Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Maendeleo aliyoleta Rais Samia kwa miaka 3 Madarakani ni kama miujiza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Magufuli alifanya yapi sasa?
Au hajawahi kufanya chochote?
Kikwete je?
Mkapa je?
Mwinyi je?
Mwalimu ?
Ccm angalieni cha kuwaambia watanganyika
 
Huwezi kusema kilichopangwa kilikuwa kidogo bali hata wao wanaona Kwa kulinganisha huko nyuma hakuna Rais ametekeleza Ilani Yao Kwa Ukubwa kumzidi Samia na sio sifa ila ndio uhalisia wenyewe.
Kwahio kinachofanyika sasa ni Miujiza na wakiomba waendelee kuwepo ni muendelezo wa hii hii Miujiza ? (More of the Same) ?

Nadhani Kitaa ukiwaambia hivi watakwambia Ugumu wa Maisha umeongezeka Leo ni Mbaya afadhari ya Jana sasa kama watumishi wetu wanaona kwamba leo ni nzuri (miujiza) nachelea kusema either they are out of touch au wanaridhika na mediocrity...
 
Wapumbavu ni wale wana excuse incompetence ya nyumbani kwao na kuibeba rwanda kuwa ni special
Incompetence iko Chadema kwenye Maridhiano ya Jina la NEC

CCM inazidi kuleta maendeleo yaliyotukuka πŸ˜‚πŸ˜‚

Wapumbavu ni wale wanaoandamanishwa na akina Halima James Mdee
 
Ni lini ugumu wa Maisha uliwahi pungua.Pili as days go on lazima ugumu wa Maisha ni lazima maisha Hayajawahi Kuwa rahisi au wewe unaijua Nchi ambayo maisha ni rahisi hapa Africa?
 
Wapumbavu ni wale wana excuse incompetence ya nyumbani kwao na kuibeba rwanda kuwa ni special
Kwani wanaosemaga Rwanda imeendelea Huwa mnatumia vigezo gani wakati hiyo ni LDC na mfumuko wa bei uko Juu?
 
Magufuli alifanya yapi sasa?
Au hajawahi kufanya chochote?
Kikwete je?
Mkapa je?
Mwinyi je?
Mwalimu ?
Ccm angalieni cha kuwaambia watanganyika
Tzn ni kubwa na mahitaji ni mengi na makubwa,Kila mtu alifanya Kwa sehemu yake na mengine hakuna ambae alifanya anafanya Samia naenhatofanya yote.

Mfano kwani huko Marekani mambo ya kufanya yameisha? Kama wao Wana miaka zaidi ya 200 hawajamaliza kufanya how comes Tzn yenye miaka 60 iwe imemaliza?

Mwisho maendeleo ni mchakato safari Moja huanzisha nyingine.Kiongozi anapimwa Kwa kutimiza yake aliyokubaliana na wapiga kura(Ilani) akikamilosha huyo amefanya.
 
Tunasifiana kwa fedha za mkopo, wacha zifanye kazi kusudiwa. Ila muda wa kulipa tusione tunaonewa tutake uvunja mkataba.
Nchi gani haikopp hapa Duniani? By the way Kati ya Bajeti ya zaidi ya Trilioni 40,mikopo haizidi Trilioni 10.

Mikopo sio hisani itarudishwa na Kodi na sio Kila Nchi inapata mikopo inayohitaji.

Mwisho Tanzania ingekopa zaidi Ili kufungua Uchumi,tuko nyuma sana kwenye kukopa ndio maana tunakamua maskini,tutachelewa kufika.
 
Nikajua unaandika kihaki kumbe kishabiki! Nilipoona kuna mtu unamuita Dhalimu nikaona kumbe na wewe ni chawa tu ambaye ukitaka kumsifia mmoja lazima umponde mwingine. Stupid 100%
 
Ni lini ugumu wa Maisha uliwahi pungua.
Haya maneno hawa wana-Siasa wangeyasema wakati wanaomba Kura ili waende Kula hakuna mtu angepiga Kura bali angelala nyumbani kwake..., kwahio unataka kuniambia Trajectory ya Maisha lazima yaendelee kuwa magumu siku baada ya siku..., Kwamba Watumwa kipindi kile kesho yao ingebidi iwe ngumu zaidi ?
Pili as days go on lazima ugumu wa Maisha ni lazima maisha Hayajawahi Kuwa rahisi au wewe unaijua Nchi ambayo maisha ni rahisi hapa Africa?
Urahisi ninaongelea mimi ni Basic Needs mtu awe na uwezo wa kujipatia Malazi, Mavazi na Chakula na uwezo huo ni ujira wa kutosheleza hayo..., kwa Serikali yoyote au yoyote anayelipwa ili aongoze akishindwa kufanya hivyo ni kwamba in my books hajafanikiwa..... Niki-qoute Hotuba ya TANU ya Mwalimu.....

  • CHAMA CHETU KINASEMA - mtu mwenye Afya ambaye tumeshindwa kumpa njia halali ya kujipatia riziki yake. Nawaomba ardhi - hakuna ardhi; hamnipi ardhi, Mnasema "Ardhi hakuna". Naomba kazi ya kibarua basi, Nipeni basi ya kibarua, "Hamnipi kazi ya kibarua. Mimi niko tayari kabisa kufanya kazi au ya kulima au ya kibarua chochote nipeni. Hamnipi Chama Chetu kinasema MTANILISHA.
 
Hizo basic needs watu wanaweza kuzipata sana tuu sijui wapi Tanzania hii watu wanalalia mlo.mmja Kwa siku wakati vyakula bei ni chee.
 
Nikajua unaandika kihaki kumbe kishabiki! Nilipoona kuna mtu unamuita Dhalimu nikaona kumbe na wewe ni chawa tu ambaye ukitaka kumsifia mmoja lazima umponde mwingine. Stupid 100%
Basi natoka neno dhalimu naweka Magufuli,jibu hoja
 
CCM hamjawahi kuishiwa vibweka.Ni rais gani mliwahi kutuambia hajafanya maajabu kimaendeleo halafu akitoka mnamponda?You,people,are full of magical ways of lying!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Basi natoka neno dhalimu naweka Magufuli,jibu hoja
Kwa kuwa umeshamkashfu JPM inaonekana umekaa kiubishi tu, huwezi kuwa serious ukaona maendeleo ya Samia kwa miaka 3 ni bora kuliko ya JPM ya miaka5....hapo kiubishi mada itaendelea ila kiakili hakuna kitu cha kuongea hapo. Hao wanaoongea hivo wanatetea nafasi zao tu, ukiwauliza wapiga kura ni asilimia mdogo saaaaaana watamtaja Samia kimaendeleo.
 
Hizo basic needs watu wanaweza kuzipata sana tuu sijui wapi Tanzania hii watu wanalalia mlo.mmja Kwa siku wakati vyakula bei ni chee.
Nadhani fanyia kazi hapo kwenye Bold......; unaongelea mlo mmoja watu wanatoka asubuhi kwenda kutafuta shilingi hawajui hata kama jioni menu itasoma..., watu wana-madeni mpaka kwenye kope yaani wanakopa leo walipe madeni ya miezi mitatu nyuma na waendelee kudaiwa miezi sita mbele ili tu leo waweze kula.....

Kwa statement yako huenda hata huyu Nchimbi yupo out of touch - Ndio hawa ukiwaambia watu wanalalamika hawana maji ya kunywa wanakwambia waambie wanywe Wine....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…