Dkt. Mpango ndio aina ya wazee tunawataka kwenye Taifa. Hana makuu, hana tamaa ya madaraka

Dkt. Mpango ndio aina ya wazee tunawataka kwenye Taifa. Hana makuu, hana tamaa ya madaraka

Nini kilitokea?
Makonda alilipa ile kodi?

Muwe na kumbukumbu, hakuna chochote kililipwa katika lile sakata.
Sijasema alilipa. Wala sijafika huko kwamba alilipa au hakulipa. Hiyo si sehemu ya mjadala wangu.

Nilichosema ni kwamba, wakati Makonda alikuwa mtu wa kuogopwa sana na watu karibu wote serikalini, kutokana na ukaribu wake na Magufuli, Dr. Philip Mpango alisimama kama mtu pekee ambaye alisimamia kanuni na kukataa kumsujudia Makonda. Akasema alipe kodi.

That alone was something kwa sababu Makonda alikuwa hajawahi kuwa challenged vile serikalini. Na ule ndio ulikuwa mwanzo wa Makonda kuanguka kutoka kuwa Magufuli's golden boy mpaka kukaa bench.

Sasa kama Makonda alilipa au hakulipa hatuna ushahidi wowote mpaka sasa, hata wewe hujaweka ushahidi kwamba Makonda hakulipa.

Na huko sijasema lolote nimesema tu kwamba Dr. Mpango alinyoosha mstari na hakuogooa kumwambia Makonda alipe kodi mchana kweupe.

Kitu ambacho watu wengine serikalini hawakuthubutu kum contradict Makonda.

Unataka kubishia hii fact au unataka kuleta ubishi wa logical non sequitur fallacy kuhusu mambo ambayo hata sijayasema unajiongezea mwenyewe tu?
 
Ni taifa la wajinga na wapumbavu tu ndio linaweza kuvutiwa na aina ta watu wa ovyo kama Dr. Mpango.
Dr Mpango, ni Mrundi. Waikumbuka hii??
Screenshot_20250120_212753_Chrome.jpg
 
Mleta mada ana element za ukweli.Dr. Philip Mpango ni mnyenyekevu , hana makuu . Hana tamaa ya madaraka.

Mimi kuna wakati mwaka juzi niliwahi kwenda Chanika nilikuwa naenda kufanya issue zangu. Sasa kuna barabara ilikuwa inatengenezwa mahali fulani na ni kama ilikuwa inatumika angali maengeneer wanaendelea na kazi zao . Nikawa namuambia mwenyeji wangu hii barabara itachelewa sana kuisha, kwa nini wameruhusu itumike akati bado inatengenezwa ? Mwenyeji wangu kule Chanika akasema itaisha tu maana inaenda kwa makamu wa rais. Nikashangaa , " Makamu wa rais anaishi Chanika!!!". Chanika ambayo wakazi wengi wa Dar es Salaam wanaona kama watu wanaoishi Chanika ni watu wa hadhi ya chini.

Hili tu linatosha kutuonesha Dr.Philip Mpango ni mtu wa aina gani. Jamaa ni mnyenyekevu.Anapenda kuwa karibu na wananchi wake wa hali ya chini.
 
Yule dingi anapenda madaraka na vyeo vya mserereko balaa. Kipindi yuko hoi hospitalini akiuguzwa Covid, bado alikomaa tu kuendelea kukalia kiti cha uwaziri na akiwa hoi bin taabani akajikongoja kuja hadharani kuongea ili alinde ulaji wake na ulaji wa aliyemteua.
Leo kakuachieni akiwa na nguvu zake kamili, utasemaje huu ujinga uloandika hapa?
 
Ukimuona mtu anamsema vibaya Mh Dr Mapango basi juwa nimaumivu na chuki kubwa juu yake kwa uwamuzi wakupiga chini nafasi ya Umakamu wa Rais na kurudi back benches.

Ndie waziri pekee wa fedha alie kuwa akiishi nyumbani na sio kwenye pepo za baharini na hii ndio siri yakupendwa kwake na Hayati Magufuli kiasi kupiga simu akiwa hospitali amuone na Watanzania wamuone.
Dr Mpango ndie Eng wa uchumi na mambo yote mnayaona na huyo waziri mtaka sifa pale ametemebelea sana nyota ya huyu Dr Mpango.

Uwezo na akili alizo nazo ziliwavutia wakubwa zake kumsogeza karibu kuanzia JK mpaka Magufuli.

Nimoja ya nyota na tunu tulizo nazo katika Taifa ni bahati mbaya hakushika kiti kwasababu za kibinadam au Mungu mwenyewe. Sio chawa ila nimsema kweli nainaonyesha anachukia uchawa na ameuchukia uchawa kwa maandishi. "Naomba nipumzike"

Huyu ndio aina ya kiongozi tunamuhitaji nina amini JK amelia alipojuwa huyu mwamba ameamua kupumzika ila walamba miguu tumefanya part maana alikuwa mnoko sana kuzuwia vimeo vyetu. Yes hakuna anaweza kuja nakusema vile Dr Mpango nimsumari wa moto kwa majizi ya wizarani na kwenye mfumo.

