PreGE2025 Dkt. Ndumbaro ataja sababu kuzuiwa kwa Martha Karua kutoka Kenya, na wenzake

PreGE2025 Dkt. Ndumbaro ataja sababu kuzuiwa kwa Martha Karua kutoka Kenya, na wenzake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu mheshimiwa atakuwa kiazi kabisa! Shughuli ya uwakili haifanyiki uwanja wa ndege. Maafisa uhamiaji hawakagui leseni za uwakili. Haikuwepo sababu ya kuwazuia kuingia Tanzania. Wangekataliwa mahakamani kama hawana leseni ya uwakili.
Itifaki unazijua wewe? Kwahiyo kama angelikuwa ni askari mercenaries wangeachwa kwanza mpaka wakutwe msituni na silaha ndio wakamatwe sio? Wewe bonge la jiniasi!!!
 
Ebu tusidanganyane....
Hakuna mgeni aliekua anakuja kumtete Lisu mahakamani, bali wageni walikuja kusikiliza kesi ya Lisu mahakamani.
Hii nchi mbona mnatuona wajinga sana hata mtoe majibu mepesi kwenye mambo ya msingi kana kwamba kila raia ni kilaza...☹️
 
Upuuzi tupu.

1. Ikiwa Watanzania tuliwasaidia watu wa ANC ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Makaburu kule nchini Afrika Kusini.
2. Ikiwa Watanzania pia tuliwasaidia watu wa ZANU ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wazungu (Waingereza) kule nchini Zimbabwe.
3. Aidha, ikiwa Watanzania vile vile pia tuliwasaidia watu wa FRELIMO ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wareno kule nchini Msumbiji.

Je, ni kwa nini basi majirani zetu wa Kenya au Uganda nao wasiwe na Haki ya kuwasaidia Wananchi wa Tanzania ili waweze kuondokana na Utawala dhalimu na usiitenda Haki wa CCM hapa nchini sawa sawa kabisa na vile ambavyo waTanzania walifanya kwa majirani zao wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji?

Remember:
"Injustice somewhere is a threat of justice everywhere."
By Martin Luther King Jr.

HAKI haina mipaka, wala Haki haijali mipaka ya nchi.

Good for the Jews is good for the gunners, and bad for the Jews is also bad for the gunners.
Kumbuka ata kupindua serikali akukubaliki...Unakumbuka tulimfukuza Zitto baada ya kujua anataka kumpindua kamanda Mbowe. ILINDI NCHI YAKO TANZANIA..Naona mnataka kutumiwa kama baadhi ya walibya walivyotumiwa na NATO.KIKOWAPI
 
Ebu tusidanganyane....
Hakuna mgeni aliekua anakuja kumtete Lisu mahakamani, bali wageni walikuja kusikiliza kesi ya Lisu mahakamani.
Hii nchi mbona mnatuona wajinga sana hata mtoe majibu mepesi kwenye mambo ya msingi kana kwamba kila raia ni kilaza...☹️
Walipewa homework na SSH jana ili waje kutufungasha kwa uongo kama huo.Bloody shenzizzz!🫸🫷😜😜😜😜😜😜😜
 
Ebu tusidanganyane....
Hakuna mgeni aliekua anakuja kumtete Lisu mahakamani, bali wageni walikuja kusikiliza kesi ya Lisu mahakamani.
Hii nchi mbona mnatuona wajinga sana hata mtoe majibu mepesi kwenye mambo ya msingi kana kwamba kila raia ni kilaza...☹️
Leta ushahidi wako hapa kuhusu ilo...Hakuna nchi inayoweza kuruhusu ujinga wa hivyo.Nendeni mkamtetee na yeye kua alishinda uchaguzi dhidi ya Ruto
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro amesema mawakili kutoka Kenya waliozuiwa kuingia nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania.

Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Mei 20, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Jijini Dodoma.

Amesema walichokuwa wanakuja kukifanya hapa nchini ni uvunjifu wa sheria za Tanzania jambo ambalo halikubaliki.

"Kwa uelewa wangu wale hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania, kwa hiyo wanachokuja kukifanya ni uvunjifu wa sheria zetu lakini kwa nini waje kwetu wakati kwao yamewashinda, nyumba yako inawaka moto unataka kuuzima kwa jirani? huu ni unafiki. Na sisi Watanzania hatutaki unafiki, kwenye eneo la haki za binadamu tupo vizuri sana na naungana na Rais Samia kwenye kauli yake ya jana," amesema Ndumbaro.

Sema sisi sisiem, na sio watanzania
 
Huyu ni mwana Siasa tu Ikulu ina wanasheria waliotukuka
Huyu si msomi wa sheria na mshauri wa Rais upande wa sheria? ukiwa mwana siasa ndiyo unakuwa mpumbavu na mpotoshaji? ndiyo maana nchi haijawahi kushinda nje kwenye kesi sababu ya kuwa na wasomi wapumbavu jamii ya huyu mzee
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro amesema mawakili kutoka Kenya waliozuiwa kuingia nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania.

Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Mei 20, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Jijini Dodoma.

Amesema walichokuwa wanakuja kukifanya hapa nchini ni uvunjifu wa sheria za Tanzania jambo ambalo halikubaliki.

"Kwa uelewa wangu wale hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania, kwa hiyo wanachokuja kukifanya ni uvunjifu wa sheria zetu lakini kwa nini waje kwetu wakati kwao yamewashinda, nyumba yako inawaka moto unataka kuuzima kwa jirani? huu ni unafiki. Na sisi Watanzania hatutaki unafiki, kwenye eneo la haki za binadamu tupo vizuri sana na naungana na Rais Samia kwenye kauli yake ya jana," amesema Ndumbaro.

Huyu ni Dr (PhD)???
 
Back
Top Bottom