makosa ya wazi namna hii????πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Kweli dozi za Lissu zimezidi jamani!!! Magu keshaelekea kibra!!! Dadeki πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
sio rushwa ni utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu nliyopitishwa na bunge la june mwaka huu

Utekelezaji wa bajeti huwa hausimami kwa sababu ya uchaguzi

Hata bajeti ya tume ya mwaka huu wanayotumia ni iliyoidhinishwa na bunge la June
Alikuwa wapi kutoa maagizo kabla ya kampeni???

Daaah CCM kwisha Habari yenu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Huyu mzee keshapoteana dadeki [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

CCM mko wapi jamani??? Mzee anawavua nguo huku[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Anavunja sheria za uchaguzi waziwazi
Na bado kazi yao ilikua kumsifia tuu oooooo 2020 hakuna kampeni oooooo CDM tushaizika eti oooooooo wanakuja kuunga mkono hoja piga spana mpk wanataharuki
 
Magufuli haheshimu sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…