GE2025 Dkt. Malisa awafungulia Kesi Rais Samia na IGP Wambura Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) The Hague

GE2025 Dkt. Malisa awafungulia Kesi Rais Samia na IGP Wambura Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) The Hague

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wakuu huu uzi hautakiwi kupoa, na tuendelee kurusha mizigo kule ng'ambo! Mi nshawapatia mzigo wangu kwa affidavit page 8 naandaa mwingine tena maalum kwa accomplices kama kina bashite na wengine kadhaa
 
HOTUBA YA ZCO MAFWELE KWA SACP MULIRO YAVUJISHWA NA ASKARI WAZALENDO

View: https://m.youtube.com/watch?v=uhpcnYvolo4

Mafwele alitoa ripoti iliyorekodiwa voice akiongea na askari polisi huku SACP Muliro akipewa mchanganuo kuwa Wapo rumande polisi wakaguzi Superintendent mmo SP wa Babati, mwingine polisi Mbeya, Dar es Salaam polisi wawili wa Bandari wawili, askari wa JWTZ wawili wapo Changombe Polisi kwa kuchana bango, TAKUKURU watumishi 4, Benki Kuu, waalimu 9 na madaktari wawili

Baada,ya ripoti hiyo ya ZCO Mafwele, afande SACP amewaonya askari polisi mru hafi mara mbili, ukipigwa umekufa na kuna siku nitawaleta maafisa wawili ....kuwa huko nje kiko vipi
 
Nijielekeze moja kwa moja kwenye mada!

Kwanza nitoe pole kwa waliopoteza ndugu zao kwa ushenzi na unyama kutokana na tamaa na ulafi wa madaraka wa kikundi cha wahuni wachache, kwangu mimi ule kamwe siwezi utambua kama uchaguzi.

Nimetumia wiki hii kwa muda wangu mchache kusimama na haki ya sauti zilizopotea kikatili ili watu wachache wajitwalie madaraka kidhalimu , kwa kupitia video 178 na picha 43 tofauti nami nimechagua picha 18 na video 32 ambazo nimeziweka katika kanzidata yangu nami nitazipakia katika wavuti huu ili haki itendeke.
Nimegundua haya machache.

Katika uchunguzi wangu nimebaini kwamba asilimia 70-85 ya watu waliuwawa katika maeneo ambayo hayakuhusisha maandamano [majumbani, mitaani, kumbi za starehe n.k] na sijaona katika video.

Pia nimebaini uwepo wa mashambulizi ya moja kwa moja kutoa uhai na sio kutuliza ghasia katika maandamano maana wengi [80-90%] ya risasi watu wamepigwa katika vichwa , tumbo, mgongo na wachache miguuni, hii ni tafsiri tosha kuwa kulikuwepo na amri na kusudio la mauaji kuliko kutuliza ghasia.

Nimebaini uwepo wa silaha nzito za kivita kupitia maganda ya risasi, na pia aina ya risasi na aina za silaha walizokuwa nazo washambuliaji [wauaji]

Hivyo basi nitoe rai kwa yoyote mpenda haki tusimame na kupaza sauti kwa kuambatanisha ushahidi katika wavuti huu kwa hawa waliopotea maana hawana utashi tena wa kujisemea na ninaamini haki itashinda na huu ushenzi kamwe hautakuja kujirudia .

Safari ya ICC ndio imeanza, uzi huu uwe endelevu na ngao ya kupata haki kwa damu zote zilizopotea.

 
Kwa kuongezea Tanzania imesaini Mkataba wa Roma wa kuanzishwa kwa ICC ila haijaridhia (kuratify) hivyo siyo mwanachama wa ICC. Ukiwa siyo mwanachama wa ICC huwezi kushtakiwa katika Mahakama hiyo.
Mkuu wewe haya unayatoa wapi,Tanzania ni mwanachama wa ICC muda mrefu,

Tanzania iliridhia Mkataba wa Roma (Rome Statute), ambao ndio msingi wa kuanzishwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), tarehe 20 Agosti 2002. Kwa kufanya hivyo, Tanzania ikawa miongoni mwa nchi wanachama wa ICC, yenye makao yake makuu mjini The Hague, Uholanzi.
 
Safi sana naandaa ushahidi wa mauaji ya kibiti yaliyompa aijipi cheo cha juu wakati ni la saba tu na uwezo wake haujai hata bakuli la uji, nautuma siku chache zijazo! Nilikuwa huko wakati haya yanatokea na nilipoteza ndugu na jamaa wengi sana
Mbunge wa Rufiji si huyo Mkwe wa Samia, Mchengerwa!! Na huyu ndio anaeshirikiana na shemeji yake Abdul kupanga mauaji ya watanganyika wakiwatumia janjaweed toka Zanzibar!
 
Back
Top Bottom