Dkt. Mpango ni kweli ulishiriki kumtuma Sabaya kufanya mambo machafu?

WATUMISHI WA UMMA WOTE

rudisheni pesa za watu zinanuksi hamtakuja maendeleo hata kidogo hela mlizokua mnalipwa mishahara hazikua halali kabisa

Hazina ilikuwa imebaki skeleton kumbe kitambo!! Jaman
 
Watanzania wagumu kweli kuelewa. Kuna upotoshaji mkubwa sana unaendelea. Sabaya amesema alienda Arusha kwa maagizo ya mamlaka iliyomteua.

Prof. Lunga (Gavana) na Dr. Mpango (aliyekuwa Waziri wa fedha) wametajwa kama watu wanaojua moja ya kazi maalum aliyowahi kuifanya huko Dar es Salaam baada ya kukamata machine ya kutengezea fedha bandia.

Na amesema hivyo ili kuonesha kuwa kuna kazi nyingi tu aliwahi kuzifanya nje ya eneo lake la kawaida la kazi. Hiyo ya kwenda Arusha haikuwa ya kwanza.

Pamoja na hayo, amekanusha kuiba fedha wala kutumia silaha. Kila alichokuwa anakifanya alipata ushirikiano wa vyombo vya dola. Hata aliyekuwa mkuu wa wilaya wa eneo husika alikuwa na taarifa juu ya uwepo wao.

Kwa maneno mengine alikuwa kwenye kazi maalum aliyotumwa na mamlaka ya uteuzi wake: siyo Dr. Mpango, Prof. Luoga au hao wengine aliowataja.
Kwahio sisi hatuna masikio? Au ni pambo?
 
Habari za midaa hii wa Jamii forums.

Leo tarehe 13 agosti kumetrendi ktk mitandao ya kijamii kile kinachoitwa no utetezi mahakamani wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya DC Sabaya.

Imeelezwa kuwa amekiri kilichokuwa kikifanyika ama alichokuwa anatekeleza ktk kesi yake ya unyanganyi kwa kutumia siraha aliagizwa na Dr Mpango, Hayati Dr J Magufuli na Gavana wa Fedha bwana Luoga.

Naamini Ndugu Sabaya amefika hatua hii baada ya kuona hakuna namna ya kuchomoka ktk kesi hii au akaona akitupia majina haya Makubwa makubwa itakua ni njia ya nitoke vipi.

Licha ya kile kinachoendelea huko mahakamani iwe ni kweli si kweli, kutajwa kwa Makamu wa Rais Mh Dr Mpango kunatia doa juu ya uhalali ktk utendaji wake kama kweli anaweza kushiriki ktk vitendo vya kihalifu na baafaya akaonekana anafaa kushika nafasi nyeti ktk nchi yetu.

Sisi tunaomuunga mkono na kumwamini kama Kiongozi Safi mwenye weledi na maadili na msomi wa kiwango cha juu tumesikitishwa na kadhia hii ya kutajwa kwenye mambo maovu.

Watanzania tunaompenda tunapenda kutoa wito ajitokeze ama mahakamani au kwenye jukwa la wazi ajisafishe na tuhuma hizi nzito.

View attachment 1891471
Kama waziri wa fedha alikuwa anajua ni lazima makamu wa rais bibi ushungi anajua kila kitu na ndio maana kamteua huyu muha muuaji
 
Mpango ajiuzulu haraka sana , ukiona kiongozi anajifanya Mcha Mungu huku kazungukwa na matunguli muogope sana

Kukamata mitambo ya kutengenezea fedha haramu ni kosa? Msiingie mtego wa Sabaya. Anashindwa kutetea uharibu alioshitakiwa nao kama kubaka, kuteka, na kunyang'anya fedha, makosa ambayo alijifanyia mwenyewe kwa sababu ana hulka za kinyoli. Anababaisha kwa ku site matukio halali ambayo mfumo ulimutuma afanye kwa maslahi ya taifa.

