Dkt. Mwigulu: Chanjo za Corona zimefanyiwa utafiti nchi za baridi zitawafaaje watu wa Dar es Salaam?

Dkt. Mwigulu: Chanjo za Corona zimefanyiwa utafiti nchi za baridi zitawafaaje watu wa Dar es Salaam?

Anajua factor zinazo tumika wakati wa majaribio au ana ongea tuu maadam yuko mbele ya kamera?

Kuna mambo mengine wana siasa mnatakiwa kukaa kimya.

By the way hakuna chanjo inayo hifadhiwa kwenye moto. Zote huhifadhiwa kwenye fridge.
Yeees!!
 
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360, Waziri Dkt. Mwigulu Nchemba amesema watanzania wanapaswa kujiuliza chanjo za watu wa nchi zenye baridi zinawezaje kuwasaidia watu wa Dar es Salaam kwenye joto.

Mwigulu amesema ndio maana watu waliotoroka wakaenda kuchanja kimya kimya zinawaletea matatizo.

Chanzo: Clouds 360

Maendeleo hayana vyama!
Kwani chanjo ya polio inatengenezwa wapi
 
Tatizo ni jiwe. Amesema Hakuna corona na hatuhitaji chanjo, Sasa haha wengine wameambiWA nendeni mkawambie wananchi hatuhitaji chanjo,,Sasa mtu hata sio fani yako unazungumzia corona kwenye television ya Taifa na kupotosha umma
 
Hvi NIMRI wanafanya nn au nao wanajifukiza? Kwa nn maghufuli asiifute NIMR na kuwafukuza wote kazi ...mpak sa hv hawajaonyesha effort yyte ya wao nao kutafta chanjo ...wamekaa tu kusikiliza matamko ya Wana siasa
Hivi unadhania suala la chanjo ni kazi rahisi tu?!!chanjo za mabusha na matende tu zimewashinda sembuse chanjo ya VIRUS?!!Hii nchi kwa sasa hadi meko atoe kauli ndio , wotee wanalalia huko!huwezi jiuliza juzi tu aliposema mambo ya mask, sasa hivi hata kwenye tv, wale wataalam wa njia tiba mbadala wameanza kuonekana tena!!kwani wameshajua kuwa sasa jamaa amekubali kuwa kuna covid19!!hapo mwanzo wote walikuwa wanaogopa!!
 
Anajua factor zinazo tumika wakati wa majaribio au ana ongea tuu maadam yuko mbele ya kamera?

Kuna mambo mengine wana siasa mnatakiwa kukaa kimya.

By the way hakuna chanjo inayo hifadhiwa kwenye moto. Zote huhifadhiwa kwenye fridge.
Mafusho na nyungu zote zinahifadhiwa kwenye joto kari 😀
 
Shida kubwa ya nchi zetu ni pale wanasiasa wanapoamua kujifanya ni wataalam wa kila kitu na kuwapuuza wataalam, huku wataalam nao wakiamua kujitoa ufahamu kulinda ulaji wao.

Mambo mengine ni aibu kabisa kila mtu sasa anajifanya daktari ilimradi apate la kuongea kumuunga mkono JPM.
Inamaana nchi za baidi kibaiolojia ni tofauti na sisi wa nchi za joto? Na kwa maana hiyo chajo zoote hadi Dawa za Arv ni tofauti?
 
Mambo mengine ni aibu kabisa kila mtu sasa anajifanya daktari ilimradi apate la kuongea kumuunga mkono JPM.
Unazungumziaje maelezo ya mwanasiasa wa uingereza bwana Boris Johnson wakati anatangaza namna ya kuachana na mambo ya lockdown hiyo jana!? Jisomee hapa chini
====
"We cannot persist indefinitely with restrictions that debilitate our economy, our physical and mental well-being, and the life chances of our children." SAYS British Prime minister Boris

"Mwigulu amesema ndio maana watu 'waliotoroka' wakaenda kuchanja kimya kimya zinawaletea matatizo"

Kwahiyo serikali inawaona wale walioenda kupata chanjo ni 'WALITOROKA'.????

Viongozi wamegeuka kama mashabiki wa mpira wa bongo pale timu yao inapokuwa imefungwa ,kila mtu anageuka kocha..

NCHI NGUMU HII...
Wamemtoroka nani? kumbe tuko ndani ya zizi??! Mwigulu alipaswa kujibu hayo maswali
 
Unazungumziaje maelezo ya mwanasiasa wa uingereza bwana Boris Johnson wakati anatangaza namna ya kuachana na mqbo ya lock down iyo jana!? Jisomee hapa chini
====
"We cannot persist indefinitely with restrictions that debilitate our economy, our physical and mental well-being, and the life chances of our children." SAYS British Prime minister Boris

Alifanya vizuri maana maisha lazima yaendelee
 
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360, Waziri Dkt. Mwigulu Nchemba amesema watanzania wanapaswa kujiuliza chanjo za watu wa nchi zenye baridi zinawezaje kuwasaidia watu wa Dar es Salaam kwenye joto.

Mwigulu amesema ndio maana watu waliotoroka wakaenda kuchanja kimya kimya zinawaletea matatizo.

Chanzo: Clouds 360

Maendeleo hayana vyama!

Vipi chanjo za ndui, pepopunda, surua na nyingine nyingi kwa watoto, zilifanyiwa utafiti wapi?
 
Haya mambo ya Corona yasimamiwe na wataalamu wa afya, siyo kila mtu awe msemaji wa Corona. Ni jambo la hovyo sana hata kumuona Bill Gate akizungumzia mambo ya gonjwa hili la Corona na chanjo yake.

Tuliambiwa katika siku za mwisho ni kutoweka kwa amana, na amana inaondoka pindi jambo linaposimamiwa na mtu asiyekuwa mbobezi wa jambo hilo hivyo tusubiri kiyama.
Shida ni kuwa wataalamu wamekaa kimya au wameamua kuacha taaluma zao na kuitikia wimbo ulioanzishwa na wanasiasa kwani wanasiasa ndio wenye fuko la feza. Haiingii akilini daktari mbobevu kama profrsa anadai chanjo haijafanyiwa utafiti wa kutosha wakati huo huo anashadidia dawa ya kienyeji iliyofanyiwa utafiti mwituni - mwituni kwa sababu taratibu za kuipitisha dawa kuwa inatibu lazima ziwe shirikishi kwa wataalamu wa dunia - WHO.
Nadhani kuna jambo linahalalishwa tu - na yawezekana ni kuepuka gharama kwani mkishatangaza kuwa hii ni pandemic basi ni jukumu la serikali kugharamia mapambano.
 
Haya mambo ya Corona yasimamiwe na wataalamu wa afya, siyo kila mtu awe msemaji wa Corona. Ni jambo la hovyo sana hata kumuona Bill Gate akizungumzia mambo ya gonjwa hili la Corona na chanjo yake.

Tuliambiwa katika siku za mwisho ni kutoweka kwa amana, na amana inaondoka pindi jambo linaposimamiwa na mtu asiyekuwa mbobezi wa jambo hilo hivyo tusubiri kiyama.
Tatizo ni kutetea msimamo uliopo bila scientic facts. Ndo maana mtoto akiumwa degedege wengine watasema ni jini, na jini halipimwi kwenye maabara.
Wakati wa vita huwekwa mbele makomandoo wa kijeshi na sio wa kugeuza risasi kuwa maji.
Maneno yamekuwa meengi sana kati hii vita. Tuimbe haka kapambio.
Toooka pepo × 1
Kiitikio: Toka pepoooo x 1
Na kurudia
 
Back
Top Bottom