PreGE2025 Dkt. Ndumbaro ataja sababu kuzuiwa kwa Martha Karua kutoka Kenya, na wenzake

PreGE2025 Dkt. Ndumbaro ataja sababu kuzuiwa kwa Martha Karua kutoka Kenya, na wenzake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu mheshimiwa atakuwa kiazi kabisa! Shughuli ya uwakili haifanyiki uwanja wa ndege. Maafisa uhamiaji hawakagui leseni za uwakili. Haikuwepo sababu ya kuwazuia kuingia Tanzania. Wangekataliwa mahakamani kama hawana leseni ya uwakili.
Alijuaje kama wanakuja kufanya uwakili??
 
Kwa ni i wqziri wa sheria anajibu suala la kisheria kqa kusema "kwa uelewa wangu...".

Na kama hawana leseni ya kumtetea Tundu Lissu, kwa nin8 nuwazuie kuingia nchibi, kwq nini msiwaachie waingie nchini halafu muwakataze kumtetea Tundu Lissu?

Wapi kina Karua wamesema wanakuja kumtetea Tundu Lissu?

Are our ministers this dumb?
Ukiona hivyo ujue hana akili kabisa

Wale ni wanachama wa Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki.

Hawakuwa hapa kufanya kazi ya Uwakili , walikuwa hapa kama Wanasheria ku observe shauri la Mwanachama wa Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki.

Ndumbaro ana shida sana kichwani kwake.
 
Huyo
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro amesema mawakili kutoka Kenya waliozuiwa kuingia nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania.

Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Mei 20, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Jijini Dodoma.

Amesema walichokuwa wanakuja kukifanya hapa nchini ni uvunjifu wa sheria za Tanzania jambo ambalo halikubaliki.

"Kwa uelewa wangu wale hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania, kwa hiyo wanachokuja kukifanya ni uvunjifu wa sheria zetu lakini kwa nini waje kwetu wakati kwao yamewashinda, nyumba yako inawaka moto unataka kuuzima kwa jirani? huu ni unafiki. Na sisi Watanzania hatutaki unafiki, kwenye eneo la haki za binadamu tupo vizuri sana na naungana na Rais Samia kwenye kauli yake ya jana," amesema Ndumbaro.

Huyo ni chawa anasema asichokiamini
 
Upuuzi tupu.

1. Ikiwa Watanzania tuliwasaidia watu wa ANC ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Makaburu kule nchini Afrika Kusini.
2. Ikiwa Watanzania pia tuliwasaidia watu wa ZANU ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wazungu (Waingereza) kule nchini Zimbabwe.
3. Aidha, ikiwa Watanzania vile vile pia tuliwasaidia watu wa FRELIMO ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wareno kule nchini Msumbiji.

Je, ni kwa nini basi majirani zetu wa Kenya au Uganda nao wasiwe na Haki ya kuwasaidia Wananchi wa Tanzania ili waweze kuondokana na Utawala dhalimu na usiitenda Haki wa CCM hapa nchini sawa sawa kabisa na vile ambavyo waTanzania walifanya kwa majirani zao wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji?

Remember:
"Injustice somewhere is a threat of justice everywhere."
By Martin Luther King Jr.

HAKI haina mipaka, wala Haki haijali mipaka ya nchi.

Good for the Jews is good for the gunners, and bad for the Jews is also bad for the gunners.
Wewe ni kiazi

USSR
 
Back
Top Bottom