Dkt. Mpango: Mkandarasi wa Bwawa la Nyerere hana Uzoefu, pia mradi upo nyuma ya muda

Tuwapeni muda viongozi wetu wasimamie kumalizika kwa mradi....

Kwa mradi mkubwa kama huu wa Trilioni 6.5 ni lazima kuwe na kuhoji...lakini pia ni lazima tuwe na mizani ya kujua kuwa "miluzi mingi humchanganya mbwa".....
 
Hata muitengeneze haiwezi kutokea...Aliwazidi akili kwaku document kila event na ku share na general public...Kil uzushi utakuwa na counter attack yake...Ukajipange upya!
Unampaja mtu asie na uzoefu kutekeleza mradi mkubwa kama huo?

Yale yale ya Richmond.
 
Unampaja mtu asie na uzoefu kutekeleza mradi mkubwa kama huo?

Yale yale ya Richmond.
We kaendelee kutengeneza tamthilia njoo nayo uone tutakavyokupangua...Hii ni karne nyingine siyo enzi zile ambazo mliwaokota raia kwakukosa knowledge
 
Unaota ndoto au tayari umepata kinywaji
 
Weeeee! Km ungelikuwa wewe ungelisema chochote zaidi ya kusifia?!! Thubutuuuu
 
Zimeanza story kama zile za sgr ilikua 2019, ikaja 2020 ikaja 2021 hadi sasa haijulikani lini mwisho wake. Sisiyemu ni adui namba moja wa taifa ili.

Tena baada ya kifo ata tbc hawaruki tena live kutoka bwawani ahahahaha. Ukweli bwawa la nyerere itachukua muda kukamilika,
 
Arab Contractors imeanzishwa miaka ya 1950.....

Imejenga mradi mkubwa wa kufua umeme "ASWAN DAM"...unasemaje kuwa hawana uzoefu ?!!!
Ndugu hawa ndugu wanajua wanachokitaka....Tutawaona tu sura zao kamili kabla hata mwaka haujaisha
 
Kalemani alifundishwa uongo na Magufuli na yeye kabeba tabia ile moja kwa moja. Kipindi chote cha Magufuli data 70% zilikuwa za kupika. Na serikali hii nayo naona inaanza kupika data.
 

Waziri nani.
 
Kabla ya kumpa mtu kazi angalia kwanza uzoefu. Brazil, Urusi na China ndiyo hujenga mabwawa kila leo. Sasa wamisri na mabwawa wapi na wapi. Brazil walionyesha siku nyingi interest na hiyo project, na wanauzoefu mkubwa lakini jamaa akajikuta Pan-African.
 

Sijui haya maneno yamelenga kufikia lengo gani? Wakati mwingine watu wanaongea utafikiri Tanzania sasa inaongozwa na chama na serikali nyingine kabisa ambayo si ya CCM.

Hawa viongozi walikuwa wapi kuongea wakati haya mapungufu makubwa hivi yanafanyika? Kwa nini waliwadanganya wananchi kwa kusifia huu mradi wa bwawa la Nyerere? Viongozi wakuu wastaafu walitembelea hilo Bwawa juzi kati wakasifia kumbe na wao walikuwa wanaongelea wasichokijua mbele ya Watanzania. Mh Makamu wa Rais akiwa Waziri wa fedha alikuwa anatoa fedha kulipa mkandarasi asiye na usoefu wakazi. Yajayo mbeleni yanatafakarisha sana.
 

Mwarabu gani yuko kibendudi zaidi ya kujua kujilipua tu? Ili kupata wale sabini?
 
Hta
Wewe unatudangnya tu,
Tusubili mwezi wa kumi na moja uishe kabla hawajajaza maji kisha ndo uje hapa
 
"Aswan Dam" imejengwa na haohao ARAB CONTRACTORS tena miaka ya 1960...... Serikali ya awamu ya 5 haikukosea......
 
Umuoni alivyofura siku hizi na kunawiri; tafuta picha zake za kabla ya kuwa waziri wa fedha.

Kuna watu wao wanafikiria shibe yao tu, hiyo ndio namna yake ya kukazia mama yupo sahihi kumtimua Kalemani nishati (ukiniuliza mimi Kalemani kajifukuzisha mwenyewe kwa kukaa kimya wakati umeme unakatika ovyo).

Sasa wao kumfurahisha boss wanaongezea na chumvi zao; as the saying goes ‘shibe mwanamalevya, njaa mwanamalegeza’.
 
Huu mradi ni bomu litalokuja kulipuka huko mbeleni.

Haya ni madhara ya mtu mmoja kuaamua kila kitu huku akipigiwa makofi na mazuzu.

Haya yangesemwa na wapinzani wangeshambuliwa vibaya sana na hata kukamatwa au kufanyiwa hujuma.
Kivipi mkuu toa analysis za kitaalamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…