Hana deal ila peleka pesa bank ya serikali nakama una zawadi kumtunuku basi peleka kwenye akaunti yaserikali mama na mtoto wapate huduma bora ni mwana mapinduzi na mzawa wa kweli katika uzalendo kwa taifa lake.

Nafasi ya umakamu wa Rais ndio ilimtoa home sweet hoem kwenda baharini ila yaonyesha hakukupenda na ameamua rudi nyumbani. Akafuge kuku na kucheza na ujukuu wake huku akikielimisha kizazi kijacho juu ya uzalendo.

Mh Dr Mapango amekuwa mnyenyekevu nakufia ukweli huku akiepuka laana ya Hayati Magufuli kwa yote yanasemwa ameamua kuacha kabisa akijuwa hakuna atake ishi milele na mwamba alikufa akisimamia watu wake wa Tanzania kwa dam na nyama.

Alikuwa nikipenzi cha Magu na amekubali kukaaa pembeni kuipisha gharika ya pili ukiacha ile ya kwanza kwa wale wakiroho tunamuona kama mtu anayo iyona kesho baada ya uchaguzi. Yale yatatokea na kile kitatokea hataki kuwa mmoja wa hayo.

Upo msemo unasema koti lakuazima usilifanye likawa la kwako na cheo chochote kina gharama ametimiza ahadi hiyo kwa gharama kubwa kwakuamini serikali ilimuamini kwa tatizo Taifa lilitupata hivyo anawashukuru na kwarudishia cheo chao ili wengine wachukue usukani ameishinda Tamaa na amemshinda shetani.

Soma Pia: Dkt. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu wa Rais, Rais Samia aridhia ombi hilo

Hakutaka kufanana na Mungu pamoja na uwezo wote aliokuwa nao hakutaka makuu amejikubali naomba viongozi wote tujifunze kwa Dr Mpango.

Taifa lilikumbwa na msiba mzito nakama sio ule msiba asingekuwa makamu wa Rais je kwanini aendelee kushika nafasi kwa ubabe na fitina wakati alipewa kama hisani na upendeleo wa Mungu.

Dr Mpango moyo wake ukamkumbusha usitamani jambo hukuandaliwa na yakuwa nafasi kubwa kama yake niupendeleo toka kwa Mungu na taifa lina watu sio yeye peke yake basi akang'atuka huu ni uzalendo mkubwa sana.

Dr Mpango wajinga wachache watabeza msimamo wako ila nataka nikuhakikishie mbingu zitasimama uwone yote yatatokea ili umtukuze Mungu na uzao wako. Wewe ni mshindi wewe ni simba na Mungu azidi kukulinda kwa Makerubi wake asubuh, mchana na usiku. Amen
Basi kama alikuwa hivyo mafisadi ni lazima wamchukie na hivi sasa watakuwa wamefurahi sana 😳
 
Hivi lini ulimuona Dr. Mpango akikemea na kulaani mojawapo katika haya mambo:
1. Utekaji na mauaji ya wakosoaji wa serikali.
2. Uchafuzi katika uchaguzi wa 2019, 2020, 2024.
3. Uuzwaji wa bandari za Tanganyika
4. Kufukuzwa kwa wamasai kule Ngorongoro
5. Wizi na ufisadi uliokithiri ndani ya serikali.

Kwangu mimi, Dr. Mpango ni miongoni mwa watu wa ovyo kabisa kuwahi kushika nafasi za juu katika serikali yetu. Hakuwa na sifa zozote za kutuvutia kabla ya kuteuliwa na ameshindwa kujenga sifa zozote hata baada ya kuteuliwa. Ni bure kabisa.
Mtaje makamu yeyote yule aliyewahi kukemea mambo ya boss wake
 
Mleta mada ana element za ukweli.Dr. Philip Mpango ni mnyenyekevu , hana makuu . Hana tamaa ya madaraka.

Mimi kuna wakati mwaka juzi niliwahi kwenda Chanika nilikuwa naenda kufanya issue zangu. Sasa kuna barabara ilikuwa inatengenezwa mahali fulani na ni kama ilikuwa inatumika angali maengeneer wanaendelea na kazi zao . Nikawa namuambia mwenyeji wangu hii barabara itachelewa sana kuisha, kwa nini wameruhusu itumike akati bado inatengenezwa ? Mwenyeji wangu kule Chanika akasema itaisha tu maana inaenda kwa makamu wa rais. Nikashangaa , " Makamu wa rais anaishi Chanika!!!". Chanika ambayo wakazi wengi wa Dar es Salaam wanaona kama watu wanaoishi Chanika ni watu wa hadhi ya chini.

