Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Vitambulisho vya Machinga sio lazima, acheni uongo

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Vitambulisho vya Machinga sio lazima, acheni uongo

Geita,mtaa wa mgusu wamewalizimisha wamajinga na wamama wauza samaki kulipa hela ya kitambulisho pia na kutishia kuwafukugia na kuwafukuza kwenye biashara zao..hakika lissu amemkaba meko mpka basi.
Lissu shikilia hapo hapo,
 
Yeah, ameyasema hayo muda mfupi uliopita huku akisisitiza elimu itolewe juu ya suala hilo.

Ni katika mfululizo wa kujibu Tundu Lissu.

Nakumbuka kina Ally Hapi walijiapiza kuwa hawajajiandaa kushindwa kumaliza vitambulisho walivyopewa wawakabidhi wafanya biashara ndogo ndogo kwa malipo ya fedha halali shilingi elfu ishirini tu za kitanzania kwa mwaka.


My take!
Wakuu, kama tutakuwa serious kweli basi hili suala la vitambulisho vinavyolopiwa Tshs. 20000 ni wizi mtupu maana hiyo kodi haina draft yoyote kisheria! Yani hata ukienda mahakamani au bungeni hayo malipo hayatambuliki kisheria! Huu ni wizi wa mchana kweupe.

Mbaya zaidi wala haijuilikani inakoenda, mahesabu yake, ukaguzi wa matumizi yake. Yani ni mambo ya hovyo hovyo tu ya uongozi wa ufalme.

Sijui Bunge la Ndugai tulililipa ili liifanyie nini nchi. Huyu Spika Mungu atakuja kumpa funzo maana hakuwahi kulinda hadhi ya bunge lake!
Kwakuwa Lissu ndio kasema?
 
Mleta mada ndio anajua hilo leo,

Chadema wanachelewa sana kuelewa mambo,

Jambo linafanyika awamu ya nne wanakuja lielewa awamu wa tano,

Hata anayoyafanya sasa Magufuli watakuja muelewa awamu ya sita, mifano ipo mingi ni jambo la kuwavumilia tu hawa wapinzani tulionao kwani wanachelewa kuelewa mambo.
Umenena
 
Mimi mke wangu amelipia kitambulisho Cha machinga,leseni ya biashara na amepewa TIN ya TRA.Analipa Kodi ya mapato na leseni ya biashara pamoja na kuwa na hicho kitambulisho Cha machinga.Angalau warudishe hata hiyo 20 Basi ,ili tubaki kulipa kodi halali!
Maana yake mkeo sio machinga ila tuu alikuwa anataka kukwepa kulipa kodi kwa kutumia kitambulisho cha machinga .we utakuwaje ba leseni ,tin na kitambulisho cha machinga kama sio kutaka kucheza faulo.
 
Safi sana Mr President Lissu kanyaga hapohapo rais Wa wanyonge kachukua 20000 za walala hoi

Watu wa political science mtusaidie KWENYE issue za kujibu hoja au kutokujibu.....
KWA mtazamo wangu mh. Raisi anapo jibu hoja za TL
Anampa credibility Ni Kama kumpigia kampeni.....

Hofu kubwa kwao Ni kuikabidhi nchi upinzani
Hofu pengine wakipewa upinzani wataharibu nchi....

All in all MUNGU ibarik Tanzania
 
Mradi wa vitambulisho vya machinga ulibuniwa ili kuipatia CCM pesa. Pesa hiyo, kwa mwaka huu ndiyo inayotumika kugharamia kampeni za CCM. Kwa hiyo mwaka huu ni machinga ndio waliojwezesha CCM kufanya kampeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa!! Hivi vitambulisho hizi hela wala hazikwenda TRA sasa je zilienda wapi????

Kuna haja ya Raisi Tundu Antiphas Lissu kuanza kuchunguza hili akiingia tu madarakani hapo November mwaka huu!
 
Maana yake mkeo sio machinga ila tuu alikuwa anataka kukwepa kulipa kodi kwa kutumia kitambulisho cha machinga .we utakuwaje ba leseni ,tin na kitambulisho cha machinga kama sio kutaka kucheza faulo.
alipewa kwanza kitambulisho cha machinga afanye biashara kabla ya mengine
 
CCM ACHENI WOGA ...JENGENI MFUMO IMARA WA HAKI KUHALALISHA...UTAWALA ,KUNA SIKU MTAJUTA!
MNABOMOA UKUTA,KUUJENGAA ITAWAGHARIMU!
 
Sijui wenzangu mnaonaje ila mie naona Kama Jiwe ameshachanganyikiwa na Lissu 😂😂😂😂

Kwa jinsi alivyokuwa anatoa amri mchana kweupe kuwa wamachinga lazima wapewe vitambulisho na akawapiga biti mbaya sana wakuu wa mikoa kusimamia siamini kama leo amezungumza haya 😂😂😂
Nakama siyo vya lazima kwanini viuzwe. Swali kifikirishi kwanini walioshindwa kuviuza walitumbuliwa tena nyuma ya Mikamera
 
Nakama siyo vya lazima kwanini viuzwe. Swali kifikirishi kwanini walioshindwa kuviuza walitumbuliwa tena nyuma ya Mikamera
Na mbaya zaidi hela ya kuviuza hatuambiwi ilipatikana kiasi gani na imetumika kwenye nini??? Awamu ya Tano kuna ufisadi sana . Kinachosababisha usisike ni vitisho vya kutekwa, kupewa kesi na kupigwa risasi
 
Back
Top Bottom