Rais Samia, leo kwa maneno yake amesema Dr. Philip Mpango alimwambia anataka SASA kupumzika (yaani amechoka), hataki tena kuendelea na hiyo nafasi. Rais akakataa, lakini Dr. Mpango akamwandikia barua rasmi ya kuomba kutaka kuachana kabisa na hiyo nafasi SASA (kujiuzuru), Rais ameridhia ombi lake hilo kwa sharti kuwa itabidi amalizie miezi tisa ya utawala wake iliyobakia.
Kama hoja itajengwa kuwa, uamuzi wake huo wa kujiuzuru unahusika baada ya huu utawala kwisha Oktoba mwaka huu basi kimantiki tangazo la Rais halina mantiki na ombi hilo la Dr.Mpango halina mantiki kwa kuwa kikatiba wote (Rais na Makamu wake) mikataba yao ya kuongoza inakoma mwishoni mwa oktoba mwaka huu.
Wataalamu wa siasa, sheria, katiba hii imekaaje?