Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Vitambulisho vya Machinga sio lazima, acheni uongo

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Vitambulisho vya Machinga sio lazima, acheni uongo

Jiwe kwa unafiki hajambo , Leo amekuwa mtu wa kugeuza kauli ndimi mbilimbili , Lissu anamnyoosha , Kigoma sijui wamemfanyaje ? Maana Tabora Leo alikuwa kapoa Kama maji ya mtungi au wamemRuangwa na moshi wa mashangazi .
 
Yeah, ameyasema hayo muda mfupi uliopita huku akisisitiza elimu itolewe juu ya suala hilo.

Ni katika mfululizo wa kujibu Tundu Lissu.

Nakumbuka kina Ally Hapi walijiapiza kuwa hawajajiandaa kushindwa kumaliza vitambulisho walivyopewa wawakabidhi wafanya biashara ndogo ndogo kwa malipo ya fedha halali shilingi elfu ishirini tu za kitanzania KWA MWAKA.


My take!
Wakuu, kama tutakuwa serious kweli basi hili suala la vitambulisho vinavyolopiwa Tshs. 20000 ni wizi mtupu maana hiyo kodi haina draft yoyote kisheria! Yani hata ukienda mahakamani au bungeni hayo malipo hayatambuliki kisheria! Huu ni wizi wa mchana kweupe.

Mbaya zaidi wala haijuilikani inakoenda, mahesabu yake, ukaguzi wa matumizi yake. Yani ni mambo ya hovyo hovyo tu ya uongozi wa ufalme.

Sijui Bunge la Ndugai tulililipa ili liifanyie nini nchi. Huyu Spika Mungu atakuja kumpa funzo maana hakuwahi kulinda hadhi ya bunge lake!
Ukinunua dai risiti, ukiuza toa risiti.
Vipi hivi vitambulisho kutokuwa na risiti Kama alivyotuasa mzee baba?
 
Back
Top Bottom