Dkt. Mpango kustaafu Siasa, atangaza kupumzika na kukuza Kilimo cha Urithi wa Baba yake

Mkuu, sidhani kama Wasira ameshafikisha A-T years!

Sana sana atakuwa anaelekea fifty 7 hapo.

Media zisikudanganye na kututoa kwenye reli katika harakati za kujadili mambo yenye tija zaidi kwa taifa letu.
Anko Wasira mwenyewe anasemaje?
 
Haya mambo yote tulikuwa tunayafahamu.
Hii posting haina sababu.
”Tulikuwa” wewe na nani?

Maana kama mimi nilikuwa sijui hata kinachoendelea kumuhusu huyu mzee ndiyo nimejua leo kwamba anataka kuachana na biashara ya siasa.
 
Acha utani. Umefanyika mkutano wa CCM Dodoma juzi.
Nchimbi uteuzi wake unahusiana na Mpango kujiuzulu,ingawa sasa sikumbuki ulikuwa uhusiano gani.
 
Hivi kuna kitu chochote anachojivunia kuwa alikifanya kwa ufanisi nyakati za umakamu wake wa Rais
 
Like ....Mimi pia naungana na kaka yangu, kaka Philip..........🤣🤣
 
Kwenye katiba hakuna kitu kinaitwa àwamu. Naona tumeihusisha na raisi wa ngapi.
1. Nyerere
2. Mwinyi
3. Mkapa
4. Kikwete
5. Magufuli
6. Samia.
Wala hakuna raisi wa mpito.
Samia hakupigiwa kura, usijidanganye yupo kwa mujibu wa katiba.

Samia alipaswa kushika madaraka kipindi alichobakiza madaraka kuandaa uchaguzi ujao kisha aondoke.

Samia hakupigiwa kura na wananchi popote Tanzania hii.
 
Ni kweli yupo kwa mujibu wa katiba. Katiba inatambuwa hiki ni kipindi chake cha kwanza. Ana haki ya kugombea tena.

Hapaswi kuondoka. Akiamuwa anaweza kuondoka.
 
siamini mpaka ifike hiyo siku na itokee vinginevyo na nijauvyo P.Mpango (PhD) ndiye raisi wa jmtz ajaye …
 
Afanye fanye ili ile barabara ya kuelekea Homboza isogee sogee kidogo kufika kituo cha afya homboza kuliko kuishia pale pale getini kwake Chanika Zingiziwa
 
Samia hakupigiwa kura, usijidanganye yupo kwa mujibu wa katiba.

Samia alipaswa kushika madaraka kipindi alichobakiza madaraka kuandaa uchaguzi ujao kisha aondoke.

Samia hakupigiwa kura na wananchi popote Tanzania hii.
Ni mgombea. Akipata hii hoja inakuwa haina mashiko tena.
 
Ana hekima gani wakati watu alioapa kuwalinda wanatekwa yeye amefunga mdomo...au ndiyo hekima kwa uelewa wako?
Hekima siyo mamlaka, inawezekana hekima zake ndio zimemuongoza kung'atuka, maana Hana mamlaka hayo ya kusitisha hayo, auu we unafikili hekima ni Nini kwa uelewa wako mjomba

NB hukuwahi muona kiongozi mwenye mamlaka lakini akakosa hekima, na wenye hekima wengi lakini wakakosa mamlaka!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…