Dkt. Mpango ndio aina ya wazee tunawataka kwenye Taifa. Hana makuu, hana tamaa ya madaraka

Dkt. Mpango ndio aina ya wazee tunawataka kwenye Taifa. Hana makuu, hana tamaa ya madaraka

Hivi lini ulimuona Dr. Mpango akikemea na kulaani mojawapo katika haya mambo:
1. Utekaji na mauaji ya wakosoaji wa serikali.
2. Uchafuzi katika uchaguzi wa 2019, 2020, 2024.
3. Uuzwaji wa bandari za Tanganyika
4. Kufukuzwa kwa wamasai kule Ngorongoro
5. Wizi na ufisadi uliokithiri ndani ya serikali.

Kwangu mimi, Dr. Mpango ni miongoni mwa watu wa ovyo kabisa kuwahi kushika nafasi za juu katika serikali yetu. Hakuwa na sifa zozote za kutuvutia kabla ya kuteuliwa na ameshindwa kujenga sifa zozote hata baada ya kuteuliwa. Ni bure kabisa.
Kimfumo ni ngumu kwenda kinyume na Boss anaekuongoza na wewe ukiwa ndani ya system!!

Swala Zima la teka teka ni kiza kulielewa coz system ndio inatujua kwa kina Sana baada ya Mungu inafuata system ya usalama ya nchie!!

Kuna watu wameonewa katika process ya upelelezi wa system nankupoteza maisha na Kuna wengine ukiambiwa uchafu wao utatamani walichofnyiwa ni sahihi!

No vile hatujui mengi na system Huwa haijielezi kwa yeyote!
 
Ukimuona mtu anamsema vibaya Mh Dr Mapango basi juwa nimaumivu na chuki kubwa juu yake kwa uwamuzi wakupiga chini nafasi ya Umakamu wa Rais na kurudi back benches.

Ndie waziri pekee wa fedha alie kuwa akiishi nyumbani na sio kwenye pepo za baharini na hii ndio siri yakupendwa kwake na Hayati Magufuli kiasi kupiga simu akiwa hospitali amuone na Watanzania wamuone.
Dr Mpango ndie Eng wa uchumi na mambo yote mnayaona na huyo waziri mtaka sifa pale ametemebelea sana nyota ya huyu Dr Mpango.

Uwezo na akili alizo nazo ziliwavutia wakubwa zake kumsogeza karibu kuanzia JK mpaka Magufuli.

Nimoja ya nyota na tunu tulizo nazo katika Taifa ni bahati mbaya hakushika kiti kwasababu za kibinadam au Mungu mwenyewe. Sio chawa ila nimsema kweli nainaonyesha anachukia uchawa na ameuchukia uchawa kwa maandishi. "Naomba nipumzike"

Huyu ndio aina ya kiongozi tunamuhitaji nina amini JK amelia alipojuwa huyu mwamba ameamua kupumzika ila walamba miguu tumefanya part maana alikuwa mnoko sana kuzuwia vimeo vyetu. Yes hakuna anaweza kuja nakusema vile Dr Mpango nimsumari wa moto kwa majizi ya wizarani na kwenye mfumo.

Hana deal ila peleka pesa bank ya serikali nakama una zawadi kumtunuku basi peleka kwenye akaunti yaserikali mama na mtoto wapate huduma bora ni mwana mapinduzi na mzawa wa kweli katika uzalendo kwa taifa lake.

Nafasi ya umakamu wa Rais ndio ilimtoa home sweet hoem kwenda baharini ila yaonyesha hakukupenda na ameamua rudi nyumbani. Akafuge kuku na kucheza na ujukuu wake huku akikielimisha kizazi kijacho juu ya uzalendo.

Mh Dr Mapango amekuwa mnyenyekevu nakufia ukweli huku akiepuka laana ya Hayati Magufuli kwa yote yanasemwa ameamua kuacha kabisa akijuwa hakuna atake ishi milele na mwamba alikufa akisimamia watu wake wa Tanzania kwa dam na nyama.

Alikuwa nikipenzi cha Magu na amekubali kukaaa pembeni kuipisha gharika ya pili ukiacha ile ya kwanza kwa wale wakiroho tunamuona kama mtu anayo iyona kesho baada ya uchaguzi. Yale yatatokea na kile kitatokea hataki kuwa mmoja wa hayo.

Upo msemo unasema koti lakuazima usilifanye likawa la kwako na cheo chochote kina gharama ametimiza ahadi hiyo kwa gharama kubwa kwakuamini serikali ilimuamini kwa tatizo Taifa lilitupata hivyo anawashukuru na kwarudishia cheo chao ili wengine wachukue usukani ameishinda Tamaa na amemshinda shetani.

