TANZIA Dkt. Masumbuko Lamwai afariki dunia

RIP..
Generation flani hivi ndio inakabidhi kijiti sijui kama vijana wengi wanafahamu au watatunza kumbukumbu ya tulipotokea.
 
Hata Joseph Selasini anatembelea nyota ya kaka yake Dr Masumbuko!
 
Huyu baba alikuwa ni kichwa alafu bonge moja la mtu mstaarabu. Chuoni ilikuwa bora nikose pindi lingine ila sio la Lamwai!

R.I.P Dr. Lamwai, Bwana akupe pumziko la amani 🙏
 
Mwanasheria nguli, Msomi Kindakindaki aliyeichachafya CCM Hadi ikatia NIDHAMU.
Rest in eternal peace
Nilipata kuelezwaharakati za jamaa huyu, nilibaki na mshangao maana wahenga wanasema alikuwa kisiki kweli kweli.

Msomi, shupavu na aliyesimamia alichokiamini. Anastahili kukubukwa kwa mchango wake kwa mageuzi ya vyama vingi kwa nchi hii.
 
Huyu baba alikuwa ni kichwa alafu bonge moja la mtu mstaarabu.
Chuoni ilikuwa bora nikose pindi lingine ila sio la Lamwai!

R.I.P Dr. Lamwai, Bwana akupe pumziko la amani 🙏
Wali-enjoy sana waliofundishwa na huyu jamaa. Msomi wa Shahada ya Uzamivu (Ph.D in Laws) University of London 1983.

The guy has left a legacy. Wahenga wanatamani chama kikuu cha upinzani cha sasa (CHADEMA) kingepata angalau wabunge 10 vichwa kama huyu jamaa
 
TIP Diwani wetu na Mbunge wetu 1995. Ulitetemesha sana. Nikikumbuka ule uchaguzi wa Temeke, Kihiyo alivyotaka kulikimbia jukwaa la Kampeni - nakumbuka ndipo ulianza msamiati wa 'vihiyo'
 
Nakumbuka pia walivyotetemesha Bunge lao la kwanza kwa kukataa kula kiapo hadi kilipobadilishwa, Nakumbuka spika Pius Msekwa alimwambia mwanasheria wa serikali siku hizo kuwa jipange sawasawa maana hili siyo bunge la mchezo
 
Dah! poleni sana, Siasa za kiswahili bana! kwa nini alifirisiwa Mali zake na yeye ni Mwanasheria? yaani wanasiasa hawakujali mdomo wake wala wa kisomi kweli? tena waliomfanyizia hawana elimu km yeye! Oxford UK kwa nini alirudi Bongo?

Alishau Wa-Bongo hawana Imani!
 
Iko iko iko na Bana Ngenge yeah!! Fataki Los Los Lokasa na Masumbuko ya Dunia.....aaaiiiii!!!!
Umenikumbusha mbali sana!!!! Enzi ya Savanna Inn...

Hebu nitajie majina ya watemi wa Kibo kipindi ile……..
 
Iko iko iko na Bana Ngenge yeah!! Fataki Los Los Lokasa na Masumbuko ya Dunia.....aaaiiiii!!!!
Umenikumbusha mbali sana!!!! Enzi ya Savanna Inn...

Hebu nitajie majina ya watemi wa Kibo kipindi ile……..
Mzee Paisi unamfahamu? Mzee Komba? nakuja baadaye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…