Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 15,335
- 29,114
9. Mwaka 1999 baada ya kupitia misukosuko mingi ya kisiasa ikiwemo mali zake kupigwa mnada, kufilisiwa na kufutiwa leseni ya uwakili aliamua kurudi CCM.
Haya mambo yalikuwepo enzi na enzi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
9. Mwaka 1999 baada ya kupitia misukosuko mingi ya kisiasa ikiwemo mali zake kupigwa mnada, kufilisiwa na kufutiwa leseni ya uwakili aliamua kurudi CCM.
Hata Joseph Selasini anatembelea nyota ya kaka yake Dr Masumbuko!1. Ndiye mtanzania wa kwanza kutunukiwa Shahada ya udaktari wa Falsafa katika sheria (Criminal and Procedural Law - LLD) Chuo Kikuu Oxford, moja ya vyuo vinavyoheshimika sana duniani.
2. Ndiye mwanafunzi wa kwanza kutoka Afrika kusoma kozi ya miaka minne kwa miaka miwili chuoni hapo. PhD in Criminal &Procedural Law (Oxford) ni miaka minne (full time) na miaka 6 hadi 8 (part time). Lakini Lamwai aliomba kusoma miaka miwili na akahitimu.
3. Mwanzoni mwa miaka ya 1990 akiwa Mhadhiri UDSM alishirikiana na wanaharakati wenzie kuanzisha vuguvugu la kudai mfumo wa vyama vingi.
4. Mwaka 1994 aligombea udiwani Kata ya Manzese kupitia NCCR. Alishinda lakini CCM wakachakachua. Akaenda Mahakamani matokeo yakabatilishwa. Uchaguzi ukarudiwa, akagombea na kushinda.
5. Akiwa diwani pekee wa upinzani Manispaa ya Kinondoni aligombea Umeya na kupata kura moja (ya kwake). Alipoulizwa kwanini aligombea wakati alijua hatashinda, alijibu "nisingegombea ningelazimika kumpigia mgombea wa CCM au kuharibu kura. Yote mawili ni makosa. Hivyo niliamua kugombea ili nimpe kura mgombea sahihi"
_
6. Ndiye Mbunge wa kwanza wa upinzani jimbo la Ubungo baada ya kushinda uchaguzi mkuu 1995.
7. Yeye na Mabere Marando wakiwa bungeni waligomea kiapo cha Utii kwa Rais, kwahoja kuwa wabunge hawapaswi kumtii Rais kwa sababu bunge ni mhimili unaojitegemea. Baada ya mabishano makali ya kisheria, Spika Msekwa alikubaliana na hoja yao. Kiapo cha wabunge kikafanyiwa marekebisho na kuondoa sehemu ya "utii kwa Rais" kisha wabunge wote wakaapa upya.
8. Mwaka 1996 aliongoza kesi maarufu ya uchaguzi iliyomvua ubunge aliyekua Mbunge wa Temeke, Ramadhani Kihiyo kutokana na kughushi taarifa za elimu yake. Mbali na kesi hiyo ameshiriki pia kusimamia kesi mbalimbali nje na ndani ya nchi. Mwaka 2006 alishiriki kuandaa muongozo wa Haki za binadamu kwa nchi za jumuiya ya madola.
9. Mwaka 1999 baada ya kupitia misukosuko mingi ya kisiasa ikiwemo mali zake kupigwa mnada, kufilisiwa na kufutiwa leseni ya uwakili aliamua kurudi CCM.
10. Dr.Masumbuko Lamwai ni kaka yake Mhe.Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo). Majina yake kamili ni Dr.Emmanuel Masumbuko Roman Selasini Lamwai.!
PICHANI: Mwanasheria wa Chadema John Mallya akiwa na mwalimu wake Dr.Masumbuko Lamwai (PhD) mwaka 2012 wakati Mallya alipohitimu shahada yake ya kwanza ya sheria (LLB).!View attachment 1441225
Nilipata kuelezwaharakati za jamaa huyu, nilibaki na mshangao maana wahenga wanasema alikuwa kisiki kweli kweli.Mwanasheria nguli, Msomi Kindakindaki aliyeichachafya CCM Hadi ikatia NIDHAMU.
Rest in eternal peace
Wali-enjoy sana waliofundishwa na huyu jamaa. Msomi wa Shahada ya Uzamivu (Ph.D in Laws) University of London 1983.Huyu baba alikuwa ni kichwa alafu bonge moja la mtu mstaarabu.
Chuoni ilikuwa bora nikose pindi lingine ila sio la Lamwai!
R.I.P Dr. Lamwai, Bwana akupe pumziko la amani 🙏
Iko iko iko na Bana Ngenge yeah!! Fataki Los Los Lokasa na Masumbuko ya Dunia.....aaaiiiii!!!!Kote huko Savannah , kote humo ni kwangu. Tumecheza muziki sana pale Tour and Huntes kwa Mzee Makassy enzi hizo. (sasa amekaa Gwajima na utapeli).
Kamanyola na Maquis pale Savvanah, White House. Kwa Manywele tulikuwa tunakula bia na nyma choma. Enzi hizo UDA ilikuwa inaishia Maji. Mitaa ya Chai unaifahamu?
Mzee Paisi unamfahamu? Mzee Komba? nakuja baadayeIko iko iko na Bana Ngenge yeah!! Fataki Los Los Lokasa na Masumbuko ya Dunia.....aaaiiiii!!!!
Umenikumbusha mbali sana!!!! Enzi ya Savanna Inn...
Hebu nitajie majina ya watemi wa Kibo kipindi ile……..
DahKimsingi maisha yenyewe hayajaanza bado, isipokuwa duniani hapa tumekuja kufanya uchaguzi wa utawala gani tunautaka baina ya ule wa Mungu au wa Shetani.
Sent using Jamii Forums mobile app