Kwa mapinduzi ya kijeshi yaliotokea zanzibar, huu ndio mwanzo wa mwisho wa muungano. Mpaka dakika hii, mawakili wetu wamekwisha peleka barua za rufaa kuhusu muungano. kama munavojuwa tulikuwa na kesi arusha na matokeo yake ikawa , korti ilijiondoa kusikiliza kesi ile. Kwa hiyo step ya mwisho ni kwenda UN kutaka kuthibitisha na kutambulika kama ni mwanachama halali wa UN. Kwa kuwa hadi hii sasa hamna makubaliano ya muungano yaliothibitishwa na serikali zote mbili, wananchi wazanzibari wana haki kudai nchi yao na utaifa wao. Kila kitu kamilifu na tunasubiri maamuzi ya UN. Tukipita hapa basi tunawahakikishia ndugu zetu wa bara kuwa nchi zetu zitakuwa za kuheshimiana zaidi na kuthaminiana. Hali ilivo sasa hivi hairuhusu ustawi wa jamii kabisa.