Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Uchaguzi huu ndio utaamua kama tuendelee au tusiendelee na Muungano

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Uchaguzi huu ndio utaamua kama tuendelee au tusiendelee na Muungano

Chadema na ACT wazalendo wanaamini katika serikali 3!

Kwani serikali tatu ndio zinaondoka muungano?? Hivi mna ukoko gani kichwani?? Hamjui kuwa hata sasa kuna serikali tatu kimuundo lakini serikali mbili kipropaganda??

Kuna mambo ya Zanzibar na kuna mambo ya Muungano. Katika mambo hayo ya muungano kuna ya Bara tu na ya Muungano. Rais wa JMT hana mamlaka kuhusu mambo kadhaa ya Zanzibar.

Ifike mahali tukae na kuondoa mambo yasiyofaa ya huu muungano. Hatuwezi kuwa na mtu anaitwa Rais wa nchi isiyokuwepo (Zanzibar). Tukitaka kuwa na Rais wa JMT basi Zanzibar iwe na waziri mkuu na bara iwe na waziri mkuu watakaounda serikali zinazohusu maswala yao yasiwe ya muungano na Rais wa jamhuri ya muungano atashughulikia yanayohusu muungano!!

Tunaweza kuwa na Britain (yenye England, Scotland na Ireland).
 
Mgombea urais wa JMT, Dkt. Magufuli amesema watanzania wawe makini wanapopiga kura kwani uchaguzi huu ndio utaamua kuendelea kuwepo kwa Muungano au kuvunjika.

Chanzo: Wasafi tv

Maendeleo hayana vyama!
Huu si muungano, huu ni uvamizi

Mgombea urais wa JMT, Dkt. Magufuli amesema watanzania wawe makini wanapopiga kura kwani uchaguzi huu ndio utaamua kuendelea kuwepo kwa Muungano au kuvunjika.

Chanzo: Wasafi tv

Maendeleo hayana vyama!
Hii kauli inanena makubwa sana.
Tumaini linapofifia katika jambo ulilotia imani , kauli za namna hii lazima zisikike.
 
Back
Top Bottom