Pre GE2025 Dkt. Slaa afikishwa mahakamani Kisutu kwa Shtaka la kusambaza taarifa za Uongo

Pre GE2025 Dkt. Slaa afikishwa mahakamani Kisutu kwa Shtaka la kusambaza taarifa za Uongo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Dr Slaa hakutaja usalama wa Taifa wa nchi gani.

Ndio tujue wanasiasa wanacheza na akili zetu.

Hii kesi Dr anashinda asubuhi.
Na ile mipesa ya mama B12 achomoki sema tu mama ataki kuwafunga wazee. Anajua tu ni njaa tu inasummbua! Miogo kila siku ,haaaa
 
Sala ya kilatini sio ya kiswahili tena?mungu wenu anasikia haraka kwa lugha ya kilatini
Tunanena kwa lugha ambayo shetani haielewi baada kushukiwa na Roho mtakatifu. Inaweza kuwa kilatini, kipare,kisukuma,kichaga au kihaya.
 
Daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaiangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza ni nini cha kufanya na taarifa kamili zitatolewa baadaye," - Kamanda Muliro.
Kwa zamani wangesema" Yule anayejiita Daktari"

😅😅😅
 
Wakuu

Kama muonavyo picha

View attachment 3197638Mwanasiasa mkongwe, Wilbroad Slaa (76) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shtaka moja la kusambaza taarifa za uongo katika mtandao wa X (zamani twitter).

Dk Slaa amefikishwa mahakamani hapo leo Januari 10, 2025 na kusomewa kesi ya jinai namba 993 ya mwaka 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.
View attachment 3197644
Mapema leo Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alithibitisha kumshikilia Dk Slaa.

"Daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaiangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza ni nini cha kufanya na taarifa kamili zitatolewa baadaye," - Kamanda Muliro.

Taarifa ya kukamatwa kwa Dk Slaa imesambaa kupitia mitandao ya kijamii, ikisikika sauti ya mwanasiasa huyo akizungumza kuhusu kukamatwa na Jeshi la Polisi na kwamba anapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mbweni, Dar es Salaam.

Soma:

- Dkt. Slaa akamatwa usiku huu nyumbani kwake Mbweni

- Jeshi la Polisi: Tumemkamata Dkt. Slaa, tunamhoji na kuangalia mifumo ya Sheria
Samia anazidi kujichafua ndani na nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom