PreGE2025 Dkt. Ndumbaro ataja sababu kuzuiwa kwa Martha Karua kutoka Kenya, na wenzake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro amesema mawakili kutoka Kenya waliozuiwa kuingia nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania.

Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Mei 20, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Jijini Dodoma.

Amesema walichokuwa wanakuja kukifanya hapa nchini ni uvunjifu wa sheria za Tanzania jambo ambalo halikubaliki.

"Kwa uelewa wangu wale hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania, kwa hiyo wanachokuja kukifanya ni uvunjifu wa sheria zetu lakini kwa nini waje kwetu wakati kwao yamewashinda, nyumba yako inawaka moto unataka kuuzima kwa jirani? huu ni unafiki. Na sisi Watanzania hatutaki unafiki, kwenye eneo la haki za binadamu tupo vizuri sana na naungana na Rais Samia kwenye kauli yake ya jana," amesema Ndumbaro.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amesema mawakili kutoka Kenya waliozuiwa kuingia nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania.

Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Mei 20, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Jijini Dodoma.

Amesema walichokuwa wanakuja kukifanya hapa nchini ni uvunjifu wa sheria za Tanzania jambo ambalo halikubaliki.

"Kwa uelewa wangu wale hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania, kwa hiyo wanachokuja kukifanya ni uvunjifu wa sheria zetu lakini kwa nini waje kwetu wakati kwao yamewashinda, nyumba yako inawaka moto unataka kuuzima kwa jirani? huu ni unafiki. Na sisi Watanzania hatutaki unafiki, kwenye eneo la haki za binadamu tupo vizuri sana na naungana na Rais Samia kwenye kauli yake ya jana," amesema Ndumbaro.
Huyu mheshimiwa atakuwa kiazi kabisa! Shughuli ya uwakili haifanyiki uwanja wa ndege. Maafisa uhamiaji hawakagui leseni za uwakili. Haikuwepo sababu ya kuwazuia kuingia Tanzania. Wangekataliwa mahakamani kama hawana leseni ya uwakili.
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro amesema mawakili kutoka Kenya waliozuiwa kuingia nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania.

Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Mei 20, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Jijini Dodoma.

Amesema walichokuwa wanakuja kukifanya hapa nchini ni uvunjifu wa sheria za Tanzania jambo ambalo halikubaliki.

"Kwa uelewa wangu wale hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania, kwa hiyo wanachokuja kukifanya ni uvunjifu wa sheria zetu lakini kwa nini waje kwetu wakati kwao yamewashinda, nyumba yako inawaka moto unataka kuuzima kwa jirani? huu ni unafiki. Na sisi Watanzania hatutaki unafiki, kwenye eneo la haki za binadamu tupo vizuri sana na naungana na Rais Samia kwenye kauli yake ya jana," amesema Ndumbaro.

Upuuzi tupu.

1. Ikiwa Watanzania tuliwasaidia watu wa ANC ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Makaburu kule nchini Afrika Kusini.
2. Ikiwa Watanzania pia tuliwasaidia watu wa ZANU ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wazungu (Waingereza) kule nchini Zimbabwe.
3. Aidha, ikiwa Watanzania vile vile pia tuliwasaidia watu wa FRELIMO ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wareno kule nchini Msumbiji.

Je, ni kwa nini basi majirani zetu wa Kenya au Uganda nao wasiwe na Haki ya kuwasaidia Wananchi wa Tanzania ili waweze kuondokana na Utawala dhalimu na usiitenda Haki wa CCM hapa nchini sawa sawa kabisa na vile ambavyo waTanzania walifanya kwa majirani zao wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji?

Remember:
"Injustice somewhere is a threat of justice everywhere."
By Martin Luther King Jr.

HAKI haina mipaka, wala Haki haijali mipaka ya nchi.

Good for the Jews is good for the gunners, and bad for the Jews is also bad for the gunners.
 
Mmh🤔🤔🤔, hawa ndiyo CCM sasa, walioshiwa pumzi kabisa...

Tunasema mara kwa mara kuwa, hii serikali chini ya CCM ya Chura Kiziwi inakabiliwa na tatizo kubwa la kisaikolijia linaloitwa low self-esteem linalozaa tatizo jingine la fear of unknown...

Just see here, iwapo tu ulichokiripoti hapa ni sahihi

Kwamba, hapa Waziri haeleweki anatoa sababu gani specific...

1. Je, hawakuwa na leseni za uwakili
au​
2. Walikuja kuleta vurugu na uvunjifu wa amani...?

Kama hiyo 👆👆👆ni sababu, how exactly ilikuwa walete vurugu na uvunjivu wa amani...?

