#COVID19 Dkt. Mollel: Chanjo ya Corona ni salama, ndio maana Rais Samia baada ya kuchanja akaenda Lugalo kuendelea na majukumu yake


Hapa ni pale wataalamu wanapoamua kuongea kama wasio na utaalam
 

Hili suala la corona limekuja kutudhibitishia kuwa tunaongozwa na watu wenye mambo ya kitoto sana. Ukiangalia ujinga waliokuwa wakiongea kipindi cha Magufuli, na huo utoto wanaoongea sasa mpaka aibu.
 
Maadamu mwataka kuonesha walio mtegemea Mungu wa Mbinguni walikuwa wajinga, mkae mkijua Mungu wa Mbinguni atakuonesheni yeye ni nani. Na hivi mmeamua kutumia chanjo hizi za voda fasta mtauona UKUU wa MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo/Israeli. Ambaye Jina lake Ni NIKO AMBAYE NIKO.
 
Wakikaa kimya watawaacha wananchi wapate utulivu wa kuchambua na kufanya maamuzi kuhusu chanjo.

Hizi sarakasi zao zinazidi kuvuruga watu, hasa zikitolewa na watu tuliowaamini na kuwapa dhamana ya madaraka makubwa.

Walipewa madaraka na wananchi au dhalimu alipora uchaguzi na kuwatangaza hao wahuni wenzake kuwa viongozi?
 
Maadamu mwataka kuonesha walio mtegemea Mungu wa Mbinguni walikuwa wajinga, mkae mkijua Mungu wa Mbinguni atakuonesheni yeye ni nani.
Ni lini mliwahi kumtegemea Mungu? Hakuna mtu mchafu anaweza kumtegemea Mungu.
 
Hahahaaaa...... Wizara ya afya!
Walisema Gwajima hajui Biology Wala Chemistry ataongeaje mambo ya chanjo..halafu muda huo huo wanatumia reference ya Rais kuchanja kwamba chanjo zipo Salama,hawezi kutuingiza shimoni.
Yawezekana ni kweli zipo Salama,lakini kwani yeye Rais amesomea mambo ya Biology na Kemia??

Yaani hawa jamaa wanazidi kuwavuruga watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni lini mliwahi kumtegemea Mungu? Hakuna mtu mchafu anaweza kumtegemea Mungu.

Wewe hujui sababu na nini maana ya Damu ya Mwana wa Mungu kumwagika pale msalabani. Hivyo sishangai kuita mtu mchafu. Sauli ima Paulo alikuwa mchafu na ziko imani zinamuita alikuwa Jahili.

Damu ya Mwana kondoo wa Mungu (YESU KRISTO )'Mungu'aliye uvaa mwili wa uwanadamu ili hatimaye huo mwili umwage damu ya kafara ya ukombozi wa mwanadamu aliye chafuliwa na dhambi ilimtakasa jabali huyu wa Kiroho. Hao uwaitao wachafu wameoshwa na Damu ya Bwana Yesu.

Wachafu ni wapi? Ni wale wanaomwaga damu za njiwa, kuku, mbusi, kondoo, watu, nk kuinajizi ardhi ya nchi, huku wakijua fika hakuna damu nyingine ya utakaso baada ya ile ya Yesu Kristo kumwagika pale Msalabani calvary. Utakaso wa dhambi utaupata tu pale utakapo mkubali/ mpoke Bwana Yesu, ukatubu dhambi zako, na ukabatizwa kwa Jina la Baba na Mwana na la Roho Mtakatifu kwa maji, na kwa Roho na Moto.
 

Achana na hao watu! Mungu alio amua kuwadhalilisha kwa kuwafanya mayaya wachanjaji wasivae gloves na kuwa kituko ulimwenguni mwote. Umevaa barako hujavaa gloves. Mungu hutumia vilivyo dhaifu kuwaumbua wanaojiadai wanayo maarifa na nguvu za kibinadamu wasimtegemee yeye na kutegemea akili zao. Akili zenyewe za kuikimbia salamu ya kumtukuza na kumsifu Mungu wa Mbinguni.
 
Huyu jamaa wakati wa enzi za mwendazake alikuwa na msimamo gani kuhusu Corona?
 
They are a confused gang.
 
Walipewa madaraka na wananchi au dhalimu alipora uchaguzi na kuwatangaza hao wahuni wenzake kuwa viongozi?

Mkuu, tukiweka pembeni walivyopatikana, katiba inawatambua hao ndio wabunge wanaotoa mawaziri.
 
Haka kajamaa katika mawaziri ambao hamna kitu Ni pamoja na haka. Ni kajinga mno. Kwahiyo madhara yanatokea siku moja.
 
Mkuu, tukiweka pembeni walivyopatikana, katiba inawatambua hao ndio wabunge wanaotoa mawaziri.

Kwa taarifa yako uhalali wa umma una maana kuliko hiyo katiba. Maana hata kama ni katiba bado hawaifuati kihivyo, labda kwa vifungu vinavyowabeba. Eti inatoa mawaziri, hivi mkuu unaona kuwa waziri ni kitu cha maana sana nini? Mawaziri wenyewe ndio hao wakati wa magufuli walikuwa wanasema chanjo za corona zina madhara, lakini hivi sasa chini ya Samia wanaongoza kuchanja, na kuhimiza watu wachanjwe maana chanjo ni salama!
 
HACHA UJINGA WAKO, TUTAJUAJE KAMA IZI WANAZOCHANJWA WENGINE NI SAWA NA ALIYOCHANJWA??
 
Huyu is a doctor by merits, kichwani kitaaluma ni mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…