Dkt. Mpango ni kweli ulishiriki kumtuma Sabaya kufanya mambo machafu?

Dkt. Mpango ni kweli ulishiriki kumtuma Sabaya kufanya mambo machafu?

Watanzania wagumu kweli kuelewa. Kuna upotoshaji mkubwa sana unaendelea. Sabaya amesema alienda Arusha kwa maagizo ya mamlaka iliyomteua.

Prof. Lunga (Gavana) na Dr. Mpango (aliyekuwa Waziri wa fedha) wametajwa kama watu wanaojua moja ya kazi maalum aliyowahi kuifanya huko Dar es Salaam baada ya kukamata machine ya kutengezea fedha bandia.

Na amesema hivyo ili kuonesha kuwa kuna kazi nyingi tu aliwahi kuzifanya nje ya eneo lake la kawaida la kazi. Hiyo ya kwenda Arusha haikuwa ya kwanza.

Pamoja na hayo, amekanusha kuiba fedha wala kutumia silaha. Kila alichokuwa anakifanya alipata ushirikiano wa vyombo vya dola. Hata aliyekuwa mkuu wa wilaya wa eneo husika alikuwa na taarifa juu ya uwepo wao.

Kwa maneno mengine alikuwa kwenye kazi maalum aliyotumwa na mamlaka ya uteuzi wake: siyo Dr. Mpango, Prof. Luoga au hao wengine aliowataja.
JamiiForums-829252439.jpg
 
Yani kitu nnachokiona sasa ni kama ile movie ya Kara sevda, kila kitu kibaya kinakuwa covered na marehemu simply because hawezi kujibu!
Usijali , Mpango na Gavana bado wapo hai na wametajwa Mahakamani,kwa hiyo ni jukumu la Mahakama kuwaita au kuwafuata ili ijirizishe kabla ya kutoa hukumu!!
 
Habari za midaa hii wa Jamii forums.

Leo tarehe 13 agosti kumetrendi ktk mitandao ya kijamii kile kinachoitwa no utetezi mahakamani wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya DC Sabaya.

Imeelezwa kuwa amekiri kilichokuwa kikifanyika ama alichokuwa anatekeleza ktk kesi yake ya unyanganyi kwa kutumia siraha aliagizwa na Dr Mpango, Hayati Dr J Magufuli na Gavana wa Fedha bwana Luoga.

Naamini Ndugu Sabaya amefika hatua hii baada ya kuona hakuna namna ya kuchomoka ktk kesi hii au akaona akitupia majina haya Makubwa makubwa itakua ni njia ya nitoke vipi.

Licha ya kile kinachoendelea huko mahakamani iwe ni kweli si kweli, kutajwa kwa Makamu wa Rais Mh Dr Mpango kunatia doa juu ya uhalali ktk utendaji wake kama kweli anaweza kushiriki ktk vitendo vya kihalifu na baafaya akaonekana anafaa kushika nafasi nyeti ktk nchi yetu.

Sisi tunaomuunga mkono na kumwamini kama Kiongozi Safi mwenye weledi na maadili na msomi wa kiwango cha juu tumesikitishwa na kadhia hii ya kutajwa kwenye mambo maovu.

Watanzania tunaompenda tunapenda kutoa wito ajitokeze ama mahakamani au kwenye jukwa la wazi ajisafishe na tuhuma hizi nzito.

View attachment 1891471
Iv kwann mwandishi hapo haja wapa hadhi yao ya elimu hayati magu na Luoga ..? Ame sema tu Dkt.Mpango ..
Angesema Dkt Magufuli, Dkt Mpango na Prof.Luoga
 
Watanzania wengi ni wagumu kuelewa ama wavivu wa kutafakari.

Sijaona mahala Sabaya akisema Mpango ama Luoga walishiriki kumtuma bali alitumwa na mamlaka yake ya uteuzi na hao jamaa aliowataja wanajua hilo.