Sabaya ni mjinga. Kukwepa kujibu matukio anayoshitakiwa nayo, kwa kujigundisha kwenye kazi halali, kisheria hakumwondolei wala kuhalalisha personal offences zake. Ni afadhali angejikita kua dress mashitaka yanayomkabiri. Ana implicate serikali na viongozi wake kama kuwadhalilisha ama tufe wengi ama kuwakomoa kwa kuwa hawajamtetea, bila kutambua kwamba ukiwa katika kazi, ukafanya makosa yako binafsi kama kubaka, ama kunyang'anya, matukio ambayo hayahusiani na kazi uliyotumwa, sheria inakuondolea kinga ya kio-office. Huo ni uharifu binafsi. Aki turn hostile, ama aamue kuwahusisha watu wengine, wakiitwa mahakamani watamwuliza, anashtakiwa kwa kosa lipi? Kubaka, kunyang'nya fedha n.k. Je ndiyo kazi walikuwa wamemtuma?
Hakuna mtu asiyejua serikali inaweze kumtumia mtu yeyeote kufanya kazi za serikali kulingana na uwezo wake au mazingira yake ya kufanikisha kazi hiyo kama alivyotumwa na hao WAheshimiwa kukamata mashine ya kufulia fedha, kitu ambacho wala hakiko katika mashitaka.

SIDHANI KAMA MWANASHERIA WAKE NDIYE KAMSHAURI UTETEZI HUO.
 
Habari za midaa hii wa Jamii forums.

Leo tarehe 13 agosti kumetrendi ktk mitandao ya kijamii kile kinachoitwa no utetezi mahakamani wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya DC Sabaya.

Imeelezwa kuwa amekiri kilichokuwa kikifanyika ama alichokuwa anatekeleza ktk kesi yake ya unyanganyi kwa kutumia siraha aliagizwa na Dr Mpango, Hayati Dr J Magufuli na Gavana wa Fedha bwana Luoga.

Naamini Ndugu Sabaya amefika hatua hii baada ya kuona hakuna namna ya kuchomoka ktk kesi hii au akaona akitupia majina haya Makubwa makubwa itakua ni njia ya nitoke vipi.

Licha ya kile kinachoendelea huko mahakamani iwe ni kweli si kweli, kutajwa kwa Makamu wa Rais Mh Dr Mpango kunatia doa juu ya uhalali ktk utendaji wake kama kweli anaweza kushiriki ktk vitendo vya kihalifu na baafaya akaonekana anafaa kushika nafasi nyeti ktk nchi yetu.

Sisi tunaomuunga mkono na kumwamini kama Kiongozi Safi mwenye weledi na maadili na msomi wa kiwango cha juu tumesikitishwa na kadhia hii ya kutajwa kwenye mambo maovu.

Watanzania tunaompenda tunapenda kutoa wito ajitokeze ama mahakamani au kwenye jukwa la wazi ajisafishe na tuhuma hizi nzito.

View attachment 1891471
Wanaonisononesha zaidi ni hawa viongozi wetu wa kidini ambao pamoja na ushetwani na unyama wa Magufuli na serekali yote aliyomrithisha Samia bado wanaendelea bila aibu kuwa nayo bega kwa bega na kuipamba.

Siku ya kiama Mungu aje kuanza na hawa viongozi wa kidini Tanzania wakawe kuni kwenye lile tanuru la moto wa milele!
 
Watanzania wengi ni wagumu kuelewa ama wavivu wa kutafakari.

Sijaona mahala Sabaya akisema Mpango ama Luoga walishiriki kumtuma bali alitumwa na mamlaka yake ya uteuzi na hao jamaa aliowataja wanajua hilo.

Sioni ni kwa namna gani hao jamaa wanahusishwa.
Huko huko kujua ndiko kutawafanya waeleze wanachokijua ili kumnusuru mtumishi wao.
 
