TANZIA Dkt. Masumbuko Lamwai afariki dunia

SELASINI JANA KASEMA HAKUNA MBUNGE ALIYEKUFA KWA KORONA ...NI UMBEA ....

NAONA ANAHOJIWA NA EATV YUKO BUSY KUSEMA NDUGU YAKE KAFA KWA MALARIA KALI ..... JAPO HAPO HAPO NDUGU WANASEMA YEYE HAHUSIKI CHOCHOTE KWAKUA ALIKUWA HAONGEI NA KAKA YAKE .....KWANINI AJE KUWA MSEMAJI WAKE AKIWA HAYUPO ..ANGEITAFUTA AMANI AKIWA HAI
 
Lamwai alikua ni jembe katika kumtoa mtu mchezoni...cross examination, kichwa cha kesi za jinai.
 
View attachment 1440056

Aliwayewahi kuwa Mbunge wa Ubungo na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Dkt. Masumbuko Lamwai amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 05, 2020.

Dkt. Lamwai atakumbukwa kama Mwanasiasa machachari, Mwanasheria nguli na Mkufunzi Mwandamizi (senior lecturer) wa Tumaini University.

Akiwa NCCR-Mageuzi, alikuwa na wanasiasa wengine wakongwe kama Mabere Marando, Marehemu Dk Sengondo Mvungi (RIP), Augustine Mrema, Makongoro Nyerere, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage, Stephen Wassira na wengine wengi.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Vyama Vingi wa 1995, NCCR-Mageuzi walitetemesha na kutingisha nchi mpaka Mwl Nyerere akaingilia kati baada kusimama majukwaani CCM.

Baadae alijivua uanachama wa NCCR na kuhamia CCM.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani.

MDOGO WA MAREHEMU DKT. LAMWAI, MH. JOSEPH SELASINI AZUNGUMZIA KIFO CHA KAKA YAKE

Kupitia mahojiano yake na kituo cha East Africa Radio asubuhi ya leo, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza hivi:

Dk Lamwai ni kaka yangu. Ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya Mzee Roman Selasini na Mama Katarina Roman.

Na kama kiongozi wa familia ametuongoza kwa hekima na busara mpaka mwisho wa uhai wake. Kama mtoto wa kwanza, ametutengenezea misingi mizuri katika familia.

Alikuwa ni mwanasheria aliyebobea katika mwenendo wa mashitaka pamoja na ushahidi (evidence and civil procedures)

MBUNGE PEKEE WA UPINZANI
Katika maisha yake ya kisiasa alipata kuwa diwani wa Manzese mwaka 1995 na baadaye alikuwa ni mbunge wa Ubungo na alikuwa mbunge pekee wa upinzani. Nakumbuka mwaka 1995 Tume ya Uchaguzi ilipofuta uchaguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam yeye hakuafiki akaendelea na kumshinda marehemu Venance Ngula wakati huo. Alidumu kwa miaka miwili na baadaye mahakama ikatengua ubunge wake.

Kipindi kilichofuata Mh. Benjamin Mkapa alimteua kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais. Hiyo ilikuwa baada ya kurejea CCM kutokea NCCR-Mageuzi. Amefariki akiwa ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi.

ALIKUWA HODARI, MWENYE MSIMAMO NA USHIRIKIANO
Namfahamu kama mtu hodari, mtu aliyekuwa na misimamo. Mtu ambaye alikuwa akikusudia jambo lake anapambana nalo mpaka ahakikishe limefika mwisho. Ni mtu alikuwa determined kwaakweli.

Alikuwa anashirikiana na watu kufanya jambo. Hata sisi wadogo zake alikuwa akituagiza hasubirii mrejesho, bali munakwenda wote.

Tumepata pengo kubwa katika familia. Tulipotelewa na wazazi na yeye alibaki kuwa kiongozi wetu na sasa ameondoka. Ni pengo ambalo halizibiki.

ALIPENDA KAZI YA UALIMU
Alipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alianzisha kampuni yake ya Uwakili inayoitwa Lamwai Advocates. Amefanikiwa kuwasomesha watoto wake wote wanne (4) ambao ni mawakili na wanashughulika na hiyo ofisi yake.

Baada ya kutoka Chuo Kikuu alikuwa ni mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Tumaini - Dar es Salaam. Aliendelea na kazi hizo mbili: Kuendesha kampuni yake pamoja na hiyo ya Uhadhiri.

