OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Tanzanialeaks apuuzwe, Hazina haijafilisika
Puuzeni taarifa ya “Tanzanialeaks” Serikali haijafilisika, Ameandika hatujalipa Bwawa - Uongo mtupu, Bwawa la Mwl Nyerere hatudaiwi hata Invoice Moja na Wiki jana tumewasha na mtambo wa 7, ( Sasa tumeshawasha 7, 8 & 9 kila mmoja 235MW). Ameandika kuhusu Yapi, hawa walikuwa na matatizo madogo...
Heshima kwenu wakuu wenzangu
Kama mtambuka juzi kati member wa JF na Waziri wa Fedha alikuja humu kukana kwamba serikali haijapungukiwa uwezo wa kifedha. Hoja yake ilijikita kuonyesha serikali ina uwezo mkubwa na kujiendesha na kutekeleza miradi yake.
Naomba wakuu wa JF wamuarifu kuna jamaa amekataa maelezo aliyotoa, labda arejee tena kutoa maelezo ya ziada kupitia haya nitakayoeleza.
Binafsi kwa utafiti mdogo nilioufanya, nimebaini mambo kadhaa yanayopingana na kanusho la Mwigulu.
1. Serikali kushindwa kufanya malipo kwa wakati
Watumishi wa serikali, wazabuni na wakandarasi mtaungana na mimi, ya kwamba kumekuwa na ucheleweshaji usio wa kawaida wa serikali kufanya malipo. Wenyewe wasema malipo hayajashuka. Unaweza kusubiri malipo kwa zaidi ya miezi mitatu. Wakuu wa taasisi wamekuwa wakinawa kwamba tatizo ni BOT na Mfumo wa Malipo wa Pamoja wa TSA. Upo ushahidi wa wakuu wa taasisi kupitisha malipo kwenye mfumo wa malipo MUSE, lakini yanabaki hewani kwa muda mrefu.
Zipo nyakati ambapo katika mwezi malipo yamekuwa yakiachiwa kidogo tu hasa kuanzia tarehe 15 kuelekea mshahara. Yaani mnanyunyiziwa kidogo tu.
Inasikitisha sana unaidai serikali, umewasilisha kila kitu, imepita hata miaka miwili, halafu unaambiwa hela zipo nyingi tu. Maelezo ya Waziri ni chonganishi kati ya wadai na wakuu wa taasisi. Kwamba wanafanya makusudi kutolipa.
2. Adhabu ya kuchelewesha malipo kwa wakandarasi na mifuko ya pensheni matrilioni ya fedha
Mh.Dkt Mwigulu uje hapa utuambie serikali imekuwa na mambo mengi kiasi cha kusahau kulipa wakandarasi na wazabuni wake, ila mapesa yapo mengi tu.
Kama fedha zipo na hamtaki kulipa kiasi cha kuongeza gharama za malipo, basi wewe na wenzako mnaingiza nchi kwenye hasara kubwa sana. Kama ni hivyo, basi unatakiwa kuachia ngazi mara tu baada ya kumaliza kusoma bandiko hili. Ili tukuonee huruma basi ukiri humu kwamba hamna fedha za kutosha. Tutatunza hii siri hapa JF watu wasisikie.
Hoja yangu hii itashadadiwa na taarifa za CAG kwa mwaka uliopita. CAG ameonyesha madeni makubwa na adhabu za matriloni ya fedha kutokana na serikali kushindwa kulipa kwa wakati. Hali hii ni tete kwa ngazi zote, serikali kuu na LGAs
3. Serikali kutelekeza miradi mikubwa ya maendeleo
Mfano rahisi ni kwamba, unapanga kujenga nyumba, unaishia kusafisha kiwanja tu na kumwaga vifusi ya mchanga, kisha unapotea. Au unafika mpaka kwenye lenta, mafundi wanakomaa na kudai chao,unakimbia na hupokei simu. Maana yake nini, kama sio umefulia?
Ndio hali ilivyo kwa serikali ya Mwigulu. Miradi mingi ya serikali imeshindwa kabisa kutekelezwa licha ya kuwekwa kwenye mpango, na mingine imetekelezwa sehemu ndogo kutokana na ukosefu wa fedha. CAG ameyasema hayo katika taarifa zake. CAG anaendelea kusema, kuchelewa kwa miradi hiyo kunafanya gharama za miradi kuwa kubwa kutokana na ongezeko la gharama ya vifaa na ufundi.
.....nitaendelea, ngoja kwanza niote jua. Moderator mwiteni Waziri Dr. Mwigulu Nchemba