Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Maendeleo aliyoleta Rais Samia kwa miaka 3 Madarakani ni kama miujiza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ukishakuwa chawa huwezi kutumia akili.

Hivi nchi zote duniani raisi anaabudiwa namna hii? Mbona tunakuwa watu wa namna hii, kusifu kila kitu, hatuwezi kuwa objective hata kidogo.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€›
 
Kuna mida ifike hizi kauli zenu zitoke kwa kujua kwamba watanganyika siyo mazuzu - wanajua kusoma na kuandika walau.
 
Huyu nae ni chawa tu wa Samia. Kwa kua kapewa cheo na mwenyewe ni mroho wa madaraka ndio anaona rais kaleta maeneleo makubwa. Et anasifia makusanyo ya TRA kuongezeka wakati tunajua shilingi imeshuka thamani kwa hivyo hela kama sio ileile itakua imepungua mtu akilinganisha thamani halisi. Maisha ya wavuja jasho yanaendelea kua magumu. Hospitali za serikali huduma ghali utafikiri ni za binafsi. Madaktari wameachwa kuendesha biashara ya matibabu kwa kutumia uwekezaji wa umma. Rushwa imeongezeka polisi na mahakama wamegeuza kazi zao kampuni zao binafsi kujipatia kipato kikubwa huku wanapewa mishahara kutoka hazina ya taifa. Nchimbi aache ulaghai hayo aliyotaja kwanza mengi ni miradi ya awamu ya 5 na mengine ni kazi za kawaida tu za serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…