Ktk mpira sabaya akifungwa inakuwa ni mbinu ya kutafuta kumpiga miaka mbowe.. Tunaita equalisation la sivyo kuna upande utajipanga kwa maangamizi makali zaidi na bibi atajuta in the end
 
Kama waziri wa fedha alikuwa anajua ni lazima makamu wa rais bibi ushungi anajua kila kitu na ndio maana kamteua huyu muha muuaji
Kosa la Dr. Mpango ni lipi? Naomba muwe mnasoma na kuelewa hoja kabla ya kujiandikia tu. Kutumwa Sabaya kuongoza operation ya kukamata mitambo ya kutengenezea fedha haramu ni kosa? Kwa hiyo mlitaka nchi iachwe watu watengeneze fedha vile wanataka? Hiyo si jinai kama jinai zingine? Sabaya ameshitakiwa kwa kosa la kushiriki ama kufanikisha ukamataji wa mitambo hiyo, tukio ambalo anasema Waziri Mpango na Governor wa BoT walijua? Assignment halali kama hiyo, inakosa gani hadi muwatuhumu Waziri na Governor wa Bank kwa kujua kwao?

Anaposema alitumwa kukamata Mitambo hiyo ambapo hata Governor wa BoT na Waziri wa Fedha wa wakati huo walijua, anakuwa anatoa utetezi wa shitaka lipi hapo huyo Sabaya?
AMEDANGANYWA. Kuacha kujibu mashtaka yanayomkabili na kuanza kuwa implicate viongozi kwa amri halali ambazo walimwagiza afanye na ambazo hazihusiani na mashtaka yake ni hallucination ambayo ni public entertainment tu. Mwambieni ajibu tuhuma alizoshitakiwa nazo. Kama ni kubaka, kunyang'anya fedha, n.k ajitetee vinginevyo anaoga mvua za kkutosha tu.
 
inafikirisha sana. Tunamtaka ajisafishe mimi naamini Ole Sabaya anatafuta pa kutokea. Mambo yamemwia magumu sana.
Atatokea wapi wakati kedhakubali kutenda kosa!? Sana sana atakuwa anajaribu kupata lesser sentence kwa kuwashirikisha hao vigogo.
 
Watanzania wagumu kweli kuelewa. Kuna upotoshaji mkubwa sana unaendelea. Sabaya amesema alienda Arusha kwa maagizo ya mamlaka iliyomteua.

Prof. Lunga (Gavana) na Dr. Mpango (aliyekuwa Waziri wa fedha) wametajwa kama watu wanaojua moja ya kazi maalum aliyowahi kuifanya huko Dar es Salaam baada ya kukamata machine ya kutengezea fedha bandia.

Na amesema hivyo ili kuonesha kuwa kuna kazi nyingi tu aliwahi kuzifanya nje ya eneo lake la kawaida la kazi. Hiyo ya kwenda Arusha haikuwa ya kwanza.

Pamoja na hayo, amekanusha kuiba fedha wala kutumia silaha. Kila alichokuwa anakifanya alipata ushirikiano wa vyombo vya dola. Hata aliyekuwa mkuu wa wilaya wa eneo husika alikuwa na taarifa juu ya uwepo wao.

Kwa maneno mengine alikuwa kwenye kazi maalum aliyotumwa na mamlaka ya uteuzi wake: siyo Dr. Mpango, Prof. Luoga au hao wengine aliowataja.
Watanzania huwa tunachukua maneno juu juu tu
 
Unasema kama ni kweli alimtuma Sabaya kufanya mambo ya hovyo ajitokeze ajisafishe?Yaani badala ya kusema kuwa ajitokeze awajibike unasema kuwa ajitokeze ajisafishe?!Tokea nizaliwe sijawahi kuona akili ndogo kama hii[emoji124][emoji124][emoji124]
Inawezekana lugha aliyoitumia mtoa comment ni kubwa sana kwako. Kujitokeza ajisafishe ni lugha ya heshima ya kumwambia mtu ajitokeze kukana au kukubali hizo tuhuma. Akikana tuhuma ndiko kujisafisha kwenyewe, na akikubali tuhuma, ndipo hoja ya kuwajibika/kukaa pembeni inapoanza kujadiliwa.
 
Watanzania wagumu kweli kuelewa. Kuna upotoshaji mkubwa sana unaendelea. Sabaya amesema alienda Arusha kwa maagizo ya mamlaka iliyomteua.

