Dkt. Mwigulu rudi tena useme vizuri kanusho la serikali "kufulia"

Hivi huko kufulia kunakosemwa hakuwezi kupelekea kusimama au kucheleweshwa kwa utekelezaji wa miradi ya DMDP? Mwaka huu benki ya dunia ilitoa mabilioni kwa ajili ya mradi wa bonde la Msimbazi, barabara za jijini, ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali, masoko, stendi kadhaa, maeneo ya wazi na daraja la pale Jangwani ambapo miradi yote hii ingetekelezwa na serikali kupitia DMDP. Hiyo fedha yake haitachepushwa kweli ili kukabiliana na ufuliaji ulioikumba serikali hadi kushindwa kulipa mishahara, stahiki za watumishi, wakandarasi na wengineo kwa wakati?
 
Umeua sooooo!!!!
 
Uchepushaji wa mafungu unawezekana hasa kwa awamu hii wanasema wakandarasi fedha za mfuko wa barabara hazipo kitu ambacho sio cha kawaida
 
Uchepushaji wa mafungu unawezekana hasa kwa awamu hii wanasema wakandarasi fedha za mfuko wa barabara hazipo kitu ambacho sio cha kawaida
Mbona wakandarasi wamesima wanalipwa!? mpaka.wameamua kumpatia mama zawadi! au mnazungumzia wakandarasi wa Kenya?
 
Kwa hivyo kupata mshahara wa laki Saba umejiona umefika na kudharau mambo ya msingi ya nchi.
Hapana. Ila najaribu kuonesha ya kwamba mtoa hoja ni muongo. Malipo mbalimbali ya Serikali yanaendelea kutolewa tena kwa wakati. Na nilichoonesha ni mfano mdogo tu. Daraja la Magufuli pale Busisi ujenzi umepamba moto. Ujenzi wa SGR hapa Mwanza Mjini ndio usiseme hadi Kiwanda Cha Samaki Cha Vic Fish kimeanza kubomolewa wiki hii kupisha ujenzi. Nini mnataka madogo?
 

Mwigulu ameshasema jamaa wa Stiglers hadai hata mia
 
Mbona wakandarasi wamesima wanalipwa!? mpaka.wameamua kumpatia mama zawadi! au mnazungumzia wakandarasi wa Kenya?
Wakandarasi gani wanalipwa hao magumashi utakatishaji wa pesa mfuko wa barabara (Road fund) umekauka hauna pesa madeni toka mwaka jana wanalia wakandarasi wengine wamekopa Bank wakilipwa walipe madeni dhamana zao ziko sokoni mpaka muda huu​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…