Uchaguzi 2020 Dkt. Mahera: Tume inaweza kuwafungia kufanya kampeni wagombea wa vyama wanaosambaza matusi badala ya sera

Uchaguzi 2020 Dkt. Mahera: Tume inaweza kuwafungia kufanya kampeni wagombea wa vyama wanaosambaza matusi badala ya sera

Matusi kama yapi kwamfano?? Labda wanaoandika mitandaoni, lakini kama anamaanisha kauli za Lissu ni vema kubainisha waziwazi! CCM ndio hawajambo kutukana wenzao na kuwaita vimajina vya hovyo kama kibaraka wa mabeberu, alafu ukimuuliza akuthibitishie hata kwa mfano tu jinsi gani mhusika ni kibaraka wa beberu unakuta hana jibu! Tunaiomba tume ijikite kusimamia uchaguzi , tena kwa haki na wasianze kutoa matamko yatakayowafanya wagombea kupata hofu hata ya kusalimia wananchi! Kuna mgombeda kamkashifu mgombea kamkashifu mgombe mwenzake kuwa anazungumzia watu kula ubwabwa wakati hata nyumbani kwake mwenyewe ubwabwa huo hautoshi! Je aliwahifika nyumbani kwake na kukuta ubwabwa huo hautoshi? kwanza mgombe aliyetaja ubwabwa kauzungumzia kama sera ya kitaifa, Je mambo ya kitaifa yanahamishwaje kuwa masuala ya familia zetu binafsi? Vipi Tume mbona hamjalikemea hili!? Tena huenda wamejitokeza baada ya mgombea mmoja kudai kauli za wengine zinamuudhi, Je yeye hizo za kwake zitzmfurahisha nani???
 
Tume ya CCM inashindwa kufanya nini?

Hii haishindwi kumtangaza aliyeshindwa kuwa kashinda. Haishindwi kumwengua yeyote kwa maslahi ya afisa uteuzi.

Hii ikikatia shauri, hakuna rufaa hata kwa Mungu. Tume ya namna gani hiyo?

Taasisi na mamlaka kama hizi zitahitaji ukarabati mkubwa katika na mara tu Tanzania tunayo ilenga itakapowadia. Tanzania itakayo kuwa imesheheni haki na uhuru.

Eeh mola wetu pokea sala zetu.
 
•Lakini ni waongo na waache uongo… hata sasa unaweza kuja hapa jengo la Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, tuko kwenye kikao tunaendelea kupitia hizo rufaa•

•Waache kutusumbua, sasa wao wanapiga kelele tungetoa hizo rufaa haraka hata hao wabunge wao wasingerudi, waache uzandiki, upuuzi na uongo•
EgWqpNOXoAAZPKP.jpg
 
•Lakini ni waongo na waache uongo… hata sasa unaweza kuja hapa jengo la Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, tuko kwenye kikao tunaendelea kupitia hizo rufaa•

•Waache kutusumbua, sasa wao wanapiga kelele tungetoa hizo rufaa haraka hata hao wabunge wao wasingerudi, waache uzandiki, upuuzi na uongo•View attachment 1570397
Mwana ccm katika ubora wake
 
Lisu anatukana hadi tume kuwa ya kijinga yenye maamuzi ya kijinga

Aliiporomoshea matusi ifakara
 
•Lakini ni waongo na waache uongo… hata sasa unaweza kuja hapa jengo la Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, tuko kwenye kikao tunaendelea kupitia hizo rufaa•

•Waache kutusumbua, sasa wao wanapiga kelele tungetoa hizo rufaa haraka hata hao wabunge wao wasingerudi, waache uzandiki, upuuzi na uongo•View attachment 1570397
Ananini la kusema huyo wakati yy mwenyewe ccm

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Charles Mahera amesema kwamba "Kama tume tunaweza kuamua kuwafungia hata kufanya kampeni, wagombea wa vyama ambao kazi yao ni kusambaza matusi na sio sera kwa kuwa sheria ipo na imetaja adhabu, tunatoa rai wabadilike na kuzingatia maadili ya uchaguzi waliyosaini"

''Kama watu walikuwa wamemchagua mtu atatangazwa kama kashinda, hatumtangazi mtu kwa shinikizo la watu, watu wauze sera zao ili wananchi wawachague kwa manufaa yao na si ya watu wa nje'

Dkt. Mahera ameyasema hayo kwenye kikao na watoa huduma ya Habari Mitandaoni leo Sep 15, 2020, ambapo pia amewataka kutumia kalamu na taaluma yao kulinda amani ya nchi kwa kufuata miongozo na taratibu za kutangaza habari za uchaguzi mkuu.

Maji ya shingo kwa CCM Sasa NEC mnaanza kuwa beba.... Tulieni dawa iingie
 
Yeye mwenyewe aonyeshe mfano wa kuwajibika kwa kujiuzulu nafasi aliyonayo kutokana na matamshi yake yanayoonyesha kuegemea CCM,matamshi ambayo yamesambaa katika mitandao ya kijamii.

Huyo ni mwana CCM damu ,nipo nnafukua mpaka nipate ile Video iliyo muonesha akiwa himiza wana CCM wenzake kubadilika ili kuwin Manispaa ya Arusha.
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Charles Mahera amesema kwamba "Kama tume tunaweza kuamua kuwafungia hata kufanya kampeni, wagombea wa vyama ambao kazi yao ni kusambaza matusi na sio sera kwa kuwa sheria ipo na imetaja adhabu, tunatoa rai wabadilike na kuzingatia maadili ya uchaguzi waliyosaini"

''Kama watu walikuwa wamemchagua mtu atatangazwa kama kashinda, hatumtangazi mtu kwa shinikizo la watu, watu wauze sera zao ili wananchi wawachague kwa manufaa yao na si ya watu wa nje'

Dkt. Mahera ameyasema hayo kwenye kikao na watoa huduma ya Habari Mitandaoni leo Sep 15, 2020, ambapo pia amewataka kutumia kalamu na taaluma yao kulinda amani ya nchi kwa kufuata miongozo na taratibu za kutangaza habari za uchaguzi mkuu.

Mahela unachokitafuta utakipata .
 
Back
Top Bottom