Dkt. Mwigulu rudi tena useme vizuri kanusho la serikali "kufulia"

Dk.amesahau dunia ni ya utandawazi!
Siku zote ukiona mtu fulani anapata title ya kielimu mfano u Dr wakati akiwa na madaraka jua amebebwa!
Kibongo bongo ndivyo ilivyo kwa hivyo usiogope mkuu hiyo ni kawaida sana.
We mheshimu mtu aliyepata wadhifa wa kielimu wakati akiwa nobody kwenye jamii yetu!.
Hao sijui Dr Mwigulu, Dr Jafo, Dr Samia nk nk hamnaga kitu humo...ni mwendo wa connection tuu!!!.
 
Haya ni maneno yale yale ya wabaya wetu alisikika “mheshimiwa” akisema……..
Kuna mwalimu wangu mmoja wa falsafa alikuwa anapenda kusema "Masikini siku zote huamini kila mtu anamchukia na kumdharau"

Ilhali unakuta tajiri yuko busy na mambo yake ila masikini anawaza kuwa tajiri hampendi na anataka aendelee kumdidimiza kumbe unakuta hata hayuko akilini mwa tajiri.

Hawa watu wakiwa nyumbani wanaita mabeberu wakienda nje wanaenda kukopa na msafara wa watu.

Halafu mabeberu hao hao wanatujengea hadi vyoo.!!!
 
Wazabuni na wakandarasi toka mwaka jana wanalia njaa malipo hakuna sasa wao kodi na 'other statutory obligations' wanalipa vipi nchi inapata wapi kodi kwa mwendo huo ajira mpya zitatengenezwa vipi mishahara inalipwaje? Kukauka kwa hazina kuko bayana mpaka mfuko wa barabara (Road fund) hauna kitu sio kwaida hii.
 
Miradi mingi inasuasua tu
 
Sasa hivi wanaiba vifurushi vya data , , wanaiba ukinunua umeme. Tanzania tunaongozwa na vibaka tupu waliotumia fursa ya katiba nzee kufungia bao la mkono, wameanza kutafuta hela za kampeni feki za kanga na kofia na boksa za kuwapa walala hoi, huku wahesabu kura na wanaotangaza wakipewa ahadi, na hela za kulipa vikoba
 
Mimi kama Mtumishi wa Serikali nimepandishwa Daraja la Mshahara mwezi uliopita nimekuwa "Principal Grade IC" na Mfumo wa ESS unanitambua hivyo na mshahara napata. Sasa hayo mengine mi sijui!
 
Mwasibu umeshusha vitu vizito asee, hoja inajibiwa na vielelezo na sio porojo. Chawa wapite mbali huu Uzi sio level yao huu moto wa Mzee wa fedha
 
Unachoshindwa kuelewa ni kwamba Ufafanuzi wa Dr Mwigullu PhD ni wa kisiasa siyo wa kifinance

Taasisi yoyote inayoshindwa kujiendesha kwa Bajeti yake ya ndani ni Mufilisi na hiyo siyo Dhambi 😄😄
Umeongea points
 
Haya ni MADHARAU. huku ma vi8 yakibugia mafuta tu
 
Wakati wa msiba wa Captain Gardner, nilisikia Kasesela akihojiwa. Dah Ile kauli hadi leo naitafakari sipati jibu. Alisema nyakati za jambo fulani linatrend kuhusu serikali yeye of course na wenzake anaowajua yeye walikuwa watamtumia marehemu ku-spin mambo. Dah Ile kauli hadi leo naitafakari ni jinsi gani watawala wanatufanya wazumbukuku. Kifupi hawataki wananchi kuhoji lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…