TANZIA Dkt. Masumbuko Lamwai afariki dunia

Poleni wafiwa wote kwa wakati huu mzito.
Hii ni safari ya kila binadamu.
Kasema Allah Mtukufu. Katika Qur-an
((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185]

kasema tena

((Leo (siku ya kiama)kila nafsi italipwa kwa iliyoyachuma duniani. Hapana dhulma leo. Allaah ni Mwepesi wa kuhisabu)) [Ghaafir: 17]
 
Wakati tunamsikitikia mwanasheria pia breaking news hapa ya mchungaji Mkuu wa pentecoste mwananyamala MMPT ametutoka usiku wa kuamkia leo
Ni majonzi mukubwa hapo mwananyamala A, mwinjuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hivi kati ya huyu Marehemu Lamwai na Lissu ni nani ametakata vilivyo katika Nyanja nzima ya Sheria na Uwakili nchini Kwetu?
 
Pumzika kwa Amani Dr. Lamwai
Pole kwa wafiwa
 
Pole sana kwa familia yake na tasnia ya sheria hapa nchini kwa kumpoteza nguli huyu wa sheria. RIP Lamwai
 
Pole kwa wote waliofikwa na msiba huu.

Nakushukuru sana kwa Lecture zako za Civil Procedure pale law school.
 
RIP Lamwai

Wakati anatoa Lecture kwenye jengo la Faculty of Law (wakati huo), ilikuwa mtu unaweza kukaa pale darajani kutokea bookshop na kuchukua notes. Alikuwa ana sauti ya juu kweli kweli.
 
Hivi kati ya huyu Marehemu Lamwai na Lissu ni nani ametakata vilivyo katika Nyanja nzima ya Sheria na Uwakili nchini Kwetu?
Lissu ni nini aisee kwenye sekta ya sheria? Huko kuna manguli ambao hawategemei vyama kusikika, wanapiga kazi zao kimya kimya tu, Lisu ni mwanasheria maarufu kupitia siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…