Unauhakika kati ya hao wawili Kalemani ndio amekudanganya?
Hicho nacho ni cha kuuliza. Wewe kama unamwamini Kalemani, subiri mwezi ujao bwawa lianze kujazwa maji.
Watendaji wengi, pamoja na mawaziri na Rais mwenyewe, wakati wa awamu ya 5, walizoea kuoongea uwongo. Katika mambo makubwa, hakuna hata moja ambalo lilikuwa la kweli. It was a good government fir the fools:
1) Dhahabu tunaibiwa nyingi sana, tunadai kodi ya dola billion 190 - uwongo
2) Makinikia kwenye makonteina, 90% ni dhahabu - uwongo
3) SGR itaanza kufanya kazi mwezi wa November 2020 - uwongo
4) Trump amepongeza utendaji kazi wa Rais Magufuli - uwongo
5) Serikali ina pesa za kutosha, tunajenga miradi yote kwa pesa zetu - uwongo
6) Uchaguzi wa 2020 utakuwa huru na wa haki - uwongo
7) Wanavyuo wote watapewa mikopo - uwongo
8) Wafanyakazi tutawaongezea mishahara, siyo ongezeko dogo kama mlivyozoea - uwongo
9) Kuna mtu kila saa moja alikuwa anaiba shilingi milioni 7 - uwongo
10) Gas wamechukua wachina - uwongo
11) Ujenzi wa bwawa la Nyerete umefikia 70% - uwongo
12) Ndege zimeingiza faida ya shilingi bilioni 17 - uwongo
13) Watanzania tembeeni vifua mbele, uchumi wetu upo pazuri - uwongo
Waliozoea kuishi katika uwongo, hawawezi kubadilika ghafla na kuwa wakweli.