Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Aliyemtuma ni JPM (mamlaka ya uteuzi), sio Mpango. Mpango alijua tu.Afungwe kivipi wakati hakuna ushahidi wa kutosha kumfunga!? Labda Mpango aje Mahakamani aseme hawajawai kumtuma Sabaya kufanya kazi maalumu ya kuwasaka wahujumu Uchumi!!
Swali kubwa: alitumwa kama undercover agent (mtu asiyejulikana) au kama DC? Mbona alikuwa akijinasibu sana kwenye misheni hizo? Hakuwa professional kabisa.
Ajiandae kurukwa na kuangushiwa jumba bovu na hao “wanaojua”. Aliyemtuma ndio hivyo tena. The dead tell no tales. Ni kawaida katika nchi zetu hizi wakubwa kutafuta watu wenye viherehere na kuwapa kazi chafu halafu kuwasakizia mbwa wasipohitajika tena ili wasije wakawa-contaminate. He is expendable.
Sabaya angekuwa smart angejua ile kufutiwa kesi ya kujifanya TISS na kupewa ukuu wa wilaya halafu kuanza kutumwatumwa ovyo tayari wajanja walishamfanya kifaa cha kufanyia kazi chafu. Angeenenda kwa tahadhari sana. Halafu anajua kazi yenyewe alirithishwa na nani. Mwenzake saa hizi anajifanya kama hakuwa yeye ingawa amechafuka kupita maelezo.