Hili tu linatosha kutuonesha Dr.Philip Mpango ni mtu wa aina gani. Jamaa ni mnyenyekevu.Anapenda kuwa karibu na wananchi wake wa hali ya chini.
Dodoma pia Anakaa Kule Zuzu

Maaurufu kama kwa Mzee Pinda

Anapenda kuishi mazingira ya kawaida sana
 
Dr Mpango, ni Mrundi. Waikumbuka hii??
View attachment 3207870
Yaani Dr. Mpango amekuwa mrundi baada tu ya kuwa makamu wa rais?
Huyo dingi amekuwa kwenye system nyeti za serikali tangu kipindi cha Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia na kipindi chote hatukujua ni mrundi? Nani sasa ni mtanzania?

Okay, leo ndio tumegundua ni mrundi kwanini sasa mpaka November ataendelea kuwa makamu wa rais, na baada ya hapo ataendelea kupewa stahiki zote za makamu wa rais yeye na mkewe mpaka kaburini?
 
Mleta mada ana element za ukweli.Dr. Philip Mpango ni mnyenyekevu , hana makuu . Hana tamaa ya madaraka.

Mimi kuna wakati mwaka juzi niliwahi kwenda Chanika nilikuwa naenda kufanya issue zangu. Sasa kuna barabara ilikuwa inatengenezwa mahali fulani na ni kama ilikuwa inatumika angali maengeneer wanaendelea na kazi zao . Nikawa namuambia mwenyeji wangu hii barabara itachelewa sana kuisha, kwa nini wameruhusu itumike akati bado inatengenezwa ? Mwenyeji wangu kule Chanika akasema itaisha tu maana inaenda kwa makamu wa rais. Nikashangaa , " Makamu wa rais anaishi Chanika!!!". Chanika ambayo wakazi wengi wa Dar es Salaam wanaona kama watu wanaoishi Chanika ni watu wa hadhi ya chini.

Hili tu linatosha kutuonesha Dr.Philip Mpango ni mtu wa aina gani. Jamaa ni mnyenyekevu.Anapenda kuwa karibu na wananchi wake wa hali ya chini.
Kumbe anaishi Mbondole?
 
Mtaje makamu yeyote yule aliyewahi kukemea mambo ya boss wake
Wapo wengi.
Kwa uchache hapa Tanzania nitakutajia watatu hapa.
1. Abeid Aman Karume. Akiwa makamu wa rais wa Nyerere alipinga Azimio la Arusha, na kwa jeuri AKAKEMIA na kupiga marufuku azimio lile kufika Zanzibar.

2. Abdu Jumbe, akiwa makamu wa rais wa Nyerere alipinga muundo wa muungano na KUKEMEA uhuni wa muungano kuimeza Zanzibar uliokuwa akifanywa na Nyerere.

3. John Malecella, akiwa makamu wa rais wa Mwinyi alipingana na sera ya serikali mbili, akaunga mkono hoja ya kutaka kuwepo serikali ya tatu ya Tanganyika na kwa ujasiri AKAKEMIA watendaji wa serikali kuwabughudhi wabunge wa G55 kinyume na takwa la boss wake.

Kwa Zanzibar wapo wawili, kwa uchache ni Maalim Seif Sharif Hamad na Othman Masoud Othman.

Kwa Kenya wapo wengi sana, wa siku za karibuni ni Gachagua.
 
Nini kiliwakuta na walibadilisha chochote?
 
Hivi lini ulimuona Dr. Mpango akikemea na kulaani mojawapo katika haya mambo:
1. Utekaji na mauaji ya wakosoaji wa serikali.
2. Uchafuzi katika uchaguzi wa 2019, 2020, 2024.
3. Uuzwaji wa bandari za Tanganyika
4. Kufukuzwa kwa wamasai kule Ngorongoro
5. Wizi na ufisadi uliokithiri ndani ya serikali.

Kwangu mimi, Dr. Mpango ni miongoni mwa watu wa ovyo kabisa kuwahi kushika nafasi za juu katika serikali yetu. Hakuwa na sifa zozote za kutuvutia kabla ya kuteuliwa na ameshindwa kujenga sifa zozote hata baada ya kuteuliwa. Ni bure kabisa.
Ulitaka hilo? Ameondoka pambana na hali yako
 
Yule dingi anapenda madaraka na vyeo vya mserereko balaa. Kipindi yuko hoi hospitalini akiuguzwa Covid, bado alikomaa tu kuendelea kukalia kiti cha uwaziri na akiwa hoi bin taabani akajikongoja kuja hadharani kuongea ili alinde ulaji wake na ulaji wa aliyemteua.
Wenzio wa Yanga hawanaga akili kwenye mambo ya mpira tu, lakini wewe hadi kwenye siasa ni hamnazo.
 
Back
Top Bottom