Soma Pia: Dkt. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu wa Rais, Rais Samia aridhia ombi hilo

Hakutaka kufanana na Mungu pamoja na uwezo wote aliokuwa nao hakutaka makuu amejikubali naomba viongozi wote tujifunze kwa Dr Mpango.

Taifa lilikumbwa na msiba mzito nakama sio ule msiba asingekuwa makamu wa Rais je kwanini aendelee kushika nafasi kwa ubabe na fitina wakati alipewa kama hisani na upendeleo wa Mungu.

Dr Mpango moyo wake ukamkumbusha usitamani jambo hukuandaliwa na yakuwa nafasi kubwa kama yake niupendeleo toka kwa Mungu na taifa lina watu sio yeye peke yake basi akang'atuka huu ni uzalendo mkubwa sana.

Dr Mpango wajinga wachache watabeza msimamo wako ila nataka nikuhakikishie mbingu zitasimama uwone yote yatatokea ili umtukuze Mungu na uzao wako. Wewe ni mshindi wewe ni simba na Mungu azidi kukulinda kwa Makerubi wake asubuh, mchana na usiku. Amen
Asante sana
 
Kimfumo ni ngumu kwenda kinyume na Boss anaekuongoza na wewe ukiwa ndani ya system!!

Swala Zima la teka teka ni kiza kulielewa coz system ndio inatujua kwa kina Sana baada ya Mungu inafuata system ya usalama ya nchie!!

Kuna watu wameonewa katika process ya upelelezi wa system nankupoteza maisha na Kuna wengine ukiambiwa uchafu wao utatamani walichofnyiwa ni sahihi!

No vile hatujui mengi na system Huwa haijielezi kwa yeyote!
Elimu uliyo soma kwa haki inakufanya unakuwa mtu makini sana.

Huwezi kufanya kazi na watu wanaomchafua mtangulizi wao kwa makusudi. Haijawahi kutokea watangulizi kuchafuana

Ila huyu mama na kundi la msoga…. Linamkosea heshima sana the late….. alipokuwa hai, hawakuweza kufanya hayo
 
Yule dingi anapenda madaraka na vyeo vya mserereko balaa. Kipindi yuko hoi hospitalini akiuguzwa Covid, bado alikomaa tu kuendelea kukalia kiti cha uwaziri na akiwa hoi bin taabani akajikongoja kuja hadharani kuongea ili alinde ulaji wake na ulaji wa aliyemteua.
Hakuna Uhusiano ……. Upo manipulated
 
Jamaa alivyokuwa Waziri wa Fedha alimuwekea mustendi Makonda alipe kodi za vifaa vya shule, kodi qmbayo Makonda alitaka kutuzungusha asilipe.

Wakati huo Makonda mtoto mpendwa wa Magufuli kila mtu alikuwa anamuogopa, ila Dr. Mpango akamuondolea uvivu.
Dr ni mtu makini sana . Kuna level fulan za maisha ukifika, vyeo na utumwa wa fikra vinakuwa havina nafasi tena
 
Kile kidingi tunaelezwa na wanyetishaji kuwa ni kikuda, kizandiki na kipigaji balaa. Maza amekuja kukishtukia dakika za lala salama na kukifyatua nje, hisia za watu wa karibu na mama ni kuwa, kikiendelea kukalia kile kutu, ipo siku huenda kingetengua kiti kikuu.
Hiz ni Speculation . Toa evidence ya upigaji wowote wa Mpango au toa project ya ufisadi aliyoshiriki na sisi tutoe za huyo Boss wako!

Toa kashfa yoyote ya mpango juu ya upigaji? Otherwise ni hater
 
Nini kiliwakuta na walibadilisha chochote?
Karibu wote niliowataja walipoteza vyeo vyao lakini walitengeneza aina fulani ya legacy yao. Na hii ndio hoja hapa.
Dr. Mpango hana legacy yoyote ya kimsimamo aliyoijenga au ataiacha mpaka kuamua kujiuzuru.
 
Mpango kapoa kama uji wa juzi. Kama mnampenda sana mchukueni hana tija.
 
Ila kama ni unyenyekevu (humility), ucha Mungu, Elimu/Maarifa, maadili na uzalenfo huyu dingi Mzee Mpango amebarikiwa sana.
Nimefanya ka kazi flan pale Tume ya Mipango, Mzee huyu akiwa Bosi pale, kiekweli Mzee huyu ni gifted kwenye vitu vingi.
Jiwe hakumpenda bure huyu Dingi.
 