Kazi ya ualimu aliipenda sana. Ni kazi ya familia. Familia yetu ina wanasiasa wengi sana na walimu wengi. Kwahiyo alipenda sana kusomesha mpaka mwisho wa uhai wake.

AFYA KUDHOOFU NA UMAUTI
Afya yake ilidhoofu katika kipindi cha wiki mbili tatu zilizopita. Lakini pamoja na kudhoofu huko, alipigwa na malaria kali ambayo alikuwa anaendelea kupata dawa.

Hata Jumapili alikaa na watoto wake wakaongea sana ni vile tu hauwezi kujua Mungu amepanga nini. Jana usiku akazidiwa na katika safari ya kumpeleka hospitali, akafia njiani.

Kwa sasa mwili umehifadhiwa Hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es salaam.

=====

SOMA: BAADHI YA KESI ALIZOWAHI KUSIMAMIA
Jinsi mbunge Ramadhan Kihiyo alivyojiuzulu baada ya kashfa ya kufoji vyeti - JamiiForums

Mbunge wa Longido Onesmo Nangole (CHADEMA) huenda akavuliwa ubunge kwa kufoji elimu - JamiiForums

Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini - JamiiForums
Kwa heri Masumbuko. Tutakukumbuka sana sisi marafiki zako. Tangulia na RIP. Amen.
 
Nakumbuka Mzee wetu Mkapa aliwahi mlaumu baada ya wabunge wengi wa CCM kushindwa kwenye kesi za uchaguzi ambapo Masumbuko alikuwa wakili upande wa upinzani.

Mkapa alisema" ukiona mtu ambaye kazi yake ni kuwavua wenzake ubunge hafai" akimaanisha Masumbuko Lamwai. Nakumbuka asilimia 99% ya kesi zoote alizosimamia Lamwai alishinda. R.I.P JEMBE
Kipindi hicho mahakama zilikuwa na uhuru kiasi na siyo kama sasa. Hawa majaji wa sasa sidhani kama wanathubutu kuwa huru kiasi hicho.
 
Kutokana na maelezo ya mbunge wa Rombo mheshimiwa Selasini ya kwamba Masumbuko Lamwai ni Tumbo moja wana share baba na mama.

Je kwanini aliitwa Masumbuko Lamwai bila kutumia Selasini nahisi ndio jina la ukoo wao?

R.I.P mwalimu Masumbuko Lamwai.
Pengine ni kam Mwigulu nchemba, kukariri madarasa.
 
View attachment 1440056

Aliwayewahi kuwa Mbunge wa Ubungo na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Dkt. Masumbuko Lamwai amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 05, 2020.

Dkt. Lamwai atakumbukwa kama Mwanasiasa machachari, Mwanasheria nguli na Mkufunzi Mwandamizi (senior lecturer) wa Tumaini University.

Akiwa NCCR-Mageuzi, alikuwa na wanasiasa wengine wakongwe kama Mabere Marando, Marehemu Dk Sengondo Mvungi (RIP), Augustine Mrema, Makongoro Nyerere, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage, Stephen Wassira na wengine wengi.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Vyama Vingi wa 1995, NCCR-Mageuzi walitetemesha na kutingisha nchi mpaka Mwl Nyerere akaingilia kati baada kusimama majukwaani CCM.

Baadae alijivua uanachama wa NCCR na kuhamia CCM.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani.

MDOGO WA MAREHEMU DKT. LAMWAI, MH. JOSEPH SELASINI AZUNGUMZIA KIFO CHA KAKA YAKE

Kupitia mahojiano yake na kituo cha East Africa Radio asubuhi ya leo, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza hivi:

Dk Lamwai ni kaka yangu. Ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya Mzee Roman Selasini na Mama Katarina Roman.

Na kama kiongozi wa familia ametuongoza kwa hekima na busara mpaka mwisho wa uhai wake. Kama mtoto wa kwanza, ametutengenezea misingi mizuri katika familia.

