Kwanza niaze na mashahihisho kwa mtoaji wa mada. Kilichopitishwa Dodoma na wabunge wa bunge maalumu siyo katiba mpya bali ni rasimu ya katiba inayopendekezwa. Ni makosa makubwa kuiita kuwa ni katiba wakati mpaka sasa inakosa uhalali wa kisiasa na kisheria kuitwa katiba.
Kumfuta kazi mwanasheria mkuu wa zanziber kitakuwa ni kitendo kinachoweza kufanywa na mwendawazimu tu kwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanziber aliapa kuilinda katiba ya Zanzibar. Rasimu inayopendekezwa inavunja katiba ya Zanzibar kitendo ambacho mwanasheria yeyote makinni wa Zanzibar hawezi kuikubali rasimu hiyo. Nitamshangaa atakayemfuta kazi mwanasheria huyo kwa kufanya wajibu wake wa kuinda katiba ya Zanzibar. Ndiyo maana ninasema atakayemfuta kazi atakuwa mwendawazimu asiyetambua katiba ya Zanzibar na kilichoandikwa kwenye rasimu ya katiba inayopendekezwa.
Naomba kuwasilisha hoja hiyo