Habari za midaa hii wa Jamii forums.
Leo tarehe 13 agosti kumetrendi ktk mitandao ya kijamii kile kinachoitwa no utetezi mahakamani wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya DC Sabaya.
Imeelezwa kuwa amekiri kilichokuwa kikifanyika ama alichokuwa anatekeleza ktk kesi yake ya unyanganyi kwa kutumia siraha aliagizwa na Dr Mpango, Hayati Dr J Magufuli na Gavana wa Fedha bwana Luoga.
Naamini Ndugu Sabaya amefika hatua hii baada ya kuona hakuna namna ya kuchomoka ktk kesi hii au akaona akitupia majina haya Makubwa makubwa itakua ni njia ya nitoke vipi.
Licha ya kile kinachoendelea huko mahakamani iwe ni kweli si kweli, kutajwa kwa Makamu wa Rais Mh Dr Mpango kunatia doa juu ya uhalali ktk utendaji wake kama kweli anaweza kushiriki ktk vitendo vya kihalifu na baafaya akaonekana anafaa kushika nafasi nyeti ktk nchi yetu.
Sisi tunaomuunga mkono na kumwamini kama Kiongozi Safi mwenye weledi na maadili na msomi wa kiwango cha juu tumesikitishwa na kadhia hii ya kutajwa kwenye mambo maovu.
Watanzania tunaompenda tunapenda kutoa wito ajitokeze ama mahakamani au kwenye jukwa la wazi ajisafishe na tuhuma hizi nzito.
View attachment 1891471