Alikuwa ni mwanasheria aliyebobea katika mwenendo wa mashitaka pamoja na ushahidi (evidence and civil procedures)

MBUNGE PEKEE WA UPINZANI
Katika maisha yake ya kisiasa alipata kuwa diwani wa Manzese mwaka 1995 na baadaye alikuwa ni mbunge wa Ubungo na alikuwa mbunge pekee wa upinzani. Nakumbuka mwaka 1995 Tume ya Uchaguzi ilipofuta uchaguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam yeye hakuafiki akaendelea na kumshinda marehemu Venance Ngula wakati huo. Alidumu kwa miaka miwili na baadaye mahakama ikatengua ubunge wake.

Kipindi kilichofuata Mh. Benjamin Mkapa alimteua kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais. Hiyo ilikuwa baada ya kurejea CCM kutokea NCCR-Mageuzi. Amefariki akiwa ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi.

ALIKUWA HODARI, MWENYE MSIMAMO NA USHIRIKIANO
Namfahamu kama mtu hodari, mtu aliyekuwa na misimamo. Mtu ambaye alikuwa akikusudia jambo lake anapambana nalo mpaka ahakikishe limefika mwisho. Ni mtu alikuwa determined kwaakweli.

Alikuwa anashirikiana na watu kufanya jambo. Hata sisi wadogo zake alikuwa akituagiza hasubirii mrejesho, bali munakwenda wote.

Tumepata pengo kubwa katika familia. Tulipotelewa na wazazi na yeye alibaki kuwa kiongozi wetu na sasa ameondoka. Ni pengo ambalo halizibiki.

ALIPENDA KAZI YA UALIMU
Alipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alianzisha kampuni yake ya Uwakili inayoitwa Lamwai Advocates. Amefanikiwa kuwasomesha watoto wake wote wanne (4) ambao ni mawakili na wanashughulika na hiyo ofisi yake.

Baada ya kutoka Chuo Kikuu alikuwa ni mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Tumaini - Dar es Salaam. Aliendelea na kazi hizo mbili: Kuendesha kampuni yake pamoja na hiyo ya Uhadhiri.

Kazi ya ualimu aliipenda sana. Ni kazi ya familia. Familia yetu ina wanasiasa wengi sana na walimu wengi. Kwahiyo alipenda sana kusomesha mpaka mwisho wa uhai wake.

AFYA KUDHOOFU NA UMAUTI
Afya yake ilidhoofu katika kipindi cha wiki mbili tatu zilizopita. Lakini pamoja na kudhoofu huko, alipigwa na malaria kali ambayo alikuwa anaendelea kupata dawa.

Hata Jumapili alikaa na watoto wake wakaongea sana ni vile tu hauwezi kujua Mungu amepanga nini. Jana usiku akazidiwa na katika safari ya kumpeleka hospitali, akafia njiani.

Kwa sasa mwili umehifadhiwa Hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es salaam.

=====

SOMA: BAADHI YA KESI ALIZOWAHI KUSIMAMIA
Jinsi mbunge Ramadhan Kihiyo alivyojiuzulu baada ya kashfa ya kufoji vyeti - JamiiForums

Mbunge wa Longido Onesmo Nangole (CHADEMA) huenda akavuliwa ubunge kwa kufoji elimu - JamiiForums

Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini - JamiiForums
Pole kwa familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwangu mimi Lamwai simuoni kama shujaa bali namuona kama msaliti aliyepaswa kufungwa jiwe la chumvi na kutoswa baharini toka zamani sana.

Kuanzia mwaka 2000 mpaka 2020 Lamwai hakuwa na mchango wowote wa maendeleo ya watanzania zaidi ya kudidimiza maendeleo ya watanzania chini ya mwamvuli wa CCM.

Kwa tunaofahamu mambo tunaelewa mchango mbovu wa Lamwai katika kuharibu hii nchi.

Ukweli tuuseme jinsi ulivyo.
Poleni wafiwa
 
Take it easy mzee. Tupo wengi wenye umri mkubwa, lakini inapofika kwenye malumbano, hapo inakuwa kitu kingine.

Napata wakati mgmu sana. Unakuta unamtukana mjukuu wako maana amekutukana, loh vinaniumiza roho
 
RIP Lamwai

Wakati anaota Lecture kwenye Jengo la Faculty of Law (wakati huo), ilikuwa mtu unaweza kukaa pale darajani kutokea bookshop na kuchukua notes. Alikuwa ana sauti ya juu kweli kweli.
Yeah jamaa alikuwa hata hatumii mic pale lecture thearter 1or 2 lakini alikuwa anasikika hadi nje
 
Back
Top Bottom