Dkt. Mpango ni kweli ulishiriki kumtuma Sabaya kufanya mambo machafu?

Dkt. Mpango ni kweli ulishiriki kumtuma Sabaya kufanya mambo machafu?

Watanzania wagumu kweli kuelewa. Kuna upotoshaji mkubwa sana unaendelea. Sabaya amesema alienda Arusha kwa maagizo ya mamlaka iliyomteua.

Prof. Lunga (Gavana) na Dr. Mpango (aliyekuwa Waziri wa fedha) wametajwa kama watu wanaojua moja ya kazi maalum aliyowahi kuifanya huko Dar es Salaam baada ya kukamata machine ya kutengezea fedha bandia.

Na amesema hivyo ili kuonesha kuwa kuna kazi nyingi tu aliwahi kuzifanya nje ya eneo lake la kawaida la kazi. Hiyo ya kwenda Arusha haikuwa ya kwanza.

Pamoja na hayo, amekanusha kuiba fedha wala kutumia silaha. Kila alichokuwa anakifanya alipata ushirikiano wa vyombo vya dola. Hata aliyekuwa mkuu wa wilaya wa eneo husika alikuwa na taarifa juu ya uwepo wao.

Kwa maneno mengine alikuwa kwenye kazi maalum aliyotumwa na mamlaka ya uteuzi wake: siyo Dr. Mpango, Prof. Luoga au hao wengine aliowataja.
Hao wengine unawaondoaje bila wenyewe kujiondoa
 
Yani kitu nnachokiona sasa ni kama ile movie ya Kara sevda, kila kitu kibaya kinakuwa covered na marehemu simply because hawezi kujibu!
Marehemu aliyataka mwenyewe. Huko aliko moto una double
 
Bora yako wewe yote yaliyokukuta lakini upo uraiani ukiwa huru,kuliko walio mahabusu kama Sabaya,Mbowe na wengine wasio jua hatma yao.beti kistaarabu kamali ni bahati tu.
Bora walio mahabusu bado wanapumua na wana Imani siku moja watakuwa huru. Je waliojifanya majeuri na sasa wako kuzimu kama akina Jpm vipi?
 
Kwanza kutumwa Na mamlaka sio shida je alifanya makosa hayo au hakufanya. Je maagizo hayo yalikua halali yanathibitika.
Naona kuna jinai nyingi Kwa Sabaya basi liandaliwe file maalumu ahojiwe matukio yote aliyofanya nafahamu alifanya pia kwa kina Mehboob wa Tanga Na kuiba zaidi ya milioni mia tatu. Vyombo vya dola mtafuteni kijana Ally Mehboob wa Tanga atatoa maelezo mazuri. Hili lilikua genge la uhalifu likitumia kivuli cha Rais.
 
Mnajikuta miungu sana nyie, anaehukumu ni Mungu na sio mwanadamu, hata wewe utakufa ila huna uhakika kama hutaenda motoni!
Matendo yake yanamhukumu. Ukiwa wa dhambi utaishia motoni tu.
 
Kwanza kutumwa Na mamlaka sio shida je alifanya makosa hayo au hakufanya. Je maagizo hayo yalikua halali yanathibitika.
Naona kuna jinai nyingi Kwa Sabaya basi liandaliwe file maalumu ahojiwe matukio yote aliyofanya nafahamu alifanya pia kwa kina Mehboob wa Tanga Na kuiba zaidi ya milioni mia tatu. Vyombo vya dola mtafuteni kijana Ally Mehboob wa Tanga atatoa maelezo mazuri. Hili lilikua genge la uhalifu likitumia kivuli cha Rais.
Under Magufuli kulikuwa na magenge mengi ya uhalifu.
 
Wwe uhakimu hakufai kabisa! Sabaya ndiyo kasema alitumwa na Mamlaka kufanya kazi maalumu,na ameisema ni kazi gani aliyotumwa,ikiwa na pamoja kufuatilia watu wenye mtambo wa kutengenezea noti bandia! Jirizishe kwanza hapo je ni kweli alitumwa na Mamlaka kwa kazi hiyo!? Au ni porojo tu!? Alafu ndiyo uje na malalamiko yako ya kumtuhumu Sabaya!!
 
Habari za midaa hii wa Jamii forums.

Leo tarehe 13 agosti kumetrendi ktk mitandao ya kijamii kile kinachoitwa no utetezi mahakamani wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya DC Sabaya.

Imeelezwa kuwa amekiri kilichokuwa kikifanyika ama alichokuwa anatekeleza ktk kesi yake ya unyanganyi kwa kutumia siraha aliagizwa na Dr Mpango, Hayati Dr J Magufuli na Gavana wa Fedha bwana Luoga.

Naamini Ndugu Sabaya amefika hatua hii baada ya kuona hakuna namna ya kuchomoka ktk kesi hii au akaona akitupia majina haya Makubwa makubwa itakua ni njia ya nitoke vipi.

Licha ya kile kinachoendelea huko mahakamani iwe ni kweli si kweli, kutajwa kwa Makamu wa Rais Mh Dr Mpango kunatia doa juu ya uhalali ktk utendaji wake kama kweli anaweza kushiriki ktk vitendo vya kihalifu na baafaya akaonekana anafaa kushika nafasi nyeti ktk nchi yetu.

Sisi tunaomuunga mkono na kumwamini kama Kiongozi Safi mwenye weledi na maadili na msomi wa kiwango cha juu tumesikitishwa na kadhia hii ya kutajwa kwenye mambo maovu.

Watanzania tunaompenda tunapenda kutoa wito ajitokeze ama mahakamani au kwenye jukwa la wazi ajisafishe na tuhuma hizi nzito.

View attachment 1891471
JamiiForums-829252439.jpg
 
Afungwe tu
Ufahamu wake wa kutambua mema na mabaya aliupeleka wapi?
Afungwe tuu.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Afungwe kivipi wakati hakuna ushahidi wa kutosha kumfunga!? Labda Mpango aje Mahakamani aseme hawajawai kumtuma Sabaya kufanya kazi maalumu ya kuwasaka wahujumu Uchumi!!
 
Back
Top Bottom