Pre GE2025 Dkt. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu Rais akimaliza muda wake, Rais Samia aridhia ombi hilo

Pre GE2025 Dkt. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu Rais akimaliza muda wake, Rais Samia aridhia ombi hilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hata wazir Mkuu wa Kanada alijiuzuru majuzi lakini bado yupo ofisini mpaka April 2025
Waziri mkuu wa Canada amejiuzuru, na kabla ya kipindi chake kumalizika, mtu mwingine atachukua nafasi yake.
Hii ya Dr. Mpango ni tofauti, anaendelea kushikiria hiyo nafasi mpaka kipindi chake kiishe. Sasa logic ya kuomba kujiuzuru sasa na kukubaliwa ni ipi?
 
Hata sasa niko Ujiji hapa.
Mpango acha apumzike tu,
Hana msaada wowote kwa mkoa wake wa Kigoma.

Wenzake wanapambana wabaki au wapate madaraka ili wasaidie mikoa yao na nchi kwa ujumla, yeye anakuwa msaliti anakimbia uongozi.
Acha akapumzike kwake Chanika
Lakini barabara zimejengwa mkuu! Umeme wa grid umeshafika Kigoma! Pale mjini pote pametandikwa lami! Sasa mnataka nini cha zaidi?
 
Mpango kapigwa TK-O.

Nadhani arrogance, conservatism na hardline approach imemuondoa.

Au labda ndio wale Mkuu wa Majeshi alisema........ wa nchi jirani

Bado majaliwa aje apigwe tukio pale akae Biteko.
Kumbe wewe na kelele zote hujui kitu kinachoendelea jikoni? Pole sana. Mpango mbona aliomba siku nyingi kujiuzulu akaombwa avute vute muda mpaka uchaguzi ufike? Hali yake kiafya siyo nzuri.
 
Nani alimwambia ingwe ijayo atapitishwa tena?
Hilo lilihitaji kuandika barua kwa Rais, tena sasa?
Rais alikuwa na sababu yoyote ya kulisema kwetu, tena sasa?
Rais angeweza kuutangazia umma kwa nafasi yake, ila aliamua kulitangaza kwenye kikao cha chama.

Dr.Mpango ana mgogoro na afya yake muda mrefu tu.

Kulisema au kutolisema kwetu hayo huwa ni maamuzi yao, unadhani hata tukifahamu tuna input gani kwenye hilo zaidi ya kupokea taarifa tu.

Umeona hata wajumbe walibaki vinywa wazi, na hawakuamua chochote, kaamua kuwapa taarifa kwamba Dr.Nchimbi ndiye mgombea mwenza, ndio kusema ndiye makamu wa rais ajaye. Na nafasi ya katibu mkuu ataijaza muda ukifika, yote hayo ni maamuzi yake yeye tu.

Hashauriwi wala hapokei ushauri kwenye hilo.
 
Mpango kapigwa TK-O.

Nadhani arrogance, conservatism na hardline approach imemuondoa.

Au labda ndio wale Mkuu wa Majeshi alisema........ wa nchi jirani

Bado majaliwa aje apigwe tukio pale akae Biteko.
Na kwa taarifa yako team Makamba ilikuwa inataka kupitia kwenye huo ''uchochoro'' wakashtukiwa. Alipoomba kujiuzulu kipindi cha nyuma, walikuwa wameshasuka mpango Makamba ndiyo awe makamu na akishakuwa makamu mengine yafuate....... NB acha kelele kama hujui mambo ya jikoni.
 

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amemwandikia barua ya kuomba apumzike Umakamu wa Rais ambapo amesema baada ya kutafakari ameridhia ombi hilo.

Lakini kwa sasa Dkt. Mpango ataendelea kuwa Makamu wa Rais hadi utakapofanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025.

Soma:Breaking News: - Uchaguzi 2025 - CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Akiongea leo January 19,2025 kwenye Mkutano Mkuu Maalum Jijini Dodoma, Rais Samia amesema

""Dkt. Philip Mpango ndiye Makamu wa Rais miezi ya karibuni hapa amekuja kuniona kuniomba apumzike, ana sababu kadhaa lakini sio za kazi, anasema yeye sasa ana miaka 68 na angependa kuishi zaidi kwahiyo naomba nipumzisheni.

Nikambishia bishia Wiki iliyopita hapa akanikabidhi barua yangu hii ( ya kujiuzulu?) na barua sikumjibu, nilipoenda kwenye Kamati Kuu nikawaeleza hiyo hali na kwa pamoja wote tukakubali tumpumzishe"
Lakini kwa sasa Dkt. Mpango ataendelea kuwa Makamu wa Rais hadi utakapofanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025.😂😂😂
 
Waziri mkuu wa Canada amejiuzuru, na kabla ya kipindi chake kumalizika, mtu mwingine atachukua nafasi yake.
Hii ya Dr. Mpango ni tofauti, anaendelea kushikiria hiyo nafasi mpaka kipindi chake kiishe. Sasa logic ya kuomba kujiuzuru sasa na kukubaliwa ni ipi?
Ni kawaida kwa CCM mgombea Mwenza kutambulishwa kwenye mkutano mkuu wa chama pindi jina la mgombea Urais linapopatikana na Tayari mkutano mkuu umempitishwa Samia Kuwa mgombea urais 2025.
Kwa hiyo ilikuwa vyema jina la mgombea mwenza nalo likajulikana!
 
Labda "kitengo" ndio kimemwambia ajiuzuru

Mzee wake Kinjekitile amekufa akikilaumu kitengo kukata jina la Lowasa miaka ile
 
Rais Samia, leo kwa maneno yake amesema Dr. Philip Mpango alimwambia anataka SASA kupumzika (yaani amechoka), hataki tena kuendelea na hiyo nafasi. Rais akakataa, lakini Dr. Mpango akamwandikia barua rasmi ya kuomba kutaka kuachana kabisa na hiyo nafasi SASA (kujiuzuru), Rais ameridhia ombi lake hilo kwa sharti kuwa itabidi amalizie miezi tisa ya utawala wake iliyobakia.

Kama hoja itajengwa kuwa, uamuzi wake huo wa kujiuzuru unahusika baada ya huu utawala kwisha Oktoba mwaka huu basi kimantiki tangazo la Rais halina mantiki na ombi hilo la Dr.Mpango halina mantiki kwa kuwa kikatiba wote (Rais na Makamu wake) mikataba yao ya kuongoza inakoma mwishoni mwa oktoba mwaka huu.

Wataalamu wa siasa, sheria, katiba hii imekaaje?
Hapa tumepigwa
 
Wadau sijui mna stress au laa,amesema anajiuzuru kipindi cha pili baada ya uchaguzi,kwa maana hataendelea na awamu ya pili,shida ya kuelewa iko wapi?
 
Back
Top Bottom