Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Pasco,

Shein amwondoe mwanasheria mkuu kwa kosa gani? Kwa kuitetea katiba ya Zanzibar aliyoapa kuilinda? Mimi ntamshangaa sana Shein, manake yeye ndo anatakiwa kufutwa kazi kama atakwenda Dodoma kuipokea katiba inayoivunja katiba ya Zanzibar aliyoapa kuilinda.

Hata maccm yaliyopitisha hii katiba yao, mi naona kama vile yapo sahihi manake yanalinda yao waliyoapa kuyalinda...
 
nimekuelewa ndani ya mistari, naona una furaha sana, kusubiri kitu kingine kikitokea mbele. asante. tusubiri kesho siku maalumu kwa taifa hili ambalo J.k anazindua azimio la kifo cha ccm(azimio la Dodoma).
 
Pasco kile unachopenda siyo kila mtu anakipenda kwa hiyo tumia neno katika nafsi yako siyo kuwakilisha watu wote. watu wengi haipendi hiyo bora katiba kama ulivyoiita maana ni kweli bora katiba bila kuzingatia maslahi ya Watanzania kwa maana ya Wazanzibar na Watanganyika
Kwa hiyo yeye ametetea maslahi ya wanzanzibar kama alivyotumwa wewe ndiye unajitia kimbelembele bila kujua unatetea maslahi gani.
Ule unaita upuuzi wa Mwanasheria wa Zanzibar kwa wengine ni mambo ya muhimu sana aliyofanya na kwa sasa ni shujaa kule Zanzibar kuliko hawa wengine wasaka tonge waliokaa na kushangilia bora katiba upuuzi mtupu.
Mtu anayejua nini maana ya Katiba na Katiba bora inapatikanaje hasingekaa pamoja na Wasaka tonge kuandika bora katiba bila kujali maslahi ya umma wa Watanganyika na Wazanzibar.
Ndiyo maana bora katiba hii au rasmu haramu. Ni watu wachache wenye maslahi binafsi na wanye uwezo wa kufikiri kwa karibu bila uzalendo watashabikia kitu iki umekiita bora katiba. Pasco
 
Last edited by a moderator:
Pasco

Kwa hicho ulichokiandika hapo nilipoweka RED kimemfurahisha sana Samweli Sita kwani ndicho hasa kilichotokea.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza niaze na mashahihisho kwa mtoaji wa mada. Kilichopitishwa Dodoma na wabunge wa bunge maalumu siyo katiba mpya bali ni rasimu ya katiba inayopendekezwa. Ni makosa makubwa kuiita kuwa ni katiba wakati mpaka sasa inakosa uhalali wa kisiasa na kisheria kuitwa katiba.

Kumfuta kazi mwanasheria mkuu wa zanziber kitakuwa ni kitendo kinachoweza kufanywa na mwendawazimu tu kwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanziber aliapa kuilinda katiba ya Zanzibar. Rasimu inayopendekezwa inavunja katiba ya Zanzibar kitendo ambacho mwanasheria yeyote makinni wa Zanzibar hawezi kuikubali rasimu hiyo. Nitamshangaa atakayemfuta kazi mwanasheria huyo kwa kufanya wajibu wake wa kuinda katiba ya Zanzibar. Ndiyo maana ninasema atakayemfuta kazi atakuwa mwendawazimu asiyetambua katiba ya Zanzibar na kilichoandikwa kwenye rasimu ya katiba inayopendekezwa.
Naomba kuwasilisha hoja hiyo
 
" " hizi ni alama muhimu sana kwenye mabandiko ya Pasco. Wahenga walisema umdhaniaye ndiye siye
 
Last edited by a moderator:
Washabiki wa UKAWA inabidi wasusie Mchakato kama walivosusia Wajumbe wao! Haingii akilini Tundu Lissu asuse hata kupiga kura Bungeni halafu tukutane nae kwenye Mistari ya Kupiga kura za Maoni ya kupitisha au kukataa Katiba.
 
Kwanza niaze na mashahihisho kwa mtoaji wa mada. Kilichopitishwa Dodoma na wabunge wa bunge maalumu siyo katiba mpya bali ni rasimu ya katiba inayopendekezwa. Ni makosa makubwa kuiita kuwa ni katiba wakati mpaka sasa inakosa uhalali wa kisiasa na kisheria kuitwa katiba.

Kumfuta kazi mwanasheria mkuu wa zanziber kitakuwa ni kitendo kinachoweza kufanywa na mwendawazimu tu kwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanziber aliapa kuilinda katiba ya Zanzibar. Rasimu inayopendekezwa inavunja katiba ya Zanzibar kitendo ambacho mwanasheria yeyote makinni wa Zanzibar hawezi kuikubali rasimu hiyo. Nitamshangaa atakayemfuta kazi mwanasheria huyo kwa kufanya wajibu wake wa kuinda katiba ya Zanzibar. Ndiyo maana ninasema atakayemfuta kazi atakuwa mwendawazimu asiyetambua katiba ya Zanzibar na kilichoandikwa kwenye rasimu ya katiba inayopendekezwa.
Naomba kuwasilisha hoja hiyo

Nimemuomba asome uzi wangu huu labda utampa mwanga kidogo

https://www.jamiiforums.com/katiba-...mwanasheria-zanzibar-ni-msimamo-wa-shein.html
 
Mkuu kama una elimu ndogo usipende nyuzi za Pasco tena ukiwa umesimama.

Daaaah! Wengi wameingia kichwa kichwa! Pasco,ye' anawaangalia tu,wanavyomparamia,bila kugundua kuwa yupo upande wao!!
 
Last edited by a moderator:
Zanzibar will prevail whatever the changamoto ,and everything will be okay !Katiba imekwama na haina pa kutokea hilo shimo la panya alilochimba Sita ,litamwagiwa maji kidogo tu litamomonyoka na mapanya yafie humohumo mengine yakitoka ymekowa.
 
wakimfuta leo, kesho yake utamsikia amekuwa kiongozi fulani chama cha upinzani na watakoma. hawawezi kufanya hilo kosa, litakuwa kosa kubwa sana litakalowagarimu. yeye ameshachukua credit mbele za watu na hakuna wa kumuadibisha.
 
Pasco
Sijasoma content ila heading tu, nauliza kakosea nini? Au mzimu wa kukataa utumwa ndo afutwe kazi kweli?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom