Dkt. Mwigulu, inakuwaje mnatuambia Miradi ya Hayati Dkt. Magufuli inaendeshwa kwa mikopo mikubwa na migumu kuhimilika?

Yaani kwanza bunge lenyewe, lifanywe ' virtual' tu kupunguza gharama za maposho ya kila siku kwa wabunge, kila mbunge akae kwenye jimboni kwake, na wachangie atakachoona kutokea ofisini kwake.... nafikiri tutasevu pesa nyingi.. kazi iendelee.
Sio kupunguza tu posho wazifutilie mbali tu mana bado wana mishahara minono halafu kuna watumishi wana mishahara kiduchu na posho hawana.
I
 
Aaaaah yako mambo ukiyaangalia... unaukumbuka ule usemi "aljununu fununu" - hata uenda wazimu nao ni fani (kila mmoja anayo namna yake)

Haya shime tuongeze juhudi ya mapambio na vigelegele...

Your browser is not able to display this video.
 
Wabunge wako wanakatwa kodi?
 
Kuhimili usafirishaji wa mizigo mizito reli ni muhimu sana, barabara zetu hazina viwango vya kuhimili presha kubwa ya magari ya mizigo na abiria. Ninachoona hapa waziri yuko desperate ni namna gani hiyo miradi itakamilika ndani ya muda mchache na bila kutumbukiza nchi kwenye madeni makubwa ya mikopo...
 
HII nchi inawalipa kodi wengi sana ila nchi yenyewe iko gizani, na viongozi wako gizani. Natamani ningekutana na mama Samia siku moja ningekuwa na LA kumwambia. Watu tulioko chini ni vigumu sana kuonekana.
 
Hizi ni pamoja na hela za halmashauri, hela ambazo task force ya TRA walikua wanapora kwenye account za wafanyabishara?
 
Hehehe Lugha imeanza kueleweka siku hizi...

Namba inasomeka vyema huko.
 
Mie kwa kweli nilishangaa kwa miradi mikubwa mingi, kuanza kwa pamoja na kutegemea ' smooth ride' kwa nchi maskini kama yetu'.. Wenzetu kwa hizi big projects, huwa wanajaribu kufanya kitu kinaitwa' Projects stagerring' kujaribu kupunguza matatizo kama haya tuliyokumbana nayo ya kutokuwa na uwezo wa smooth project financing......haya bana, kazi iendelee.
 
Naamini tatizo lako laweza kuwa haujawahi kusimamia mradi Wala kujua mradi unavyoendeshwa. Vile vile hujui gharama za kuchelewesha mradi
 
Wewe ni mmojawapo wa watu wajinga tena usiejielewa. Ulaghai kwa vitu ambavyo vinaonekana? kila mradi aliosema na kuahidi, ametekeleza kwa vitendo tena bila kutetereka. Sasa kama warithi wake wameshindwa kukusanya kodi ili wamalizie hiyo miradi, unawezaje kumlaumu yeye?
 
Dingi yenu alikuaga mwongo kichizi.

Hizo 1.9trillion unajumlisha na zile pesa za kubambikia watu makosa ya uhujumu uchumi.

Bure Sana yule dingi.
 
Hizi ni pamoja na hela za halmashauri, hela ambazo task force ya TRA walikua wanapora kwenye account za wafanyabishara?
Taja mfano halisi wa account hata moja na kiasi kilichoporwa pamoja na tarehe husika, kitu ambacho naamini watanzania wengi wanadaiwa malimbikizi ya kodi hivyo kulipa kwa mkupuo inakuwa ni shida.
 
Naamini tatizo lako laweza kuwa haujawahi kusimamia mradi Wala kujua mradi unavyoendeshwa. Vile vile hujui gharama za kuchelewesha mradi

Nilijua tu huna jipya. Maana sioni maelezo ya msingi zaidi ya porojo zilezile.
 
Nilijua tu huna jipya. Maana sioni maelezo ya msingi zaidi ya porojo zilezile.
Hata kama porojo ni zile zile lakini hatujawahi kusikia miradi ikikwama kipindi cha hayati JPM. Na hii imechangiwa kiasi kikubwa na mpango mzuri wa makusanyo
 
Ndugu yangu inaumiza na inakera sana.

Utawala uliopita ulijaa ghiliba sana katika kuendesha nchi. Walisema nchi yetu ni tajiri, na miradi hiyo tunaitekeleza kwa pesa zinazotokana na makusanyo ya mapato yetu ya ndani. Walienda mbali kwa kusema zamani haikuwezekana kwasababu pesa zilikuwa kwa mafisadi, sasa mafisadi yamebanwa na pesa ya miradi inapatikana.

Watanzania wenzetu wengi, wakiwemo wasomi waliamini hiyo kauli ya kitapeli.

Kauli hizo zililenga kujipatia umaarufu wa kisiasa zaidi kuliko uhalisia.

Waziri wa fedha wa wakati huo mara kwa mara alitoa kauli bubgeni kuwa deni letu ni himilivu na kwamba kwa trend ya deni letu la nje bado tuna sifa ya kukopesheka kwa miaka mingine mingi.

Sasa imefika wakati wa sisi wananchi kubebeshwa gharama za madeni bila kujali vipato vyetu.

Wacha cha moto tukione.
 
Acha maneno mengi weka data mezani ili tuamini hiko unachosema
 
si ndo huyu VP ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…