Lazima tufahamu ya kawmba huu mradi umejengwa kwenye eneo la urithi wa asili ulio chini ya UNESCO hivyo makampuni mengi makubwa yalikataa kwa kua yangekua blacklisted.Tanzania ni zaidi ya uijuavyo...
Kwahiyo, kwa lugha inayoeleweka, Mkandarasi HANA SIFA za kupewa hiyo kazi lakini serikali ya Rais Mtukufu bado ikatoa kazi kwa Mkandarasi asiye na sifa!
Yaani, kwa maana nyingine tulimpa kazi Middle Man...
Na pesa anapewa Middle Man
Middle Man anachukua chake, na kinachobaki anawapa subcontractors wanaofanya kazi yenyewe!!
Yaani ni sawa na mtu unampa kazi Civil Contractor akujengee mjengo halafu nae ana-subcontract kila idara including civil works!
Hivyo ikabidi nchi iamue kumpa mwarabu ili akisubcontract sawa tu ilimradi mradi huu ukamilike kwa kua tulikuwa hatuna namna wakubwa walitubana.
Makamu wa Rais anajua hii maneno so tusilaumiane km tutalipa mzigo ule ule tuache kazi iendelee.
Mwandishi umesema kua mafuriko ya covid ndio yalisababisha delay si kweli wakati wa covid kazi pale ilifanyika isipokua kuna wakati kuna mafuriko yalitokea ambayo yalisimamisha kazi pale power house.
Tuache siasa kwani hata hapa jf kuna taarifa iliwahi kuandikwa ikieleza kampuni ya Elsewedy ambayo ni mojawapo ya wajenzi wa bwawa ilitakiwa kuwa blacklisted.
Tuseme tu tulikua hatuna pa kwenda ndio maana mwarabu alipewa hiyo kandarasi.