Dkt. Mashinji afika Kisutu kusikiliza kesi inayowakabili viongozi wa CHADEMA. Mdee agoma kumpa mkono, Wakili ajitoa kumtetea

Dkt. Mashinji afika Kisutu kusikiliza kesi inayowakabili viongozi wa CHADEMA. Mdee agoma kumpa mkono, Wakili ajitoa kumtetea

Mkono tu hataki kuutoa je angeombwa papuchi ingekuwaje? Siasa sio uadui
 
Ndio unapojua elimu yetu tunayopata haituelimishi zaidi ya kujua kusoma kuandika na kuhesabu tunabaki na upumbavu wetu.

Kwamba Mdee anatwambia watu waliokwenye chama au imani flani hawatakiwi kuhama wakihama niwasaliti na niwatu wabaya?

Kama wanachama wote wa CCM walioanzisha vyama vya upinzani wangenuniwa sijui ingekwaje.
CCM wanajua kula na kupuliza na wanajua propaganda za siasa ndio maana hata waliohama wanarudi kwao maana hawakununiwa walipoondoka bado wanaalikwa Ikulu n.k

Sasa CHADEMA kuanza Kuwaita watu wasaliti na wanafiki kisa kuhama Chama ni ukosefu tu wa elimu.
Serikali iboreshe elimu maana Kama watanzania Watakua Kama Mdee kwamba hata kwenye dini ukihama dhehebu Moja kwenda jingine unanuniwa mfano Uhame RC uhamie TAG eti RC wakununie ni ujinga.

Labda CHADEMA wapeleke marekebisho ya Katiba kwamba ukiingia chama cha siasa ni Maisha yote hakuna kuhama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzukulu, Muasisi wa siasa za uadui humjui? Watu walikatazwa kwenda kumuona mbunge aliyefungwa kwa chuki,hukuliona hilo?

Watu walikatazwa hata kumchangia damu mtu aliyemiminiwa risasi za kutosha kama jambazi,hukuliona hilo?

Kati ya kumnyima mkono wa kusalimia msaliti na kumtwanga mtu risasi kwa "the so called usaliti",wewe waona bora ni lipi?
 
Childish and rubbish! Unashindwa kumpa mtu mkono uliyekuwa naye ktk uongozi kwa sababu ya kuhama chama! Hiyo ni ndoa? Bangi kichwani tu!
Baadaye wanalalama ooh CCM inatubagua! Tofauti ni nini hapo?
Kama unataka kushikana mikono, nenda wewe nyumbani kwa Mashinji uwe unamshika mkono kuanzia asubuhi mpaka jioni. Tusilazimishane ujinga. Kwa nini apewe mileage mtu msaliti??
 
ZAB. 1:1 SUV
Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
SUV: Swahili Union Version
 
Natafakari tu kwa mtu msomi wa kiwango cha Dr Mashinji kwenda mahakamani kila wiki inamharibia ratiba zake nyingi za kijamii na kiuchumi.

So sitashangaa nikisikia kamwandikia barua DPP kukiri makosa ya kuandamana bila kibali cha polisi.

Narudia tena sitashangaa kama hilo linawezekana kisheria.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ndio unapojua elimu yetu tunayopata haituelimishi zaidi ya kujua kusoma kuandika na kuhesabu tunabaki na upumbavu wetu.
Kwamba Mdee anatwambia watu waliokwenye chama au imani flani hawatakiwi kuhama wakihama niwasaliti na niwatu wabaya?
Kama wanachama wote wa CCM walioanzisha vyama vya upinzani wangenuniwa sijui ingekwaje.
CCM wanajua kula na kupuliza na wanajua propaganda za siasa ndio maana hata waliohama wanarudi kwao maana hawakununiwa walipoondoka bado wanaalikwa Ikulu n.k
Sasa CDM kuanza Kuwaita watu wasaliti na wanafiki kisa kuhama Chama ni ukosefu tu wa elimu.
Serikali iboreshe elimu maana Kama watanzania Watakua Kama Mdee kwamba hata kwenye dini ukihama dhehebu Moja kwenda jingine unanuniwa mfano Uhame RC uhamie TAG eti RC wakununie ni ujinga.
Labda CDM wapeleke marekebisho ya Katiba kwamba ukiingia chama cha siasa ni Maisha yote hakuna kuhama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya ndiyo marobot ya Lumumba yanayoishi kwa kutetea kila upumbavu kwa malipo ya Tsh 7,000 kwa siku. Imetosha umeonekana nenda kwa Polepole kachukue hela yako kisha kakojoe ulale. Huna hadhi ya jukwaahili Daaadeekiii
 
Back
Top Bottom