Dkt. Mwigulu Nchemba, acha kuwadharau Watanzania kwa kauli hizi

Dkt. Mwigulu Nchemba, acha kuwadharau Watanzania kwa kauli hizi

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Kuna maneno yanatrend mtandaoni kua Mwigulu anasema kwamba hahitaji kupendwa na wengi wapigakura wake wanatosha kumpenda. Hii ni baada ya bajeti yake kuzua taharuki kubwa kuhusu kuongeza tozo kwenye miamala ya line simu.Anadai kua yeye amependekeza bajeti ili mambo yaende hajali watu wanaumia kiasi gani.

Kama kweli haya maneno ni yake, hiki ni kiburi cha hali ya juu sana hahitaji kua waziri wa fedha. Hatuwezi kua na mtu kwenye wizara nyeti kama ya fedha na kujiona kama Mungu mtu. Hizi dharau si nzuri kwa watanzania, hajawahi kuyaishi maisha magumu ndio maana anatoa kauli hizi ambazo kimsingi hazina tofauti na zile za Albert Chalamila.

"Napendekeza kuongeza ushuru wa miamala na vocha, katika hili nawaonea HURUMA sana watanzania kwa kubebeshwa mzigo, naweza kuwa unpopular minister of finance ila ni lazima mambo yaende. Nikipendwa na wapiga kura wangu na mashabiki wa Yanga inatosha" ~ Mwigulu Nchemba"

20210612_034655.jpg

======

Hilo mbona dogo , hivi uliona body language yake ilivyojaa kibri cha kishamba ?
That is why I say a good finance minister should be an urbanite.
Sio mtu alikua anachunga ng'ombe wa kienyeji leo ndio anatoa mwelekeo wa mapato na matumizi ya nchi.
Huyu anaweza kukaa meza moja na Mtei au Msuya wakanywa chai ?
 
kuna uzi wangu humu nilishaliona hilo kitambo
 
That is why I say a good finance minister should be an urbanite.
Sio mtu alikua anachunga ng'ombe wa kienyeji leo ndio anatoa mwelekeo wa mapato na matumizi ya nchi.
Huyu anaweza kukaa meza moja na Mtei au Msuya wakanywa chai ?
Kwani "Mtei na Msuya walikuwa 'urbanites'"; au una maana gani na neno hilo!

Kiufupi, mchango wako umepoteza lengo kabisa kutokana na uelewa wako finyu unaoonekana katika mstari huo uliouandika hapo.

Kuchunga ng'ombe hakumwondolei uwezo wa uelewa wa mambo mhusika katika jambo lolote lile.

Bado unashikilia 'mentality' ya kijinga jinga sana.

Tafadhali, usinihusishe na kumtetea huyo Kilaza anayejadiliwa hapa. Ukilaza wake hauna uhusiano wowote na uchungaji ng'ombe unaouzungumzia wewe.
 
Hajawahi kuwa na akili wala busara kama yule wa "kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe" naye si alikuwa wizara hiyohiyo!!!? Kwani alitegemea siku moja atanyea debe!!?
 
Nimetaja wanne.
Kwanini uulize Mtei na Msuya tu na kuwaacha Andandangisye Steven na Jamal?

..katika mawaziri wa fedha wa Tz Mtei na Msuya wana rekodi ya kipekee.

..Mtei alikuwa waziri wa fedha wakati wa vita vya kagera.

..Jiulize ni mawaziri wa fedha wangapi wametumikia nchi zao wakati wa vita.

..Msuya alikuwa waziri wa fedha uchumi na mipango mwaka 1985.

..Yeye ndiye aliyeongoza dhamana ya kufufua uchumi mara baada ya Rais Mwinyi kuingia madarakani.

..Kuna wakati Rais Kikwete alisema Msuya ndiye Baba wa mageuzi ya uchumi Tanzania.

NB:

..Edwin Mtei ndiye Baba wa sarafu ya Tz. Yeye ndiye gavana muanzilishi wa Benki Kuu ya Tz.
 
Hiyo wizara kama inakosa watu wa maana bora tu ibaki wazi na bajeti yake awe anakuja kusoma hata karibu mkuu tu, Mwigulu Viatu alivyovalishwa vinampwaya sanaa,Hafeet hata kidogo

Hata wizara zingine namuona yupoyupo tu kazi kusifia sifia hovyo ile agonge teuzi zaid
 
That is why I say a good finance minister should be an urbanite.
Sio mtu alikua anachunga ng'ombe wa kienyeji leo ndio anatoa mwelekeo wa mapato na matumizi ya nchi.
Huyu anaweza kukaa meza moja na Mtei au Msuya wakanywa chai ?
Kwani msuya na mtei ni watoto wa mjini?
 
Mkuu Kwani humjui uyu jamaa ,kwanza uyu ni mpenda sifa ,kujipendekeza, na ana roho mbaya Sana ,cheo kwake Ndo kila kitu

Hawa ndo viongozi ccm wanajivunia kuwa nao hamna kitu pale

Ukiwa waziri unahudumia watanzania wote , Sasa kibri Cha madaraka naona kimefika mahala pake , kwamba wenye nchi sio kitu tena kwake , mwache tu jeuri ,kibri haijawai muacha mtu salama
 
Huyo kalewa madaraka au madaraka yamemzidi kimo kiasi kwamba hajui anachoongea kina madhara gani kwa umma kutokana na ulevi wa madaraka.

Hii haina tofauti na kauli ya Waziri mmoja aliyesema ndege itanunuliwa hata ikibidi watu wale majani, Mwingine aliwaambia watu wenyeshida ya usafiri; you can go to hell, na Mwingine aliwaambia wananchi; kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe, mwingine alipata kuwaambia watu; kama huwezi kulipa basi uvuke kwa kuogelea.

Basi kila awamu inao viongozi walevi wa madaraka, hao hawafai kuongoza watu bali wanyama, na hiyo ni tabia ya mtu aliyechunga ng'ombe utotoni yeye anadhani watu ni ng'ombe au mbuzi aliokuwa akichunga.
 
Back
Top Bottom