Watu hawa (serikali & CCM) wana hofu/woga ambao hata wao wakiulizwa mnaogopa nini hasa, obvious hawawezi kueleza au kuwa na majibu sahihi ya kumwambia mtu timamu akawaelewa..!

Watu wanaokabiliwa na tatizo la fear of unknown, humwona kila mtu anayekatiza mbele yao ni adui anataka kuwadhuru au kutwaa utawala wao...!

Hii ni hatari sana, kwani, watu wenye tatizo hili huishia kufanya maamuzi ya hovyo na yenye madhara kwao wenyewe na kwa wengine pia...

Mathalani;

#Sina hakika kama Martha Karua na wenzake walikuja kama "mawakili wa Tundu Lissu"

#Tunachofahamu Martha Karua na wenzake kama wanachama wa East Africa Law Society, walikuja kufuatilia kesi ya mwanachama mwenzao Tundu Lissu..

#Labda, wanahofia kilichotokea Kenya mwaka Jana huko Kenya na kutaka kuiangusha serikali ya William Ruto...
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro amesema mawakili kutoka Kenya waliozuiwa kuingia nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania.

Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Mei 20, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Jijini Dodoma.

Amesema walichokuwa wanakuja kukifanya hapa nchini ni uvunjifu wa sheria za Tanzania jambo ambalo halikubaliki.

"Kwa uelewa wangu wale hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania, kwa hiyo wanachokuja kukifanya ni uvunjifu wa sheria zetu lakini kwa nini waje kwetu wakati kwao yamewashinda, nyumba yako inawaka moto unataka kuuzima kwa jirani? huu ni unafiki. Na sisi Watanzania hatutaki unafiki, kwenye eneo la haki za binadamu tupo vizuri sana na naungana na Rais Samia kwenye kauli yake ya jana," amesema Ndumbaro.

Kwa nini waziri wa sheria anajibu suala la kisheria kwa kusema "kwa uelewa wangu...".

Na kama hawana leseni ya kumtetea Tundu Lissu, kwa nini muwazuie kuingia nchini, kwa nini msiwaachie waingie nchini halafu muwakataze kumtetea Tundu Lissu?

Wapi kina Karua wamesema wanakuja kumtetea Tundu Lissu?

Are our ministers this dumb?
 
Huyu mheshimiwa atakuwa kiazi kabisa! Shughuli ya uwakili haifanyiki uwanja wa ndege. Maafisa uhamiaji hawakagui leseni za uwakili. Haikuwepo sababu ya kuwazuia kuingia Tanzania. Wangekataliwa mahakamani kama hawana leseni ya uwakili.
We have so many minerals in our country, but what you presented is an extraordinary mineral, haya ndio madini, stay blessed. Nilijua tu mama amezunguukwa na tabaka la watu wanaomdanganya na huu ni mfano hai. Yeoyote mwenye facts za kwamba Karua alikua anakuja kumwakilisha Lissu Mahakamani aje na ushahidi hapa na sio kuwahadaa watanzania.
Karua ni mwanasheria mbobezi hawezi kufanya ujinga huo eti atoke kenya aje amwakilishe mteja wake haiwezekani jamani.
Kumbukeni watanzania sio wajinga. Boss wetu hii ngoma ni nzito tusiichukulie kiwepesi. Nashauri kama huna majibu ya kisomi please just remain silent and enjoy your evening cup of coffee.
Naikumbuke upo umoja wa mawakili katika nchi za umoja wa afrika mashariki.
Kwa muktadha huu, kwenye mikataba ya kitaifa bado tutapigwa sana.
 
Kwa ni i wqziri wa sheria anajibu suala la kisheria kqa kusema "kwa uelewa wangu...".

Na kama hawana leseni ya kumtetea Tundu Lissu, kwa nin8 nuwazuie kuingia nchibi, kwq nini msiwaachie waingie nchini halafu muwakataze kumtetea Tundu Lissu?

Wapi kina Karua wamesema wanakuja kumtetea Tundu Lissu?

Are our ministers this dumb?
Amejipa kazi ya mahakama, huyu mzee ni mjinga sn
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro amesema mawakili kutoka Kenya waliozuiwa kuingia nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania.
Wachezaji na makocha wa kigeni huwa wanaingia kwanza nchini then wanafanyiwa utaratibu wa vibali vya kufanya kazi wakiwa tayari Bongo.
 
Back
Top Bottom