Sioni ni kwa namna gani hao jamaa wanahusishwa.
 
Bora walio mahabusu bado wanapumua na wana Imani siku moja watakuwa huru. Je waliojifanya majeuri na sasa wako kuzimu kama akina Jpm vipi?
Hata wwe na mimi ipo siku yetu tutanyakuliwa na umauti,ni swala la muda tu!!
 
Kwa jeuri aliyokuwa nayo huyo dogo inahitaji hata degree kujua haya matendo yake na maagizo yalianzia wapi?
 
Kwanza kutumwa Na mamlaka sio shida je alifanya makosa hayo au hakufanya. Je maagizo hayo yalikua halali yanathibitika.
Naona kuna jinai nyingi Kwa Sabaya basi liandaliwe file maalumu ahojiwe matukio yote aliyofanya nafahamu alifanya pia kwa kina Mehboob wa Tanga Na kuiba zaidi ya milioni mia tatu. Vyombo vya dola mtafuteni kijana Ally Mehboob wa Tanga atatoa maelezo mazuri. Hili lilikua genge la uhalifu likitumia kivuli cha Rais.
Mbona huyo Sabaya hajawai kuja kwangu!? Mpaka kawafuaata hao inamaana wanajuwana wanayofanya sirini!!
 
KIKUBWA SABAYA AKABIDHI BARUA AU NYARAKA ZINAZOTHIBITISHA HAYO
au ukitaja tu basi unakua ushahidi
 
Unasema kama ni kweli alimtuma Sabaya kufanya mambo ya hovyo ajitokeze ajisafishe?Yaani badala ya kusema kuwa ajitokeze awajibike unasema kuwa ajitokeze ajisafishe?!Tokea nizaliwe sijawahi kuona akili ndogo kama hii🚶🚶🚶
 
hakuna kesi hapo.
kama alikuwa anatekeleza majukumu yake aliyo elekezwa na aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu ktk kuhakikisha kodi ya Serikali inalipwa. sasa huo unawezaje kuuita eti ni unyang'anyi?!!
ukiangalia hii kesi kwa jicho la tatu imejaa kisasi dhidi ya sabaya kutokana na majukumu yake aliyo kuwa akiyatekeleza, kwa vyovyote vile lazima angechukiwa sana na either;
1. wafanyabiashara au wanasiasa au wote kwa pamoja. ndicho kilicho tokea.
 
Watanzania wagumu kweli kuelewa. Kuna upotoshaji mkubwa sana unaendelea. Sabaya amesema alienda Arusha kwa maagizo ya mamlaka iliyomteua.

Prof. Lunga (Gavana) na Dr. Mpango (aliyekuwa Waziri wa fedha) wametajwa kama watu wanaojua moja ya kazi maalum aliyowahi kuifanya huko Dar es Salaam baada ya kukamata machine ya kutengezea fedha bandia.

Na amesema hivyo ili kuonesha kuwa kuna kazi nyingi tu aliwahi kuzifanya nje ya eneo lake la kawaida la kazi. Hiyo ya kwenda Arusha haikuwa ya kwanza.

Pamoja na hayo, amekanusha kuiba fedha wala kutumia silaha. Kila alichokuwa anakifanya alipata ushirikiano wa vyombo vya dola. Hata aliyekuwa mkuu wa wilaya wa eneo husika alikuwa na taarifa juu ya uwepo wao.

Kwa maneno mengine alikuwa kwenye kazi maalum aliyotumwa na mamlaka ya uteuzi wake: siyo Dr. Mpango, Prof. Luoga au hao wengine aliowataja.
Sio hawaelewi ila wanapotosha makusudi
 
Haya chadema mnajitahidi kupotosha uma kwa kuunda vimada vyenu tumeshamwelewa Sabaya alichomanisha msipotoshe na hizo tuhuma za kupora fedha mnamwekelea
 
Back
Top Bottom