Dkt. Mpango ndio aina ya wazee tunawataka kwenye Taifa. Hana makuu, hana tamaa ya madaraka

Nini kilitokea?
Makonda alilipa ile kodi?

Muwe na kumbukumbu, hakuna chochote kililipwa katika lile sakata.
Sijasema alilipa. Wala sijafika huko kwamba alilipa au hakulipa. Hiyo si sehemu ya mjadala wangu.

Nilichosema ni kwamba, wakati Makonda alikuwa mtu wa kuogopwa sana na watu karibu wote serikalini, kutokana na ukaribu wake na Magufuli, Dr. Philip Mpango alisimama kama mtu pekee ambaye alisimamia kanuni na kukataa kumsujudia Makonda. Akasema alipe kodi.

That alone was something kwa sababu Makonda alikuwa hajawahi kuwa challenged vile serikalini. Na ule ndio ulikuwa mwanzo wa Makonda kuanguka kutoka kuwa Magufuli's golden boy mpaka kukaa bench.

Sasa kama Makonda alilipa au hakulipa hatuna ushahidi wowote mpaka sasa, hata wewe hujaweka ushahidi kwamba Makonda hakulipa.

Na huko sijasema lolote nimesema tu kwamba Dr. Mpango alinyoosha mstari na hakuogooa kumwambia Makonda alipe kodi mchana kweupe.

Kitu ambacho watu wengine serikalini hawakuthubutu kum contradict Makonda.

Unataka kubishia hii fact au unataka kuleta ubishi wa logical non sequitur fallacy kuhusu mambo ambayo hata sijayasema unajiongezea mwenyewe tu?
 
Mleta mada ana element za ukweli.Dr. Philip Mpango ni mnyenyekevu , hana makuu . Hana tamaa ya madaraka.

Mimi kuna wakati mwaka juzi niliwahi kwenda Chanika nilikuwa naenda kufanya issue zangu. Sasa kuna barabara ilikuwa inatengenezwa mahali fulani na ni kama ilikuwa inatumika angali maengeneer wanaendelea na kazi zao . Nikawa namuambia mwenyeji wangu hii barabara itachelewa sana kuisha, kwa nini wameruhusu itumike akati bado inatengenezwa ? Mwenyeji wangu kule Chanika akasema itaisha tu maana inaenda kwa makamu wa rais. Nikashangaa , " Makamu wa rais anaishi Chanika!!!". Chanika ambayo wakazi wengi wa Dar es Salaam wanaona kama watu wanaoishi Chanika ni watu wa hadhi ya chini.

Hili tu linatosha kutuonesha Dr.Philip Mpango ni mtu wa aina gani. Jamaa ni mnyenyekevu.Anapenda kuwa karibu na wananchi wake wa hali ya chini.
 
Leo kakuachieni akiwa na nguvu zake kamili, utasemaje huu ujinga uloandika hapa?
 
Basi kama alikuwa hivyo mafisadi ni lazima wamchukie na hivi sasa watakuwa wamefurahi sana 😳
 
Mtaje makamu yeyote yule aliyewahi kukemea mambo ya boss wake
 
Dodoma pia Anakaa Kule Zuzu

Maaurufu kama kwa Mzee Pinda


Anapenda kuishi mazingira ya kawaida sana
 
Dr Mpango, ni Mrundi. Waikumbuka hii??
View attachment 3207870
Yaani Dr. Mpango amekuwa mrundi baada tu ya kuwa makamu wa rais?
Huyo dingi amekuwa kwenye system nyeti za serikali tangu kipindi cha Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia na kipindi chote hatukujua ni mrundi? Nani sasa ni mtanzania?

Okay, leo ndio tumegundua ni mrundi kwanini sasa mpaka November ataendelea kuwa makamu wa rais, na baada ya hapo ataendelea kupewa stahiki zote za makamu wa rais yeye na mkewe mpaka kaburini?
 
Kumbe anaishi Mbondole?
 
Mtaje makamu yeyote yule aliyewahi kukemea mambo ya boss wake
Wapo wengi.
Kwa uchache hapa Tanzania nitakutajia watatu hapa.
1. Abeid Aman Karume. Akiwa makamu wa rais wa Nyerere alipinga Azimio la Arusha, na kwa jeuri AKAKEMIA na kupiga marufuku azimio lile kufika Zanzibar.

2. Abdu Jumbe, akiwa makamu wa rais wa Nyerere alipinga muundo wa muungano na KUKEMEA uhuni wa muungano kuimeza Zanzibar uliokuwa akifanywa na Nyerere.

3. John Malecella, akiwa makamu wa rais wa Mwinyi alipingana na sera ya serikali mbili, akaunga mkono hoja ya kutaka kuwepo serikali ya tatu ya Tanganyika na kwa ujasiri AKAKEMIA watendaji wa serikali kuwabughudhi wabunge wa G55 kinyume na takwa la boss wake.

Kwa Zanzibar wapo wawili, kwa uchache ni Maalim Seif Sharif Hamad na Othman Masoud Othman.

Kwa Kenya wapo wengi sana, wa siku za karibuni ni Gachagua.
 
Nini kiliwakuta na walibadilisha chochote?
 
Ulitaka hilo? Ameondoka pambana na hali yako
 
Wenzio wa Yanga hawanaga akili kwenye mambo ya mpira tu, lakini wewe hadi kwenye siasa ni hamnazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…