Sijasema alilipa. Wala sijafika huko kwamba alilipa au hakulipa. Hiyo si sehemu ya mjadala wangu.

Nilichosema ni kwamba, wakati Makonda alikuwa mtu wa kuogopwa sana na watu karibu wote serikalini, kutokana na ukaribu wake na Magufuli, Dr. Philip Mpango alisimama kama mtu pekee ambaye alisimamia kanuni na kukataa kumsujudia Makonda. Akasema alipe kodi.

That alone was something kwa sababu Makonda alikuwa hajawahi kuwa challenged vile serikalini. Na ule ndio ulikuwa mwanzo wa Makonda kuanguka kutoka kuwa Magufuli's golden boy mpaka kukaa bench.

Sasa kama Makonda alilipa au hakulipa hatuna ushahidi wowote mpaka sasa, hata wewe hujaweka ushahidi kwamba Makonda hakulipa.

Na huko sijasema lolote nimesema tu kwamba Dr. Mpango alinyoosha mstari na hakuogooa kumwambia Makonda alipe kodi mchana kweupe.

Kitu ambacho watu wengine serikalini hawakuthubutu kum contradict Makonda.

Unataka kubishia hii fact au unataka kuleta ubishi wa logical non sequitur fallacy kuhusu mambo ambayo hata sijayasema unajiongezea mwenyewe tu?
Ni kweli, zile furniture hakupewa makonda baada ya kushindwa kulipa kodi, wizara ilizigawa kwa utaratibu wake. Makonda alikua mpaka jiwe mwenyewe anamuogopa. Wakati jiwe akiongelea hilo suala la makonda alikua akitetemeka! Sauti na sura unaona huyu mtu kasanda. Makonda mpaka kesho serikalini hawampendi na hata mawaziri wakienda Chuga wanajinyenyekeza kwake!
 
Hiz ni Speculation . Toa evidence ya upigaji wowote wa Mpango au toa project ya ufisadi aliyoshiriki na sisi tutoe za huyo Boss wako!

Toa kashfa yoyote ya mpango juu ya upigaji? Otherwise ni hater
Kwani hoja hapa ni nini?
Mleta mada ametengeneza hoja duni na mbovu ya kufikirika kuhusu msimamo wa Dr. Mpango kwenye issue za maslahi ya kitaifa.

Mimi nimehoji, ni kipi katika maslahi ya taifa Dr. Mpango aliamua kusimama nacho kiasi cha kuhisi huenda ndio kimezaa kujiuzuru kwake. Jibu HAKUNA.
 
Yule dingi anapenda madaraka na vyeo vya mserereko balaa. Kipindi yuko hoi hospitalini akiuguzwa Covid, bado alikomaa tu kuendelea kukalia kiti cha uwaziri na akiwa hoi bin taabani akajikongoja kuja hadharani kuongea ili alinde ulaji wake na ulaji wa aliyemteua.
Mkuu,

Umefanya judgement call kusema anapenda nadaraka bila kuangakia kuwa.

1. Inawezekana aliamrishwa.
2. Inawezekana alifanya vike akiamini kwa moyo wake wote jwamba ni kitu cha uzalendo, uchapakazi na uadilifu kulitumikia taifa lako hata ukiwa na haki ile.

Zaidi, mtu anayependa madaraka haandiki barua ya kujiuzulu umakamu wa rais.

Dr. Mpango si mwanasiasa, ni mtu ambaye vyeo vya kisiasa vinamfuata yeye kwa sababu ya credentials zake.

Angekuwa mwanasiasa tungeona anaendelea kuwa makamu wa rais wa Samia na pengine anajipanga kuwa rais baada ya Samia.
 
Ila kama ni unyenyekevu (humility), ucha Mungu, Elimu/Maarifa, maadili na uzalenfo huyu dingi Mzee Mpango amebarikiwa sana.
Nimefanya ka kazi flan pale Tume ya Mipango, Mzee huyu akiwa Bosi pale, kiekweli Mzee huyu ni gifted kwenye vitu vingi.
Jiwe hakumpenda bure huyu Dingi.
Mcha Mungu gani au mtu mwenye ubinadamu anayeweza kukaa kimya watu wakiuwawa, kuteswa, kupotezwa?

Ni mzalendo gani anayeweza kukaa kimya rasimali zikiibwa?
 
