Dkt. Samizi atembelea na kukagua miradi ya barabara na madaraja iliyojengwa kwa fedha za Serikali

Dkt. Samizi atembelea na kukagua miradi ya barabara na madaraja iliyojengwa kwa fedha za Serikali

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
DKT. SAMIZI ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA BARABARA NA MADARAJA ILIYOJENGWA KWA FEDHA ZA SERIKALI YA RAIS SAMIA.

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Mkoani Kigoma Mhe. Dkt Florence George Samizi kipindi hiki cha mapumziko ya Bunge ameendelea kufanya ziara Jimboni kwa kufanya shughuli za maendeleo, kutembelea na kukagua miradi pamoja na kusikiliza na kutatua kero za Wananchi ili kutekeleza vyema Ilani ya CCM.

Leo Jumamosi Oktoba 18, 2022, Dkt. Samizi akiwa na Wataalamu wa TARURA wametembelea miradi ya miundombinu ya barabara na madaraja na kujionea kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Rais Samia kwa kutoa Mamilioni ya fedha kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo (Enabel).

Wananchi wamemwaga pongezi nyingi saana Kwa Rais Samia kwa ujenzi wa Daraja la kuvuka Mto Malagarasi linalounganisha Kata ya Kumsenga na Kata ya Kitanga Jimbo la Kasulu Dc, hivyo shida ya kuvuka na kamtumbwi itakwisha kwa Wananchi na sasa wataweza kusafirisha mazao, wenyewe ,wagonjwa, mifugo n.k

Mhe. Dkt. Samizi akizungumza na Wafugaji wa Kijiji cha Kumlela kata ya Mabamba walifurahia sana daraja la Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwani sasa mifugo yao inapita vizuri kwenye daraja.

#KaziInaendeleaMuhambwe.
IMG-20221008-WA0057.jpg
IMG-20221008-WA0058.jpg
IMG-20221008-WA0059.jpg
IMG-20221008-WA0060.jpg
IMG-20221008-WA0055.jpg
IMG-20221008-WA0056.jpg
IMG-20221008-WA0054.jpg
IMG-20221008-WA0053.jpg
IMG-20221008-WA0051.jpg
IMG-20221008-WA0052.jpg
 
Ndiyo maana wana-africa mashariki wanatudharau Kwa UJINGA...mtoa mada wewe ni lofa
 
Ameona dr samiz amepost mwenyewe na kujipiga mapicha yeye mwenyewe
 
Back
Top Bottom