Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mgombea Mwenza wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema iwapo CCM itashinda uchaguzi wa mwezi October, Serikali ya Chama hicho itatenga shilingi Bilioni 200 na kuzitoa kama mikopo ya Vijana na Wajasiriamali Nchini.
Nchimbi amesema sambamba na hilo, pia watarasimisha shughuli za Wajasiriamali wadogo ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika uchumi wa Taifa.
Akizungumza akiwa katika mkutano wa kampeni Wilayani Siha, Mkoani Kilimanjaro, Dkt. Nchimbi pia ametangaza mpango wa kuanzisha mfumo wa mawasiliano kati ya Wananchi na Serikali, utakaomwezesha kila Mtanzania kufikisha kero na mahitaji yake moja kwa moja kwa Mamlaka husika.