Prof. Lunga (Gavana) na Dr. Mpango (aliyekuwa Waziri wa fedha) wametajwa kama watu wanaojua moja ya kazi maalum aliyowahi kuifanya huko Dar es Salaam baada ya kukamata machine ya kutengezea fedha bandia.

Na amesema hivyo ili kuonesha kuwa kuna kazi nyingi tu aliwahi kuzifanya nje ya eneo lake la kawaida la kazi. Hiyo ya kwenda Arusha haikuwa ya kwanza.

Pamoja na hayo, amekanusha kuiba fedha wala kutumia silaha. Kila alichokuwa anakifanya alipata ushirikiano wa vyombo vya dola. Hata aliyekuwa mkuu wa wilaya wa eneo husika alikuwa na taarifa juu ya uwepo wao.

Kwa maneno mengine alikuwa kwenye kazi maalum aliyotumwa na mamlaka ya uteuzi wake: siyo Dr. Mpango, Prof. Luoga au hao wengine aliowataja.
mbona unafundisha watu kufanya interpretation mamlaka ya uteuzi si JPM? Kazi ya Dc ni kufanya operation za kukamata watu? polisi wanafanya kazi gani?
 
Watanzania wengi ni wagumu kuelewa ama wavivu wa kutafakari.

Sijaona mahala Sabaya akisema Mpango ama Luoga walishiriki kumtuma bali alitumwa na mamlaka yake ya uteuzi na hao jamaa aliowataja wanajua hilo.

Sioni ni kwa namna gani hao jamaa wanahusishwa.
Wanahusishwa kwasababu wanajua, sasa ili mambi yawe safi wayatolee ufafanuzi haya.
 
Watanzania wagumu kweli kuelewa. Kuna upotoshaji mkubwa sana unaendelea. Sabaya amesema alienda Arusha kwa maagizo ya mamlaka iliyomteua.

Prof. Lunga (Gavana) na Dr. Mpango (aliyekuwa Waziri wa fedha) wametajwa kama watu wanaojua moja ya kazi maalum aliyowahi kuifanya huko Dar es Salaam baada ya kukamata machine ya kutengezea fedha bandia.

Na amesema hivyo ili kuonesha kuwa kuna kazi nyingi tu aliwahi kuzifanya nje ya eneo lake la kawaida la kazi. Hiyo ya kwenda Arusha haikuwa ya kwanza.

Pamoja na hayo, amekanusha kuiba fedha wala kutumia silaha. Kila alichokuwa anakifanya alipata ushirikiano wa vyombo vya dola. Hata aliyekuwa mkuu wa wilaya wa eneo husika alikuwa na taarifa juu ya uwepo wao.

Kwa maneno mengine alikuwa kwenye kazi maalum aliyotumwa na mamlaka ya uteuzi wake: siyo Dr. Mpango, Prof. Luoga au hao wengine aliowataja.
Sang'udi umemuelewa vizuri mtuhumiwa.Inaonekana Sabaya alikuwa kwenye kikosi kazi maalum,ambacho kilikuwa kinapewa maagizo kutoka mamlaka ya uteuzi,lakini huyu mfanyabiashara Mohamed Saad yeye alikuwa na mitambo ya kufyatua Nini? au alikuwa anafanya biashara gani,ambayo mamlaka ya uteuzi ililazimika kutuma kikosi kazi kumfuatilia.Kwa kifupi ,pamoja na Sabaya kuwa alikuwa anapata maagizo kutoka juu,lakini alikosa weledi wakati wa kutekeleza majukumu yake
au alimtumia fursa hiyo kujinufaisha yeye binafsi ,kwa kupitia mgongo wa Mamlaka ya uteuzi.Hili ni funzo kwa Mamlaka za uteuzi kutumia mifumo iliyopo serikalini wakati wa kufanya shughuli zake,(tunalo jeshi la polisi,takukuru,na Usalama wa Taifa) ,ambao wamesomea na Wana weledi katika kutekeleza majukumu yao.
 
Back
Top Bottom