Dkt Nchimbi: CCM imekasirishwa sana na mauwaji ya Ali Kibao na serikali iharakishe haraka uchunguzi na matukio yakomeshwe

Sasa yakomeshwe vp na mtu wameshamjuwa na hatuoni hatua hatua kwanza ichukuliwe hata ya kunyonga hao watu ndo iwe fundisho kwa wengine
Huko twitter kwa motto balaaa, huyo MTU anayeitwa mafwere ndio nani? Naona Watu wanatuma email kwenye Shule anayosoma binti yake huko South Africa
 
Kumbe ndio huyu?
 
Hivi Mafwele akiuawa kutokana na tuhuma hizi Boniface Jacob hatokuwa mshukiwa namba moja??Hivi watoto wake wakidhuriwa Bonoface Jacob atakuwa hajahusika?
Namshauri Mafwele amfingulie kesi boniface Jacob mara moja
Mafwele hawezi kufungua mashitaka popote hapa duniani, maana anajijua ni muhalifu, na akitia pua tu mahakamani ushahidi wa uhalifu wake uko wazi peupe. Kama huamini namba zake ziko hapo. Mpigie simu mshauri aende mahakamani, tena uzuri ni mahakama za ccm, chama hiki hiki kinachomtuma kuua wapinzani. Uoene kama atathubutu. Auye kwa upanga naye lazima auwawe kwa upanga.
 
Mh. Dkt Nchimbi na Mwenyekiti wanashindwa kuelewa upepo wa wananchi. Nadhani uwezo wao wa kufikiria umekuwa mdogo kiasi kwamba hawatambui na kuchambua. Nilitegemea Mh. Dkt Nchimbi na Dkt Samia cha kwanza ilikuwa kumuondoka IGP, Waziri wa mambo ya ndani halafu uchunguzi uendelee. Na hicho ndicho Mh. Mbowe anakitaka. Vingine hivi ni porojo tu. CCM yetu inaharibiwa na watu kutokufuata ushauri
 
Mbowe alimpigia simu Nchimbi mara tano? Kwa umuhimu upi na lengo gani? Kwa kutaka nini hasa?
 
Mtu katili na hatari sana huyu
 
Huu ni uwongo!
 
Futuhiiiiiiiii ndiyo ni FUTUHI.
 
Hivi Mafwele akiuawa kutokana na tuhuma hizi Boniface Jacob hatokuwa mshukiwa namba moja??Hivi watoto wake wakidhuriwa Bonoface Jacob atakuwa hajahusika?
Namshauri Mafwele amfingulie kesi boniface Jacob mara moja
Kwani Jackob amesema mafwele akipotea asiulizwe? Yule uvccm aliyesema wakiwapoteza watu polisi wasihangaike alichukuliwa hatua gani?
 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema chama hicho hakiwezi kuvumilia matukio ya utekaji na uvunjifu wa amani na hakitakubali.

Mbali na hilo, Dk Nchimbi ametaka vyama vya upinzani ikiwemo Chadema kuungana pamoja kukemea, kukataa kufarakanishwa juu ya matukio ya utekaji na amepuuza taarifa za mitandaoni zinazolenga kuwahusisha viongozi wa Chadema na utekaji, mauaji.

Pia, CCM imelaani tukio la kutekwa na kuuawa kwa Mjumbe wa Sekeretarieti ya Chadema, Ali Kibao kikisisitiza hilo halikubaliki.

Kibao alitekwa Septemba 6, 2024 na watu wenye silaha eneo la Kibo Complex, Tegeta jijini Dar es Salaam akiwa kwenye basi la Tashriff akienda nyumbani kwake mkoani Tanga.

Mwili wake uliokotwa siku iliyofuata eneo la Ununio, Dar es Salaam ukiwa umeharibika na inaelezwa uso wake ulimwagiwa tindikali.

"Mtu yoyote anayehatarisha usalama wa raia, anayeteka raia au kikundi chochote kinachohatarisha usalama kinaharibu taswira ya CCM," amesema.

Dk Nchimbi amesema hayo leo Ijumaa, Septemba 13, 2024 alipozungumza na wahariri na waandishi wa habari, ofisi ndogo za CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Katika maelezo yake Dk Nchimbi amesema: "Tumemsikia Mwenyekiti wa Chadema, (Freeman) Mbowe akitoa mwelekeo wa chama chake kuwa kitachukua hatua. Nikiri Mbowe ni rafiki yangu, lakini Mbowe amefikishwa hapo na genge la utekaji?"

Dk Nchimbi amesema amekutana na Mbowe hivi karibuni katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi, Bakari Machumu: "Na Mbowe alinieleza juu ya suala la Kibao, kwa kumtazama Mbowe hahusiki na tukio hili la utekaji."

 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Nchimbi ameeleza kuwa CCM inaunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa uchunguzi ufanyike ili kubaini wahusika.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wandishi wa habari leo Septemba 13, 2024 katika Ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi Lumumba, Dar es salaam
Your browser is not able to display this video.
 
Katibu mkuu umeupiga mwingi. Jinsi wafuasi wa Mbowe wanavyopingaga kila kitu sijui kama na hii kauli ya katibu mkuu wa CCM wataipinga..😄
Wewe unaungaunga mkono Kila kitu.

Sasa hapo huoni anawapiga dongo nyie wananadharia njama (Conspiracy theorists) mnaoshinda kuzua mitandaoni kuwa CHADEMA wanatekana wenyewe Kwa wenyewe na tuhumu zenu huwa mnazielekeza Kwa Mbowe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…