Ni kweli, zile furniture hakupewa makonda baada ya kushindwa kulipa kodi, wizara ilizigawa kwa utaratibu wake. Makonda alikua mpaka jiwe mwenyewe anamuogopa. Wakati jiwe akiongelea hilo suala la makonda alikua akitetemeka! Sauti na sura unaona huyu mtu kasanda. Makonda mpaka kesho serikalini hawampendi na hata mawaziri wakienda Chuga wanajinyenyekeza kwake!
Za chinichini ni kwamba Jiwe alikuwa anatokewa na mauzauza Ikulu, Makonda ndiye akawa mtu pekee anayeweza kuleta waganga wa kuyatuliza mauzauza hayo.

Ndiyo maana alikuwa ana nguvu sana kwa Jiwe, nq hii ni moja ya sababu Jiwe alikazia sana issue ya kuhamia Dodoma.

This is not to say that I believe in witchcraft, this is to say there is such a thing as belief in witchcraft which has real effects.
 
Mkuu,

Umefanya judgement call kusema anapenda nadaraka bila kuangakia kuwa.

1. Inawezekana aliamrishwa.
2. Inawezekana alifanya vike akiamini kwa moyo wake wote jwamba ni kitu cha uzalendo, uchapakazi na uadilifu kulitumikia taifa lako hata ukiwa na haki ile.

Zaidi, mtu anayependa madaraka haandiki barua ya kujiuzulu umakamu wa rais.

Dr. Mpango si mwanasiasa, ni mtu ambaye vyeo vya kisiasa vinamfuata yeye kwa sababu ya credentials zake.

Angekuwa mwanasiasa tungeona anaendelea kuwa makamu wa rais wa Samia na pengine anajipanga kuwa rais baada ya Samia.
Mkuu acha kutengeneza dhana ya kufikirika wakati uhalisia uko wazi.
Huyu mzee kwa miaka minne hii iliyokwisha muda mwingi ameutumia kulazwa, kutibiwa, kusafiri nje na kupumzishwa. Kwa kifupi, Dr. Mpango alikuwa unproductive katika utendaji wa baraza la mawaziri. Kwanini hakuachia madaraka mapema?
 
Za chinichini ni kwamba Jiwe alikuwa anatokewa na mauzauza Ikulu, Makonda ndiye akawa mtu pekee anayeweza kuleta waganga wa kuyatuliza mauzauza hayo.

Ndiyo maana alikuwa ana nguvu sana kwa Jiwe, nq hii ni moja ya sababu Jiwe alikazia sana issue ya kuhamia Dodoma.

This is not to say that I believe in witchcraft, this is to say there is such a thing as belief in witchcraft which has real effects.
Maybe, because as mere RC He had a lot of powers. Na jamaa alivyo kibri alitukana kila mtu aliyepita mbele yake. Isivyo bahati karudi kwenye system. Nadhani system inataka vichaa kadhaa ... Rais yeyote anayejiheshimu hawezi kuwachagua Makonda na Chalamila. They are hard working ila midomo yao ni michafu mno
 
Za chinichini ni kwamba Jiwe alikuwa anatokewa na mauzauza Ikulu, Makonda ndiye akawa mtu pekee anayeweza kuleta waganga wa kuyatuliza mauzauza hayo.

Ndiyo maana alikuwa ana nguvu sana kwa Jiwe, nq hii ni moja ya sababu Jiwe alikazia sana issue ya kuhamia Dodoma.

This is not to say that I believe in witchcraft, this is to say there is such a thing as belief in witchcraft which has real effects.
Kiranga anayesema haamini kwenye imani ya uwepo wa Mungu na Shetani, ndio Kiranga huyo huyo anayekuja kutuaminisha hapa kuwa Magufuli alikuwa anakumbana na nguvu za mashetani pale Ikulu ta magogoni!!

Mungu yupo jamani.
 
Mkuu acha kutengeneza dhana ya kufikirika wakati uhalisia uko wazi.
Huyu mzee kwa miaka minne hii iliyokwisha muda mwingi ameutumia kulazwa, kutibiwa, kusafiri nje na kupumzishwa. Kwa kifupi, Dr. Mpango alikuwa unproductive katika utendaji wa baraza la mawaziri. Kwanini hakuachia madaraka mapema?
Unajuaje kwamba hakutaka kuachia mapema na kuambiwa asubiri mpaka mwaka wa uchaguzi?

Unajua hata Samia alipokosa kuelewana na Magufuli alitaka kujiuzulu umakamu wa rais, akaambiwa asubiri hapo hapo dawa inachemka?

Upo katika mfumo ambao usiri ni kawaida halafu unauliza jambo ambalo si mimi wala wewe anayeweza kuwa na majibu ya uhakika.

Halafu wewe ndiye unaniambia mimi niache kutengeneza dhana ya kufikirika?

Huoni hapo umetengeneza tuhuma za "nyani haoni kundule" ?
 
Back
Top Bottom