Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
DKT. MWIGULU NCHEMBA ASISITIZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI OFISI YA HAZINA NDOGO KIGOMA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ametembelea Ofisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha Mkoani Kigoma na kuzungumza na Watumishi wa Taasisi hizo kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu shughuli za maendeleo na kuwasihi kuendelea kuwajibika kwa weledi.
Mhe. Dkt. Nchemba alitembelea Ofisi ya Hazina Ndogo Mkoani Kigoma, Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kufanya nao mazungumzo ambapo aliwapongeza Watumishi wa Taasisi hizo kwa uwajibikaji wao na kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na kuzingatia kanuni wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Alisema kufuatia juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya jitihada kubwa za kuboresha mazingira ya kuwahudumia wananchi wake hivyo na wasaidizi wake wanatakiwa kufanya kazi kwa kufuata misingi iliyowekwa.
"Serikali inafanya kazi kubwa katika kuwahudumia wananchi na kuweka mazingira wezeshi kwa watoa huduma na kuboresha miundombinu katika sekta zote, tuendelee kutoa huduma kwa wananchi bila upendeleo na kwa wakati" Mhe. Dkt. Nchemba.
Mkuu wa Hazina Ndogo Mkoa wa Kigoma Bw. Frank Msaki alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa inayofanywa katika Kanda ya Kigoma kuhakikisha huduma muhimu kwa wananchi zitapatikana kwa wakati na wao kama wasaidizi wake wataendelea kutoa huduma kwa kufuata misingi ya haki na uwajibikaji.
Kwa ipande wake, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kigoma, Bw. Beatus Nchota alisema usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato katika Mkoa wa Kigoma unatokana na mwitikio mkubwa wa walipa kodi kufuatia elimu ya mlipa kodi wanayoitoa mara kwa mara kwa wafanyabiashara wa Mkoa huo